Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze Biblia, ambapo leo tutajifunza kwa ufupi juu ya upeo wa kimbinguni.
Mungu alipomuumba mwanadamu, alimwumba na vitu vitatu NAFSI, MWILI na ROHO…kwasababu Mungu naye ndio yupo hivyo hivyo, anayo nafsi, mwili na Roho, maana alituumba kwa mfano wake…Nafsi yake ndio yeye mwenyewe, roho yake ndio Roho Mtakatifu, na mwili wake ndio ule Uliokuwepo Pale Kalvari, ukafufuka na kupaa mbinguni…Kwahiyo uhai uliokuwa ndani ya Mwili unaoitwa Yesu ndio Mungu mwenyewe(nafsi yake) ukisoma Wabrania 1:3 utaliona hilo…Na Roho iliyokuwepo ndani ya ule mwili wa Yesu ndiye Roho Mtakatifu mwenyewe. Hilo linatuthibitishia kuwa Mungu ni mmoja, na nafsi yake ni moja na Roho yake ni moja, na mwili wake ni mmoja.
1 Timotheo 3:16 “Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu”.
Huyo ni Bwana Yesu anazungumziwa hapo, Mungu katika mwili, aliyehubiriwa katika mataifa na akapaa juu mbinguni…kwasababu hakuna mwingine aliyepaa Mbinguni mpaka kwenye kiti cha enzi zaidi yake yeye..
Yohana 3:13 “Wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu”.
Utauliza mbona Biblia inasema Nabii Eliya na Henoko walipaa na kuchukuliwa mbinguni…Ndugu Nabii Eliya hakupelekwa mbinguni Bwana alipo sasa, bali alipelekwa mahali panapoitwa Peponi (paradiso), ndio maana sehemu nyingine biblia inasema Henoko alihamishwa, sio alipaa (Waebrania 11:5)….wakati mwingine biblia inapataja paradiso kama mbinguni, kwasababu ya uzuri uliopo huko…Lakini hao watu hawakupelekwa mbinguni Bwana aliko sasa, kule hakuna mwanadamu ambaye ameshafika, ni makao mapya yanaandaliwa kule kwa watu wote waliookolewa kufika siku moja kwa pamoja…hakuna mwanadamu aliyetutangulia kufika kule…Ni Bwana Yesu tu! Peke yake ndio yupo kule akituandalia makao na malaika watakatifu..Sasa kama Eliya kashafika huko kutakuwaje tena… “sehemu ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia”? unaona?.
Utauliza tena, na hao wanaoona maono wakipelekwa mbinguni, ina maana maono yao ni batili?..Wengi wao wanaosema wamepelekwa mbinguni kiuhalisia hawajapelekwa mbinguni kwasababu huko hakuna mtu ambaye ameshafika…wanachokiona ni Maono ya mbinguni…Bwana anawaonyesha maono ya jinsi mbinguni kunavyofanana fanana, lakini sio kwamba wamefika,..Sasa Bwana anaweza kuwapa maono ambayo wakati mwingine ni dhahiri kabisa mtu anaweza akahisi yupo mahali pengine katika mwili kabisa…lakini yakawa ni maono tu sio sehemu halisi…
Hata katika namna za kawaida mtu anaweza kuota ndoto ambayo ni kama dhahiri kabisa, katika ndoto akahisi kabisa vile vitu kama vile haoti, akasikia harufu, akachoka, akahisi baridi ndani ya ndoto, akahisi jua linampiga, akahisi njaa, wakati mwingine akahisi mpaka maumivu katika ndoto, Lakini si kweli kwamba huyo mtu saa hiyo yupo katika huo ulimwengu…Hizo zinaitwa njozi. Na ndivyo Bwana anavyozungumza na watu, anaweza kuwapa watu wake maono kama vile wapo Mbinguni kabisa, wakaona pengine barabara za dhahabu, au almasi, wakaona bustani nzuri, wakaona Malaika watakatifu, wakaona uzuri usioelezeka wa huko, hisia ambazo wanaweza wakadhani ni kweli wamefika kule..Hapana kule hawajafika isipokuwa wamepewa tu maono ya kule.
Lengo la Bwana kuwaonyesha vile ni kutaka kuwaonjesha watu wake uzuri watakaokwenda kukutana nao kule, na wawafikishie wengine ujumbe. Na Bwana anaweza kumpa mtu yeyote maono hayo. Sasa ukikosa maarifa ya kuyaelewa haya, unaweza ukajipiga kifua mbele na kufikiri kwamba umeshawahi kufika mbinguni kabla ya wengine…Mambo yaliyopo kule wala hatuwezi kuyafikiria wala kuyastahimili katika hii miili yetu na akili zetu, mpaka tubadilishwe ndipo tutakapoweza kuyaelezea.
