SWALI: Naomba kufahamu,Yale maneno yanayookana juu ya msalaba wa Bwana Yesu (I.N.R.I) yana maana gani, Nimekuwa nikiyaona kwenye picha za msalaba lakini siyaoni mahali popote kwenye biblia?.
JIBU: Tukisoma kitabu cha Yohana sura ya 19 mstari wa 19-20 inasema..
“Naye Pilato akaandika anwani, akaiweka juu ya msalaba, imeandikwa, YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI.
20 Basi anwani hiyo waliisoma wengi katika Wayahudi; maana mahali pale aliposulibiwa Yesu palikuwa karibu na mji; nayo iliandikwa kwa Kiebrania, na Kirumi, na Kiyunani”.
Kama tunavyosoma,. Pale juu ya msalaba wa Bwana Yesu, Pilato alingongelea kibao ambacho kilikuwa kinamwelezea kuwa yeye ni nani,.. Sasa maneno hayo YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI kwa Kilatino (au, Kirumi) yanasomeka hivi…”Iesus Nazarenus Rex Iudaeorum.” Na kifupi chake ndio hiyo I.N.R.I…
Sasa madhehebu mengi hususani, Katoliki, Anglikana na Lutheran, wanapenda kutumia Ufipisho huo wa lugha ya kilatino (kirumi), kiyawakilisha yale maneno yaliyoandikwa juu ya msalaba wa Yesu.
Lakini Ukweli ni kwamba juu ya msalaba, hayakuandikwa maneno yale katika ufupisho wowote, bali yaliandikwa vile vile kama yalivyokuwa tena kwa lugha zote tatu, ili kila mtu aliyepita aweze kuyasoma, na ndio maana wale Mafarisayo wakamwambia Pilato. Usiandike, kuwa huyu ni Mfalme wa Wayahudi; bali andika kuwa yeye ndio anajiita, mfalme wa Wayahudi…Unaona ikiashiria kwamba maandishi yale yalikuwa yanasomeka kabisa na sio kwamba yameandikwa kwa kifupisho fulani.
Lakini pamoja na hayo yote, kujua au kutokuja msalaba ulikuwaje, kwamba ulikuwa ni mrefu sana, au ni mfupi sana, au ulikuwa ni wa alama ya kujumlisha, au ni wa nguzo iliyosimama, au kwamba maandishi yake yaliandikwa kwa wino wa bluu au wa njano, Hayo yote hayachangii chochote katika wokovu wetu?? Kwasababu hata katika Neno hilo hilo YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI, ukisoma injili nyingine utaona linasema tu MFALME WA WAYAHUDI(Marko 15:26), na sehemu nyingine linasema HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI(Luka 23:38)..Unaona sasa ukiyatafsiri hayo katika lugha ya kilatino (kirumi) utaona ni tofauti kabisa na hiyo yenye kifupisho cha INRI.
Sasa Hiyo yote ni kutufundisha kuwa tunachopaswa kujua ni kwamba Kristo alisulibiwa juu ya mti, na kwamba kusulibiwa kwake kumeleta ondoleo la dhambi la maisha yetu. Hicho ndicho kiini cha msalaba, na kwamba yoyote amwaminiye Yesu Kristo atapata ondoleo la dhambi zake na ukombozi wa Maisha yake, Hivyo tusiitazame misalaba sana, na kuipa heshima mpaka sasa imeshawafanya wengine wafikie hatua ya kuiabudu na kuisujudia..jambo ambalo ni machukizo makubwa mbele za Mungu.
Ubarikiwe.
Tafadhali share na wengine.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Siku moja Kabla ya kinauma kuokoka nilikuwa katika moja ya makanisa,nikamsikia anaeitwa PROPHET. () akisema nyingi yaani waumini.Bado wachanga,kiroho Ile ukomae unapaswa upate vitabu vitano vilivyoondolewa ktk biblia hapo unaweza hata kuwaita malaika ukaongea nao .akataja moja ya kitabu Hicho ni cha TOBITI.me kweli? NA hivyo vitabu vipo watu wanavyo?
About the author