Ni Muhimu kufahamu kama Je kujipamba ni dhambi? au kujichubua ngozi ni dhambi? kama kuchonga nyusi ni dhambi, kupaka lipstick ni dhambi na kama kupaka wanja ni dhambi?
Kiuhalisia Kujipamba kunahusisha kupaka rangi uso, kujichubua ngozi, kuchonga nyusi, kupaka lipstick, kupaka wanja, kupaka hina,kusuka nywele, kuvaa hereni, bangili, na mikufu, kuweka kucha za bandia, kuweka nywele za bandia (wigi), kujipulizia marashi makali.
Watu wengi hususani wanawake hawapendi kuambiwa ukweli, kutokana na kwamba wanahofia wataonekana wamepitwa na wakati. Lakini ukweli ni kwamba kujipamba ni DHAMBI, Tena ni dhambi ambayo inawapeleka wanawake wengi kuzimu, na wanaume baadhi wanaofanya hayo..
Katika Biblia kulikuwepo na mwanamke mmoja tu ambaye alikuwa anajipamba…Na huyo si mwingine zaidi ya mwanamke Yezebeli..
2Wafalme 9:30 “Hata Yehu alipofika Yezreeli, Yezebeli akapata habari; akatia uwanja machoni mwake, akapamba kichwa chake, akachungulia dirishani”.
Mwanamke huyu biblia inasema alikuwa mchawi…na aliwakosesha sana wana wa Israeli na alimsumbua sana Nabii Eliya. Na alienda kuzimu! kwasababu anaonekana tena katika kitabu cha Ufunuo kutajwa kama Nabii wa Uongo, na Manaabii wa Uongo pamoja na wachawi, na waabudu sanamu wote biblia imesema sehemu yao ni katika lile ziwa la moto. Kasome (Ufunuo 2:20)
Na biblia inasema miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, hivyo hatuwezi kulifanya hekalu la Mungu kuwa nyumba inayofanana na nyumba za makahaba. Na Neno linasema mtu akiliharibu hekalu la Roho Mtakatifu, Mungu naye atamharibu mtu huyo.
1Timotheo 2:9 “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; 10 bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu”.
1Timotheo 2:9 “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
10 bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu”.
Hivyo kujipamba kwa aina yoyote ile ni dhambi.. kusuka nywele ni dhambi, kujichubua ngozi ni dhambi, kuchonga nyusi ni dhambi, kupaka lipstick ni dhambi, kupaka wanja ni dhambi nk Mwanamke anapaswa ajiweke katika hali yake ya asili, kadhalika na wanamume pia..Ni wajibu wetu wote kujiweka safi na nadhifu, lakini si kuharibu uhalisia.
Mungu akubariki.
Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
+225693036618/ +225789001312
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789 001312.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
WEWE NI HEKALU LA MUNGU.
NI KWA JINSI GANI MUNGU ANAPATILIZA MAOVU YA BABA ZETU SAWASAWA NA KUTOKA 20:5-6?
AMPOKEAYE NABII KWA KUWA NI NABII, ATAPATA THAWABU YA NABII; MSTARI HUU UNAMAANA GANI?.
SHETANI ANATOLEA WAPI FEDHA, ANGALI TUNAJUA FEDHA NA DHAHABU NI MALI YA BWANA?
ASKOFU MKUU NA MCHUNGAJI MKUU NI NANI?
Rudi Nyumbani:
Print this post
mungu wangu
ni kumuomba MUNGU akusaidie tu unajua wanawake weng jehanan inasubiri ,ukiwaambia unaonekana hulijuw NENO
Bwana akubariki.
thanks so mach
Amen, Be blessed
Mungu atusaidie sana
ndio..
Bwana Yesu asifiwe! Je kusuka nywele zangu za asili bila kuongeza na za bandia ni dhambi? Mbona Biblia inasema mwanamke akiwa na nywele ndefu ni utukufu kwa mumewe?
ni kweli iyi
Pembe ndogo ina maana gani ktk unabii
pembe ndogo inamwakilisha mpinga kristo