Na maono haya Bwana anayowapa watu, yanatofautiana mwingine ataonyeshwa hivi mwingine vile…mwingine kwenye maono hayo ataonyeshwa barabara za dhahabu, mwingine almasi, mwingine marumaru, mwingine ataonyeshwa makasri, mwingine mahekalu, mwingine ataonyeshwa tunu za kipekee, mwingine ataonyweshwa malaika wamevaa kanzu nyeupe wameshikilia upanga, mwingine ataonyeshwa wamevaa nyeupe zenye mshipi wa dhahabu na wameshikilia matarumbeta, mwingine ataonyeshwa wamevaa blue n.k Nk kwa jinsi Bwana atakavyopenda kumwonesha mtu. Ndio maana utaona kila mmoja anakuja na ushuhuda wake tofauti na mwingine wa mambo aliyoyaona…
Sasa kama wangekuwa wamepelekwa mahali halisi, wasingekuja kila mmoja na ushuhuda wake? Unaona? Wote wangekuja na ushuhuda unaofanana…Lakini kwasababu ni maono, maono hayawezi kufanana…ndio maana utaona Hata kwenye Biblia Yohana wa Patmo alipewa maono yenye maudhui sawa na yale ya Nabii Danieli lakini yalikuwa hayafanani…utaona Danieli anaonyeshwa wanyama wanne wanatoka baharini, mmoja alikuwa mfano wa simba, mwingine chui, mwingine Dubu na mwingine kiumbe kisichojulikana (Danieli 7:3-7)…Lakini Yohana anaonyeshwa mnyama mmoja akitoka baharini aliye mfano wa chui, miguu yake kama ya dubu na kinywa kama kinywa cha simba..(Ufunuo 13:2). Sasa alichoonyeshwa Yohana wa Patmo na Danieli ni kitu kimoja isipokuwa katika maono tofauti..ndio maana utaona kuna utofauti kidogo huyu kaonyeshwa wanyama wanne, lakini huyu kaonyeshwa mnyama mmoja mwenye maumbile ya wanyama wote wanne.
Utaona tena jambo hilo katika Kitabu cha Ezekieli, yeye alionyeshwa makerubi wana nyuso nne kila upande, uso wa mwanadamu, tai, Ndama, pamoja na simba, yaani kerubi mmoja ana nyuso nne..kwenye maono ndivyo alivyoonyeshwa..
Ezekieli 1: 5 “Kukatokea katikati yake mfano wa viumbe hai vinne. Kuonekana kwao kulikuwa hivi; walikuwa na sura ya mwanadamu. 6 Na kila mmoja alikuwa na nyuso nne, na kila mmoja alikuwa na mabawa manne. 7 Na miguu yao ilikuwa miguu iliyonyoka; na nyayo za miguu yao zilikuwa kama nyayo za miguu ya ndama; zikimetameta kama rangi ya shaba iliyosuguliwa sana. 8 Nao walikuwa na mikono ya mwanadamu chini ya mabawa yao, pande zote nne; na wote wanne walikuwa na nyuso zao na mabawa yao hivi; 9 mabawa yao yaliungana, hili na hili; nao hawakugeuka walipokwenda, walikwenda kila mmoja kuelekea mbele. 10 Kwa habari za mfano wa nyuso zao; walikuwa na uso wa mwanadamu; na hao wanne walikuwa na uso wa simba upande wa kuume; na hao wanne walikuwa na uso wa ng’ombe upande wa kushoto; na hao wanne walikuwa na uso wa tai pia”.
Ezekieli 1: 5 “Kukatokea katikati yake mfano wa viumbe hai vinne. Kuonekana kwao kulikuwa hivi; walikuwa na sura ya mwanadamu.
6 Na kila mmoja alikuwa na nyuso nne, na kila mmoja alikuwa na mabawa manne.
7 Na miguu yao ilikuwa miguu iliyonyoka; na nyayo za miguu yao zilikuwa kama nyayo za miguu ya ndama; zikimetameta kama rangi ya shaba iliyosuguliwa sana.
8 Nao walikuwa na mikono ya mwanadamu chini ya mabawa yao, pande zote nne; na wote wanne walikuwa na nyuso zao na mabawa yao hivi;
9 mabawa yao yaliungana, hili na hili; nao hawakugeuka walipokwenda, walikwenda kila mmoja kuelekea mbele.
10 Kwa habari za mfano wa nyuso zao; walikuwa na uso wa mwanadamu; na hao wanne walikuwa na uso wa simba upande wa kuume; na hao wanne walikuwa na uso wa ng’ombe upande wa kushoto; na hao wanne walikuwa na uso wa tai pia”.
Lakini Yohana wa Patmo yeye alionyeshwa Kila Kerubi na uso mmoja, yupo aliyekuwa na uso wa Tai, mwingine Uso wa Ndama, mwingine wa Mwanadamu na mwingine wa Simba, lakini hakuoneshwa kuwa kerubi mmoja ana nyuso nne kama alivyooneshwa Nabii Ezekieli.
Ufunuo 4: 6 “Na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri; na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma. 7 Na huyo mwenye uhai wa kwanza alikuwa mfano wa simba; na mwenye uhai wa pili alikuwa mfano wa ndama; na mwenye uhai wa tatu alikuwa na uso kama uso wa mwanadamu; na mwenye uhai wa nne alikuwa mfano wa tai arukaye. 8 Na hawa wenye uhai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita; na pande zote na ndani wamejaa macho, wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja”.
Ufunuo 4: 6 “Na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri; na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma.
7 Na huyo mwenye uhai wa kwanza alikuwa mfano wa simba; na mwenye uhai wa pili alikuwa mfano wa ndama; na mwenye uhai wa tatu alikuwa na uso kama uso wa mwanadamu; na mwenye uhai wa nne alikuwa mfano wa tai arukaye.
8 Na hawa wenye uhai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita; na pande zote na ndani wamejaa macho, wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja”.
Kwahiyo Mbinguni hakuna aliyefika sasa, ni sehemu mpya Bwana anayowaandalia watu wake, na watakaofika ni wale tu waliooshwa dhambi zao kwa damu yake, yaani wale waliomwamini yeye na kutubu na kubatizwa, na kuishi maisha ya utakatifu (Waebr 12:14)..Wapendwa wetu waliokufa katika Kristo sasa wapo mahali pa mangojeo panapoitwa Paradiso au peponi (Ni mahali wamehifadhiwa pa raha sana, lakini ni pa muda tu, wakingoja siku ile ifike)..Na sisi tutakapokufa kabla ile siku haijafika tutakwenda kuungana nao kule, ni sehemu nzuri sana, wote tutakuwa tunaingoja ile siku kwa pamoja.
