kanisa la kwanza duniani ni lipi?

kanisa la kwanza duniani ni lipi?

Maana ya kanisa ni “walioitwa” kwahiyo watu walioitwa watoke sehemu fulani wanaitwa kanisa…..Hivyo tafsiri ya kanisa sio jengo kama inavyodhaniwa na wengi…

Kwahiyo katika maandiko kanisa la kwanza lilianza siku ile ya PENTEKOSTE. Roho Mtakatifu aliposhuka juu ya watu! Soma Matendo Mlango wa pili yote.

Wale waliomwamini Yesu, na kubatizwa walishukiwa na Roho Mtakatifu, na hivyo Roho huyo huyo aliwaongoza kukusanyika pamoja kwa lengo la kujifunza Neno ambalo Mitume ndio waliokuwa wanalifundisha,  pia walidumu katika kushiriki meza ya Bwana, katika kufanya ushirika na katika  Kusali. Hayo mambo manne ndiyo yaliyokuwa yanafanyika katika kanisa la kwanza.

Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu

39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.

40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi.

41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.

42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali”.

(Hilo ndilo kanisa la kwanza)

Kanisa katoliki llinalosemekana kama kanisa la kwanza, hilo ilikuja kuzaliwa mwaka wa 325 Baada ya Kristo. Ambalo hilo lilikuwa kinyume na kanisa la kweli la Kwanza la Pentekoste.

Kanisa katoliki, ni kanisa la uongo kwasababu halikudumu katika hayo mambo manne hapo juu… halidumu katika fundisho la Mitume kama kanisa la Kwanza,  fundisho la Mitume linasema tusiabudu sanamu na pia linasema mpatanishi kati ya  Mungu na mwanadamu ni mmoja tu Yesu Kristo, wakati kanisa katoliki linaamini Mariamu pia ni mpatanishi…..

Pia kanisa katoliki halidumu katika kumega mkate, kwani mwenye ruhusu ya kushiriki ni Padre tu! peke yake jambo ambalo ni kinyume na maandiko, pia halidumu katika kufanya ushirika wala kusali…Sala zinazofanywa ni za desturi za kipagani, kusalia rozari na sanamu jambo ambalo kanisa la kwanza halikufanya. Maombi ya moja kwa moja kwa Mungu hayatiliwi mkazo, na zaidi ya yote maombi ya masafa marefu hayapo kabisa ndani ya kanisa katoliki.


Mada Nyinginezo:

MARIAMU NI NANI?

UHURU WA ROHO.

JE! BIKIRA MARIA NI MALKIA WA MBINGUNI?

JE! NI SAHIHI KUMUITA MARIA MAMA WA MUNGU?


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

9 comments so far

InnoPosted on11:35 um - Julai 2, 2022

Kiufupi mmekuwa mkiokoteza sababu kiasi kwamba mmefikia hatua mpaka mnaonekana kama malimbukeni mnaoutafuta umaarufu kupitia ujuaji na uongo wenu. Hapa ni wenye akili ndogo kama ya kwako ndo wanaweza wakawa wamekuelewa upuuzi uloandika.. Mnatapatapa hamjui mfanye kipi muache kipi.

John wanjalaPosted on9:58 um - Juni 23, 2022

The adventist church has been rejected with many people..but i came to know that it is the only church that leads her people to JESUS CHRIST for preaching the 3 angels massage to all men.

John wanjalaPosted on9:53 um - Juni 23, 2022

Catholic is the mother of harlots.

AsiyejulikanaPosted on9:34 mu - Desemba 25, 2021

Endeleeni kupotoshwa…tatizo la wengi hawaijui kisawa sawa kanisa katoliki.. (the essence of catholic church ndio maana mnatapa tapa tu…mnalibeza bure kanisa la watu. Kwasababu auna idea nalo na kama unayo basi ni kidogo.

AsiyejulikanaPosted on12:08 um - Septemba 2, 2021

kanisa katoliki ndilo lilkua la kwanza

Patrick barasa onyangoPosted on11:59 mu - Desemba 17, 2020

Kanisa katoliki lilikuwa hata kabla ya yesu kukuja duniani, ndilo lililomsulubisha yesu. Na baada ya yesu. Likaendelea kupinga injili likidhani litaizimisha, na baada ya kushindwa, likajiunga na kanisa la kweli, ili liweze kupinga injili kisiri. Na likaweka makao makuu kule roma. Kuanzia hapo roho mtakatifu akaondoka hapo.likabaki kanisa la kimwili. Na ndio mwanzo wa makanisa mengi hapa duniani.

AsiyejulikanaPosted on12:44 um - Desemba 5, 2020

n kweli fafanua

AsiyejulikanaPosted on4:28 um - Desemba 1, 2020

Acheni uongo kanisa katoliki lilianza tu baada ya Kristo kufufuka. Mitume walianza kusali wakiumega mkate. Hujui kabisa historia ya kanisa katoliki

Leave a Reply