Swali: Biblia inasema kuwa Bwana Yesu atawahukumu walio hai, na waliokufa (2Timotheo 4:1)
Jibu: Turejee..
2Timotheo 4:1 “Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, ATAKAYEWAHUKUMU WALIO HAI NA WALIOKUFA; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake”..
Maneno kama haya yanarudiwa tena katika kitabu cha 1Petro 4:5
1Petro 4:5 “Nao watatoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu WALIO HAI NA WALIOKUFA”.
Zamani na hata sasa, ipo imani ya kwamba mtu akishakufa ndio tayari “kashahukumiwa” hakuna tena hukumu huko aendako.. maana yake mitihani aliyopitia akiwa duniani tayari ni hukumu tosha, hakuna tena hukumu baada ya kifo.
Lakini Biblia inatufudisha jambo jingine tofauti na hilo, kwamba watu wote ambao wamekufa pasipo kujalisha wamekufaje siku ya mwisho watafufuliwa na Bwana YESU na kuhukumiwa..
Yohana 5:25 “Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai. 26 Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake. 27 Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu. 28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. 29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu”.
Yohana 5:25 “Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai.
26 Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake.
27 Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu.
28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.
29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu”.
Soma pia Mathayo 11:24 utaona kuwa hata baada ya hukumu ya moto ya Sodoma na Gomora bado watu wa miji hiyo watasimama tena kuhukumiwa katika siku ya mwisho..
Kwahiyo hukumu si ya walio hai tu, bali watu wote, (walio hai na waliokufa)..
Je umempokea YESU?.. Kumbuka sasa anasema nasi kama Mwanakondoo, lakini siku ya mwisho atakuwa ni Mhukumu.. wakati mlango wa Neema utakapofungwa, hakutakuwa na nafasi nyingine ya kutubu wala kupokea wokovu, bali kitakachokuwa kimesalia na hukumu..
Ufunuo 20:11 “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. 12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao”.
Ufunuo 20:11 “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.
12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao”.
Mpokee YESU leo, kama bado hujafanya hivyo.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
Fahamu maana ya Mithali 21:3 Kutenda haki na hukumu Humpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka.
Nini maana ya Hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma?
ITAFAKARI SIKU YA HUKUMU.
NIFANYE NINI ILI NIIKWEPE HUKUMU.
Kuna hukumu za aina ngapi?
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