Biblia inasema siku ile itakapofika wafu wote (yaani wale waliokufa katika haki, waliohifadhiwa paradiso sehemu ya raha na mangojeo)..watafufuka (yaani watarudi katika miili hii ya asili kwanza)..na watakatifu walio hai watawaona na kuungana nao, na kwa pamoja kufumba na kufumbua tutabadilishwa miili yetu na kuvaa ya miili ya utukufu..itakayoweza kustahimili hayo mambo mazuri na mapya tutakayokwenda kuyakuta huko juu…Na ghafla tutavutwa juu mbali sana na hii ardhi (Itakuwa ni shangwe kubwa sana siku hiyo) tutaiingia mbingu ya mbingu….(na mambo tutakayoyakuta huko hakuna awezaye kuyasimulia kwasababu hakuna mtu alishawahi kufika huko kabla)…Lakini kwa walio nje ya Kristo itakuwa ni kilio na kusaga meno na maombolezo makubwa…
Siku ya mwisho yaja! Maran atha maana yake “BWANA WETU ANAKUJA” Na watakatifu waliopo paradiso wanaitamani hiyo siku ifike haraka…siku ya kufutwa machozi yao, na taabu zao na kuingizwa katika umilele.
Ufunuo 22: 20 “Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; naja upesi. Amina; na uje, Bwana Yesu”.
Mpe Kristo maisha yako leo, ili uwe na uhakika wa kuwepo miongoni mwa watakaokwenda kuyaona mambo mazuri Bwana aliyowaandalia watu wake..
Bwana akubariki sana.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
TOFAUTI KATI YA NDOTO NA MAONO NI IPI?
BASI MUNGU AKAMUADHIMISHA SANA..
UNYAKUO NI NINI?
SIKU YA BWANA NI NINI?
NINI HUDUMA YA MALAIKA WATAKATIFU SASA?
Rudi Nyumbani
Home
Print this post
Karibu tujifunze Neno la Mungu, Biblia takatifu..Kama tunavyojua vitabu hivi vya biblia pamoja na kwamba vimeandikwa wakati mwingine kwa mfumo wa Hadithi, lakini vimebeba ufunuo mkubwa sana ndani yake. Ndio maana tunapaswa tujifunze Biblia na sio tuisome tu!…kwasababu kuna tofauti kubwa kati ya kujifunza na kusoma.
Tumekwisha kuvipitia kwa ufupi vitabu 8 vya kwanza, ambapo cha Mwisho kilikuwa ni kitabu cha RUTHU ambacho kilikuwa kinaelezea chimbuko la Mfalme Daudi lilipotokea, tulimwona mwanamke huyu Ruthu, ambaye hakuwa hata myahudi (alikuwa mtu wa mataifa) kwa Imani aliweza kubeba uzao wa Kifalme ndani yake, kama vile Rahabu kwa imani alivyohesabiwa miongoni mwa wayahudi japo hakuwa myahudi ..na tuliona pia kitabu hiki kiliandikwa na Nabii Samweli ambaye ndiye aliyekuwa mwamuzi wa mwisho kabisa wa Taifa la Israeli.
Na sasa kitabu kinachofuata ni kitabu cha SAMWELI wa Kwanza..Kitabu hichi kiliandikwa na Nabii Samweli mwenyewe kama jina la kitabu lilivyo, sehemu za mwisho wa kitabu baada ya Samweli kufa ziliandikwa na Nabii Gadi na Nabii Nathani ambao tutakuja kuona habari zao huko mbeleni.
Kitabu hichi cha SAMWELI WA KWANZA (au 1 Samweli). Ni kitabu kinachoelezea mabadiliko makubwa ya Taifa la Israeli. Ni kitabu kinachoelezea mabadiliko ya nyakati. Kumbuka wakati wana wa Israeli wanatoka Misri hawakuwa na Mfalme na haukuwa mpango wa Mungu mtu fulani mmoja atawale juu ya wengine…
wangekuwepo viongozi lakini sio Mfalme, kuwepo kwa mfalme ndani ya Taifa la Israeli haukuwa mpango kabisa wa Mungu…kwani kwa kupitia mfumo wa kifalme ndio uliowatesa wao wakiwa Misri, walitumikishwa vikali kwa amri ya Mfalme wa Misri, kwahiyo Bwana alipowaweka Huru mbali na hiyo kamba hakutaka tena watoto wake wafungwe au wajifunge katika mfumo huo kwasababu alijua madhara yake…Na sio tu kuwa na mfalme bali hata hakutaka watwae watumwa miongoni mwa ndugu zao na kuwatumikisha kama walivyotumikishwa walipokuwa Misri.
Walawi 25: 38 “Mimi ndimi Bwana, Mungu wako, niliyewatoa katika nchi ya Misri ili niwape nchi ya Kanaani, nipate kuwa Mungu wenu. 39 Tena kwamba nduguyo amekuwa maskini pamoja nawe, akajiuza kwako; usimtumikishe mfano wa mtumwa; 40 kwako wewe atakuwa mfano wa mtumishi aliyeajiriwa, au mfano wa msafiri; naye atatumika kwako hata mwaka wa yubile; 41 ndipo atakapotoka kwako aende zake, yeye na wanawe pamoja naye, naye atairejea jamaa yake mwenyewe, tena atairejea milki ya baba zake. 42 KWA KUWA HAO NI WATUMISHI WANGU, NILIOWALETA WATOKE NCHI YA MISRI; WASIUZWE MFANO WA WATUMWA. 43 Usitawale juu yake kwa nguvu; ila umche Mungu wako. 44 Tena katika habari za watumwa wako na wajakazi wako, utakaokuwa nao; mataifa walio kando-kando yenu, katika hao mtanunua watumwa na wajakazi. 45 Tena katika wana wa wageni wakaao kati yenu mtajinunulia, na katika jamaa zao walio pamoja nanyi, waliowazaa katika nchi yenu; wao watakuwa milki yenu. 46 Nanyi mtawafanya kuwa urithi kwa watoto wenu baada yenu, wawe milki yao; siku zote mtatwaa watumwa wenu katika hao; LAKINI MSITAWALE KWA NGUVU JUU YA NDUGU ZENU, HAO WANA WA ISRAELI, WENYEWE KWA WENYEWE”.
