Israeli ipo bara gani?

Israeli ipo bara gani?

Israeli ipo  Bara la Asia, katika ukanda wa Asia Magharibi (au ukanda wa Mashariki ya kati). tofuati na inavyodhaniwa na baadhi ya watu  kuwa Israeli ipo bara la Ulaya.

Ikumbukwe kuwa Bara la Asia ndio bara lililokubwa kuliko yote duniani, na limegawanyika katika maeneo makuu sita (6),

  1. Asia ya Kaskazini: Nchi ya Siberia
  2. Asia ya Kusini: India, Pakistani, Sri Lanka n.k.
  3. Asia ya Mashariki: Kuna Nchi kama China, Japan, North Korea, Taiwan n.k
  4. Asia ya Magharibi (Mashariki ya kati) : Lebanoni, Jordani, Palestina, Siria, n.k.
  5. Asia ya Kati: Kuna nchi kama, Kazakhastani, Kyrgyzstani, Tajikistani n.k.
  6. Asia ya Kusini mashariki: Vietnam, Thailand, Indonesia n.k.

Kwa maelezo marefu juu ya mataifa hayo unaweza kuyasoma Wikipedia fungua link hii >> https://sw.wikipedia.org/wiki/Asia

Sasa katika  huo ukanda wa Asia Magharibi /Asia ya kati ambao ndio unaundwa na nchi kama Jordan, Siria, Lebanoni, Palestina, Saudi Arabia, Oman, Yemen n.k Ndio huko sasa nchi ya Israeli nayo inapatikana.

Hivyo ni vema pia kujua juu ya historia ya muhimu zaidi ihusulo taifa hili,. Kwani huko ndiko alipotokea mkombozi wa huu ulimwenguni, ajulikanaye kama YESU KRISTO wa Nazareti.  Ambaye kwa kupitia yeye mimi na wewe tumepokea uzima wa milele bure kama tukimwamini.

Hakuna mwadamu aliyewahi kutokea mwenye malengo, na mkamilifu kama Yesu Kristo..Huyu alitumwa na Mungu mwenyewe ili kuja kutuokosa sisi tulio katika shida na vifungo na mateso ya dhambi. 

Na siku akirudi, miguu yake itatua tena kwa mara ya kwanza katika taifa hili hili la Israeli, juu ya milima ujulikanao kama mlima wa mizeituni (Zekaria 14:4), na taifa hili ndilo litakalokuwa makao yake makuu, ambapo atatawala kama BWANA WA MABWANA na MFALME WA WAFALME juu ya dunia nzima katika  Yerusalemu yake mpya atakayoifanya.

Wakati huo dunia haitakuwa kama ilivyo sasa, kwani itakuwa imeshatengenezwa na kurudishwa katika katika hali ambayo haielezeki kwa jinsi ya kibinadamu. Tutatawala Pamoja naye kwa muda wa miaka 1000 ni kisha baada ya hapo tutaingia katika umilele.

Kwa maelezo marefu, fungua vichwa vya masomo mengi hapo chini ufahamu kalenda yote  ya ki-Mungu kwetu sisi wanadamu duniani..

Shalom.

Mada Nyinginezo:

KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIANI?

UTAWALA WA MIAKA 1000.

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

UNYAKUO.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Justine
Justine
1 year ago

Shalom naomba kuuliza naweza kupata vitabu

ZAKALIA
ZAKALIA
2 years ago

Amina ubarikiwe kwa masomo mazuri