Swali: Bwana YESU alikuwa na maana gani aliposema “Nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu”?
Jibu: Turejee..
Yohana 12:32 “Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu”.
Kuinuliwa juu kwa Bwana YESU, kupo kwa namna mbili (02), namna ya kwanza ni “KUINULIWA MSALABANI” na namna ya pili ni “KUINULIWA NA WINGU kwenda mbinguni”.
Tuangalie maana moja baada ya nyingine..
1. KUINULIWA MSALABANI.
Hii ndio maana ya kwanza kabisa ya “Kuinuliwa kwa Bwana YESU”.. Na kunafananishwa na wakati ule Musa alipomwinua nyoka wa shaba jangwani, ili kila mtu amtazamapo apone..
Yohana 3:14 “Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; 15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye”.
Yohana 3:14 “Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;
15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye”.
Kwa nguvu ile ile iliyowavuta watu wenye majanga ya kuumwa na nyoka jangwani, ndio nguvu hiyo hiyo iliyoachiwa pale msalabani, kwamba kila mtu mwenye mzigo wa dhambi na vifungo, autazamapo msalaba wa Bwana YESU kwa ufunuo, basi atapata msaada wa kufunguliwa kutoka katika dhambi, magonjwa na kila aina ya mateso ya ibilisi.
2. KUINULIWA NA WINGU.
Hii ni maana ya pili ya kuinuliwa juu kwa Bwana YESU, kulikotoa nguvu ya kuwavuta watu kwa Mungu..
Turejee Matendo 1:8..
Matendo 1:8 “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. 9 Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, AKAINULIWA, wingu likampokea kutoka machoni pao”.
Matendo 1:8 “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
9 Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, AKAINULIWA, wingu likampokea kutoka machoni pao”.
Kwa namna gani au kwa njia gani, baada ya kuinuliwa Bwana YESU juu katika wingu watu walivutwa kwake na hata sasa tunavutwa kwake, si kwa njia nyingine zaidi ya Roho Mtakatifu.
Kwasababu alisema baada ya kupaa kwake atashuka Roho Mtakatifu, ambaye huyo ataushuhudia ulimwengu kwa habari ya dhambi, haki na hukumu (Yohana 16:8).
Kupitia nguvu za Roho Mtakatifu, siku ile tu ya Pentekoste aliposhuka watu elfu tatu walimwamini Bwana YESU na nguvu zake, uamsho mkuu ambao mitume hawajawahi kuuona, hiyo ni kuonesha kuwa ahadi ya Mungu (yaani Roho Mtakatifu), ina nguvu zaidi ya vitu vyote.
Zekaria 4:6 “Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, BALI NI KWA ROHO YANGU, asema Bwana wa majeshi”.
Je Neno la msalaba umelitii??.. Umesamehewa dhambi?.. umeoshwa dhambi zako kwa damu yake?.. je umekimbilia msalabani upate wokovu?
1Wakorintho 1:18 “Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. 19 Kwa kuwa imeandikwa, Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, Na akili zao wenye akili nitazikataa”.
1Wakorintho 1:18 “Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.
19 Kwa kuwa imeandikwa, Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, Na akili zao wenye akili nitazikataa”.
Mwamini YESU leo kama bado haujafanya hivo, na tubu kwa kumaanisha dhambi na ubatizwe.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii..
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MANENO SABA YA YESU MSALABANI.
YESU MNAZARETI, ANWANI YA MSALABA.
MSALABA NI ZANA YA UJENZI WA MAISHA YAKO.
Je! Bwana Yesu alisulubiwa juu ya msalaba au juu ya mti uliokuwa wima?
TAFUTA UTAKASO WA SEHEMU KUU NNE ZA MWILI WAKO.
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