Walawi 25: 38 “Mimi ndimi Bwana, Mungu wako, niliyewatoa katika nchi ya Misri ili niwape nchi ya Kanaani, nipate kuwa Mungu wenu.
39 Tena kwamba nduguyo amekuwa maskini pamoja nawe, akajiuza kwako; usimtumikishe mfano wa mtumwa;
40 kwako wewe atakuwa mfano wa mtumishi aliyeajiriwa, au mfano wa msafiri; naye atatumika kwako hata mwaka wa yubile;
41 ndipo atakapotoka kwako aende zake, yeye na wanawe pamoja naye, naye atairejea jamaa yake mwenyewe, tena atairejea milki ya baba zake.
42 KWA KUWA HAO NI WATUMISHI WANGU, NILIOWALETA WATOKE NCHI YA MISRI; WASIUZWE MFANO WA WATUMWA.
43 Usitawale juu yake kwa nguvu; ila umche Mungu wako.
44 Tena katika habari za watumwa wako na wajakazi wako, utakaokuwa nao; mataifa walio kando-kando yenu, katika hao mtanunua watumwa na wajakazi.
45 Tena katika wana wa wageni wakaao kati yenu mtajinunulia, na katika jamaa zao walio pamoja nanyi, waliowazaa katika nchi yenu; wao watakuwa milki yenu.
46 Nanyi mtawafanya kuwa urithi kwa watoto wenu baada yenu, wawe milki yao; siku zote mtatwaa watumwa wenu katika hao; LAKINI MSITAWALE KWA NGUVU JUU YA NDUGU ZENU, HAO WANA WA ISRAELI, WENYEWE KWA WENYEWE”.
Umeona! Kwahiyo Mungu, alikataza watoto wake wasiwe watumwa katika hiyo nchi waliyoahidiwa…Na zaidi ya yote ukiendelea kusoma utaona Bwana hakuwaruhusu hata pia kutozana RIBA wao kwa wao.
Lakini tunaona wana wa Israeli baada ya miaka mingi kupita walisahau hilo agizo..wakatamani utawala wa kishupavu kama wa Mataifa yaliyowazunguka..Ndipo ukafika wakati waisraeli wote wakakusanyana wakamwendea Nabii Samweli ambaye ndiye alikuwa mwamuzi wa kipindi hicho wakamwambia wanataka mfalme juu yao ili wafanane na mataifa mengine ya Duniani.
Jambo lile likamchukiza sana Samweli na Mungu, na Mungu akawapa mfalme kama walivyotaka, na Bwana akamwongoza Nabii Samweli aandike kitabu cha mambo hayo ili iwe kumbukumbu kwa vizazi vinavyokuja mbele yao na iwe fundisho kwetu sisi watu wa zamani hizi…Kwahiyo sehemu ya Mwanzo wa kitabu hichi inaelezea historia ya Samweli, kuzaliwa kwake na ukuhani katika hema ya Mungu, pamoja na Eli kuhani..Na kuanzia sura ya 8 na kuendelea ndipo tunaona wana wa Israeli wakitaka mabadiliko. Na sehemu iliyobakia inaelezea maisha na matendo ya Mfalme wa Kwanza wa Israeli (Sauli) mwanzo wake na mwisho wake.
1 Samweli 8:4 “Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama; 5 wakamwambia, Angalia, wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; basi, tufanyie mfalme atuamue, mfano wa mataifa yote. 6 Lakini neno hilo likawa baya machoni pa Samweli, waliposema, Tupe mfalme atuamue. Naye Samweli akamwomba Bwana. 7 Bwana akamwambia Samweli, Isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokuambia; kwa maana hawakukukataa wewe, bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao. 8 Kwa kadiri ya matendo yote waliyonitenda tokea siku ile nilipowatoa katika Misri hata leo, kwa kuniacha mimi, na kwa kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokutenda wewe. 9 Basi sasa, isikilize sauti yao; walakini, uwaonye sana, na kuwaonyesha desturi ya mfalme atakayewamiliki. 10 Naye Samweli akawaambia wale watu waliotaka mfalme maneno yote ya Bwana. 11 Akasema, Mfalme atakayewamiliki ninyi atakuwa na desturi hii; atatwaa wana wenu na kuwaweka kwake, kwa magari yake, na kuwa wapanda farasi wake; nao watapiga mbio mbele ya magari yake. 12 Naye atawaweka kwake kuwa maakida juu ya elfu, na maakida juu ya hamsini; na wengine atawaweka walime shamba lake, na kuvuna mavuno yake, na kufanyiza zana zake za vita, na vyombo vya magari yake. 13 Na binti zenu atawatwaa kuwa wafanyaji wa marhamu, na wapishi, na waokaji. 14 Atatwaa makonde yenu, na mashamba yenu ya mizabibu, na ya mizeituni, yale yaliyo mazuri sana, ili awape watumishi wake. 15 Naye atawatoza ushuru wa mbegu zenu na wa mizabibu yenu, awape maakida wake, na watumishi Wake. 16 Atawatwaa watumishi wenu na wajakazi wenu, na ng’ombe zenu walio wazuri sana, na punda zenu, naye atawatia katika kazi zake mwenyewe”. 17 Atawatoza fungu la kumi la makundi yenu; nanyi mtakuwa watumwa wake. 18 NANYI MTALIA SIKU ILE KWA SABABU YA MFALME WENU MLIYEJICHAGULIA; BWANA ASIWAJIBU SIKU ILE. 19 Walakini hao watu wakakataa kuisikiliza sauti ya Samweli; wakasema, Sivyo hivyo; lakini tunataka kuwa na mfalme juu yetu;”
1 Samweli 8:4 “Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama;
5 wakamwambia, Angalia, wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; basi, tufanyie mfalme atuamue, mfano wa mataifa yote.
6 Lakini neno hilo likawa baya machoni pa Samweli, waliposema, Tupe mfalme atuamue. Naye Samweli akamwomba Bwana.
7 Bwana akamwambia Samweli, Isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokuambia; kwa maana hawakukukataa wewe, bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao.
8 Kwa kadiri ya matendo yote waliyonitenda tokea siku ile nilipowatoa katika Misri hata leo, kwa kuniacha mimi, na kwa kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokutenda wewe.
9 Basi sasa, isikilize sauti yao; walakini, uwaonye sana, na kuwaonyesha desturi ya mfalme atakayewamiliki.
10 Naye Samweli akawaambia wale watu waliotaka mfalme maneno yote ya Bwana.
11 Akasema, Mfalme atakayewamiliki ninyi atakuwa na desturi hii; atatwaa wana wenu na kuwaweka kwake, kwa magari yake, na kuwa wapanda farasi wake; nao watapiga mbio mbele ya magari yake.
12 Naye atawaweka kwake kuwa maakida juu ya elfu, na maakida juu ya hamsini; na wengine atawaweka walime shamba lake, na kuvuna mavuno yake, na kufanyiza zana zake za vita, na vyombo vya magari yake.
13 Na binti zenu atawatwaa kuwa wafanyaji wa marhamu, na wapishi, na waokaji.
14 Atatwaa makonde yenu, na mashamba yenu ya mizabibu, na ya mizeituni, yale yaliyo mazuri sana, ili awape watumishi wake.
15 Naye atawatoza ushuru wa mbegu zenu na wa mizabibu yenu, awape maakida wake, na watumishi Wake.
16 Atawatwaa watumishi wenu na wajakazi wenu, na ng’ombe zenu walio wazuri sana, na punda zenu, naye atawatia katika kazi zake mwenyewe”.
17 Atawatoza fungu la kumi la makundi yenu; nanyi mtakuwa watumwa wake.
18 NANYI MTALIA SIKU ILE KWA SABABU YA MFALME WENU MLIYEJICHAGULIA; BWANA ASIWAJIBU SIKU ILE.
19 Walakini hao watu wakakataa kuisikiliza sauti ya Samweli; wakasema, Sivyo hivyo; lakini tunataka kuwa na mfalme juu yetu;”
Kwa ufupi mwanzo wa matatizo makubwa yaliyowakumba wana wa Israeli yalianzia wakati huu walipojitakia mfalme….huko mbeleni utakuja kuona Wafalme ndio waliowakosesha sana wana wa Israeli na kuwasababisha waingie utumwani na kutapanywa katika mataifa yote duniani.
Na zaidi ya yote utaona Bwana aliwaonya hapo juu, kuwa Mfalme wanayemtaka atawafanya wana wao na binti zao kuwa watumwa, watatumikishwa kwa utumishi mkali..Na watalipishwa ushuru kwa kila kitu, desturi ambayo hapo mwanzo hawakuwa nayo, na wataiona hiyo nchi ya Kaanani Bwana aliyowapa ni chungu! Wataona hakuna tofauti na kule Misri walipotoka..Na Bwana akawaambia siku hiyo baada ya mateso hayo wataomba msaada kwa Bwana lakini Bwana hatawasikia……. Lakini hawakuelewa kama biblia inavyosema! Wakapewa mfalme kama walivyotaka…Na Neno la Bwana likaja kutimia juu yao kama lilivyo miaka kadhaa mbeleni: walitumikishwa kwa utumishi mkali mpaka siku moja wakakusanyika kuomba wapunguziwe makali ya utumishi baada ya Mfalme Sulemani kufa…Tunayasoma hayo katika..
2 Nyakati 10:2 “Ikawa Yeroboamu mwana wa Nebati aliposikia, (maana alikuwako Misri, ambako amekimbilia mbele ya mfalme Sulemani), Yeroboamu akarudi kutoka Misri. 3 Wakapeleka ujumbe, wakamwita, Yeroboamu akaja na Israeli wote, wakamwambia Rehoboamu, wakasema, 4 Baba yako alilifanya zito kongwa letu; basi sasa upunguze utumwa mgumu wa baba yako, na kongwa lake zito alilotutwika, nasi tutakutumikia. 5 Akawaambia, Mnirudie baada ya siku tatu. Watu wakaenda zao………………….. 9 Akawaambia, Je! Mwanipa shauri gani la kuwajibu watu hawa, waliosema nami, wakisema, Utufanyie jepesi kongwa alilotutwika baba yako. 10 Na wale vijana waliokua pamoja naye wakamwambia, wakasema, Uwaambie hivi watu wale waliosema nawe, wakinena, Baba yako alilifanya zito kongwa letu, lakini wewe tufanyie jepesi; uwaambie hivi, KIDOLE CHANGU CHA MWISHO NI KINENE KULIKO KIUNO CHA BABA YANGU. 11 Basi kama baba yangu aliwatwika kongwa zito, mimi nitaongeza kongwa lenu; baba yangu AKIWAPIGA KWA MIJELEDI, LAKINI MIMI NITAWAPIGA KWA NGE. 12 Basi Yeroboamu na watu wote wakamjia Rehoboamu siku ya tatu, kama mfalme alivyoamuru, akisema, Mnirudie siku ya tatu. 13 Mfalme akawajibu kwa ukali; mfalme Rehoboamu akaliacha shauri la wazee, akasema nao kwa shauri la vijana, 14 akinena, Baba yangu aliwafanyia kongwa zito, NAMI NITAWAONGEZEA; BABA YANGU ALIWAPIGA KWA MIJELEDI, LAKINI MIMI NITAWAPIGA KWA NGE. 15 Basi mfalme hakuwasikia wale watu; MAANA JAMBO HILI LILITOKA KWA MUNGU, ili alithibitishe neno lake alilomwambia Yeroboamu mwana wa Nebati kwa mkono wa Ahiya Mshiloni.”
2 Nyakati 10:2 “Ikawa Yeroboamu mwana wa Nebati aliposikia, (maana alikuwako Misri, ambako amekimbilia mbele ya mfalme Sulemani), Yeroboamu akarudi kutoka Misri.
3 Wakapeleka ujumbe, wakamwita, Yeroboamu akaja na Israeli wote, wakamwambia Rehoboamu, wakasema,
4 Baba yako alilifanya zito kongwa letu; basi sasa upunguze utumwa mgumu wa baba yako, na kongwa lake zito alilotutwika, nasi tutakutumikia.
5 Akawaambia, Mnirudie baada ya siku tatu. Watu wakaenda zao…………………..
9 Akawaambia, Je! Mwanipa shauri gani la kuwajibu watu hawa, waliosema nami, wakisema, Utufanyie jepesi kongwa alilotutwika baba yako.
10 Na wale vijana waliokua pamoja naye wakamwambia, wakasema, Uwaambie hivi watu wale waliosema nawe, wakinena, Baba yako alilifanya zito kongwa letu, lakini wewe tufanyie jepesi; uwaambie hivi, KIDOLE CHANGU CHA MWISHO NI KINENE KULIKO KIUNO CHA BABA YANGU.
11 Basi kama baba yangu aliwatwika kongwa zito, mimi nitaongeza kongwa lenu; baba yangu AKIWAPIGA KWA MIJELEDI, LAKINI MIMI NITAWAPIGA KWA NGE.
12 Basi Yeroboamu na watu wote wakamjia Rehoboamu siku ya tatu, kama mfalme alivyoamuru, akisema, Mnirudie siku ya tatu.
13 Mfalme akawajibu kwa ukali; mfalme Rehoboamu akaliacha shauri la wazee, akasema nao kwa shauri la vijana,
14 akinena, Baba yangu aliwafanyia kongwa zito, NAMI NITAWAONGEZEA; BABA YANGU ALIWAPIGA KWA MIJELEDI, LAKINI MIMI NITAWAPIGA KWA NGE.
15 Basi mfalme hakuwasikia wale watu; MAANA JAMBO HILI LILITOKA KWA MUNGU, ili alithibitishe neno lake alilomwambia Yeroboamu mwana wa Nebati kwa mkono wa Ahiya Mshiloni.”
Umeona? Wafalme wote wa Israeli waliwatumikisha wana wa Israeli kama watumwa, hata Mfalme Sulemani naye, aliwatumikisha wana wa Israeli kupita kiasi…jambo ambalo Mungu hakulitaka.
Kwahiyo kitabu hichi kinaelezea mabadiliko ya Utawala wa wana wa Israeli, kutoka kutawaliwa na Mungu mbinguni mpaka kujitakia mfalme wa kidunia awatawale..Hivyo kina mafunuo mengi sana ndani yake na siri nyingi ni vizuri kama hujakisoma ukisome peke yako, Bwana atakufunulia mambo mengi sana yanayohusiana na wakati huu tunaoishi…lakini jambo moja la kipekee ambalo tunaweza kujifunza juu ya kitabu hiki ni juu ya UBAYA WA KUIGA WATU WA ULIMWENGU HUU..Hekima ya Mungu ni kuu kuliko hekima ya ulimwengu huu, wana wa Israeli walitazama kwa nje jinsi utawala wa kifalme unavyopendeza, hawakujua ndani yake jinsi ulivyo mbaya, mpaka walivyoingia…
Na sisi katika safari yetu ya ukristo tunajifunza, Mambo ya ulimwengu huu, ustaarabu wa ulimwengu huu kwa nje yanaweza kuonekana ni mazuri, yanavutia lakini ndani yake yanamadhara makubwa, Mungu anapotuonya tukae mbali na ulimwengu si kwasababu anatuonea wivu, hapana ni kwa faida yetu wenyewe…anajua madhara tutakayoyapata huko mbeleni endapo tukiuiga ulimwengu, endapo tukienenda kama ulimwengu unavyoenenda…Endapo tukianza kutamani na sisi kuvaa vimini na suruali kama watu wa ulimwengu wanavyovaa, kujipamba kama watu wa ulimwengu wanavyojipamba,..Tutaingia kwenye mtego ambao mwisho wa siku tutaomba Mungu atutoe na Mungu hatatusikia siku hiyo, kama alivyowaambia wana wa Israeli kuwa “18 NANYI MTALIA SIKU ILE KWA SABABU YA MFALME WENU MLIYEJICHAGULIA; BWANA ASIWAJIBU SIKU ILE”.
Tunapoonywa sasa ni wakati wa kusikia, utakapozama kwenye uchawi utafika wakati utalia na Bwana asikujibu!..utakapozama kwenye anasa kupindukia na hali sasa unasikia maonyo hutaki kugeuka itafika wakati utalia na Bwana asikujibu…utakapozama kwenye uasherati na kila siku Bwana anakuonya kwa maonyo haya hutaki kusikia…utafika wakati utalia na Bwana asikujibu!…Unapozama kwenye kuacha uongozi wa Mungu na kufuata uongozi wa mwanadamu, Bwana anakwambia hivi, wewe unasema vile, Bwana anakwambia geuka huku hii ndio njia, lakini wewe unasema dini yangu haisemi hivyo wala watu wote hawasemi hivyo…ndugu yangu utafika wakati utalia na kuomboleza na Bwana hatakusikia!…Unyakuo utakapopita na utakapoachwa utalia na Bwana asikusikie…
Unajua ni kwanini watu wengi wenye magonjwa ya kutisha(japo si wote), Hawaponi? Watu wanaoingia kwenye mitego ya Ibilisi hawanasuki?…Ni kwasababu ya kushupaza shingo wakati wanaonywa..
Mithali 1:29 “Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, Atavunjika ghafula, wala hapati dawa.”
Na imefika wakati wameshazama kwenye matatizo ndipo wanamlilia Mungu,..wengi wanasamehewa makosa yao lakini mauti inakuwa ipo pale pale…sasa hasara zote hizo za nini? Kwanini leo usifanye uteule wako na wito wako imara kama biblia inavyosema katika
2 Petro 1: 10 “Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe. 11 Maana hivi mtaruzukiwa kwa ukarimu kuingia katika ufalme wa milele wa Bwana wetu, Mwokozi wetu Yesu Kristo”.
2 Petro 1: 10 “Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.
11 Maana hivi mtaruzukiwa kwa ukarimu kuingia katika ufalme wa milele wa Bwana wetu, Mwokozi wetu Yesu Kristo”.
Kama hujampa Bwana maisha yako, saa ya wokovu ni sasa, unachotakiwa kufanya sasahivi na hapo ulipo kutubu dhambi zako zote ulizozifanya hapo kabla, na unazozifanya sasahivi…unamwambia Bwana hutaki kuzifanya tena, na wewe mwenyewe ukidhamiria kweli kweli kutokuzifanya tena, kama ulikuwa unakula rushwa unaacha, kama ulikuwa unafanya uasherati unaacha, kama ulikuwa mshirikina unaacha unakwenda kuchoma vifaa vyote vya kishirikina, kama ulikuwa ni mtukanaji, msagaji, mlawiti, shoga, mtoaji mimba, mfanyaji masturbation, mtazamaji pornography, mvaaji vibaya nk. Vyote unaviacha unaanza maisha mapya ndani ya Kristo na Bwana mwenyewe atakusamehe na kukupa maisha mapya ndani yake…Na kama madhara yalikuwa makubwa na ulikuwa hujui kwa mapana madhara yake pia atakuponya ugonjwa wako, atakurejeshea uzima, ila jambo la kwanza ni kutubu kwa kumaanisha kutokufanya tena.
Bwana akuabariki.
Kwa maombezi/ Ushauri/ Ratiba za Ibada/Maswali/ Whatsapp/ Piga namba hizi: +255693036618/ +255789001312
AMEN.
Mada Nyinginezo:
KWANINI SAMWELI ALIRUHUSUIWA KUHUDUMU HEKALUNI KAMA VILE WALAWI WAKATI YEYE NI MU-EFRAIMU?
JE! MUNGU ANAWEZA KULETA MAJIBU KUPITIA NGUVU ZA GIZA KAMA ALIVYOFANYA KWA MFALME SAULI?
USIONDOE ALAMA YA MPAKA ILIYOWEKWA NA MABABA.
CHAGUA NI JIWE LIPI LITAKALO KUFAA KWA UJENZI.
‘’MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI’’..NA NDIVYO ILIVYO KWA UASHERATI
UKOMA NA UJANE ULIO NDANI YAKO, UMEUPATIA TIBA?
Rudi Nyumbani:
Melkizedeki ni nani?
Neno la Mungu linatuambia katika 1Timotheo 3:16 kuwa “bila shaka siri ya utauwa ni kuu.” Au kwa lugha rahisi Neno hili tunaweza kusema “bila shaka siri ya Uungu ni kuu; Hii ikiwa na maana kuwa kuufahamu uungu wa Mungu, si kitu chepesi tu cha kufikirika kibinadamu, bali kipo katika Siri na Siri hiyo ni kubwa sana..Hivyo hiyo inatuhimiza sisi tumwombe Mungu atufunulie ili tuzidi kumjua yeye siku baada ya siku.
Kumbuka Hapa katika hii siri ndipo palipoleta mgawanyiko na mkanganyiko mkubwa kati ya Ukristo na Imani nyingine kama vile uislamu, Na hapa hapa ndipo palipoleta migawanyiko mingine mikubwa katikati ya wakristo wenyewe.
Lakini sisi hatutaingia huko leo, bali kwa ufupi tutamtazama huyu Melkizedeki ni nani, kwa kurejea baadhi ya vifungu vya maandiko. Sasa kumbuka biblia inaweka wazi kabisa, kwamba Kristo alikuwepo kabla hata kabla ya kitu chochote kuwepo duniani.
Yohana 8:57 “Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu? 58 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko”.
Yohana 8:57 “Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu?
58 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko”.
Unaona Lakini swali tunajiuliza alikuwepoje? Hili ni swali ambalo hata wakristo wengi leo hii tunashindwa kulijibu ipasavyo. Tutasema Yohana 1:1 Inathibitisha hilo kuwa hapo mwanzo kulikuwepo na Neno naye Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa, ambaye ndio YESU. Hivyo Yesu alikuwepo tangu mwanzo mbinguni na baba yake mpaka ilipofika wakati wa yeye akashuka duniani kuja kutuokoa.
Lakini hatujui kuwa huyu YESU ambaye anaonekana kwa maumbile yale, hakuwepo tangu mwanzo. Safari yake ilianzia AD 1, tutaliona hilo tunavyozidi kusonga mbele.
Kama biblia inavyosema hapo mwanzo kulikuwako “Neno”, Hivyo kwa asili yake NENO sio mtu, Hili ni Neno la kigiriki Logos, likiwa na maana ya WAZO LA MUNGU, /KANUNI au NIA ya Mungu.
Sasa hili Neno kazi yake kubwa ilikuwa ni nini?
Tukisoma:
1Yohana 1:1 “Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya NENO LA UZIMA; 2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu); 3 hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo”.
1Yohana 1:1 “Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya NENO LA UZIMA;
2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);
3 hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo”.
Unaona hapo Hili Neno kumbe limebeba UZIMA ndani yake (Yohana 1:4), ambao uzima huo Mungu alitaka kuudhihirisha kwetu tangu zamani. Hapa mitume wanasema walikuwa wanalisikia tangu zamani, hivyo halikuwa jambo jipya katika masikio yao lakini baadaye sasa wakati ulipofika wakaja kupata neema ya kuliona kwa macho yao wenyewe na kulipapasa siku lilipokuja kufanyika mwili ndani ya YESU KRISTO.
Sasa tumeshaona uzima wowote ni Neno la Mungu (Wazo la Mungu) kwa mwanadamu, Kazi yake kubwa ni kurejesha kilichopotea na kukikomboa. Hivyo katika maandiko Neno hili la uzima halikuanzia kwenye Ule mwili wa YESU KRISTO pekee, hapana bali lilianzia tangu mbali sana, isipokuwa lilifichwa tu machoni pa watu wasilitambue kwasababu SIRI ya utauwa ilikuwa bado haijafichuliwa. Hivyo hili NENO Lilichukua maumbile mengi mengi tofauti kwa lengo tu la kutimiza kusudi lile lile kuleta uzima ndani ya watu.
➔Tunaona lilikuwepo kuanzia Edeni, mwanzoni kabisa mwa safari ya mwanadamu kama Ule mti wa Uzima katika bustani, Lile lilikuwa ni NENO LA MUNGU..lilikuwepo pale kuwapa uzima Adamu na hawa, kuwazuia na mauti, lakini walipoasi wakafukuzwa mbali nalo.
➜Baadaye likaja likachukua umbile lingine tena la MERIKEBU(SAFINA), Lilisimama pale ili kuwakomboa wanadamu na uzao wao usipotee kabisa katika uso wa dunia, akaokoka Nuhu na watu wengine 7.
➜Baadaye likaja kuchukua umbo la mnyama MWANAKONDOO, siku ile Ibrahimu alipokwenda kumtoa mwanawe wa pekee kuwa sadaka ya kuteketezwa likasimama kama dhabihu badala ya Isaka kama Yule kondoo aliyekuwa mlimani kichakani, vyote hivyo vilifanyika kwa mafumbo makubwa sana, kufunua UZIMA hasa udumuo utakaokuja huko mbeleni..
➜Ndio baadaye tunakuja kuona linachukua tena maumbile ya wanadamu likaonekana duniani kwa wakati mchache kutimiza kusudi Fulani ndio sasa hapo tunamwona mtu anayeitwa MELKIZEDEKI. Kama kuhani kumpatanisha Ibrahimu na Mungu kwa kitambo tu. Lakini ukuhani halisi ulikuwa bado haujafunuliwa.
Waebrania 7:1”Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki; 2 ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani; 3 hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwana Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele………………. Waebrania 7:15 “Tena hayo tusemayo ni dhahiri sana zaidi, ikiwa ametokea kuhani mwingine mithili ya Melkizedeki;[anazungumziwa YESU KRISTO] 16 asiyekuwa kuhani kwa sheria ya amri iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na ukomo; 17 maana ameshuhudiwa kwamba, Wewe u kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki”.
Waebrania 7:1”Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki;
2 ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;
3 hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwana Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele……………….
Waebrania 7:15 “Tena hayo tusemayo ni dhahiri sana zaidi, ikiwa ametokea kuhani mwingine mithili ya Melkizedeki;[anazungumziwa YESU KRISTO]
16 asiyekuwa kuhani kwa sheria ya amri iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na ukomo;
17 maana ameshuhudiwa kwamba, Wewe u kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki”.
Mahali pengine tena Neno lilipochukua umbile la kibinadamu, ni pale Shedraka, Meshaki na Abednego walivyotupwa kwenye tanuru la moto Likatokea kwa mfano wa mwana wa Mungu, likawa linazungumza nao kisha likaondoka..Kwasababu lilikuwa bado halijashuka rasmi duniani. Lakini utaona lengo lake ni lile lile kuleta uzima na kuokoa.
Sehemu nyingine lilitokea kama MWAMBA. Kule jangwani wana wa Israeli walipokuwa wanakaribia kufa na kiu lilisimama mbele yao ili kuwaokoa, Na Musa hakulifahamu hilo mpaka alipofanya uzembe ule wa kuupiga ule mwamba mara mbili ndipo alipojua kuwa kumbe alikuwa amesimama mbele ya uzima wenyewe, mbele ya mkombozi mwenyewe.
(1Wakorintho 10:4 “wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo”.)
➜Baadaye likaja kujidhihirisha katika maumbile mengi tofauti tofauti mfano kama Hekalu, Sehemu nyingine kama malaika, sehemu nyingine kama nguzo ya moto. Sehemu nyingine kama NYOKA WA SHABA.
(Yohana 3:14 “Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyohivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye”.)
➜Sehemu nyingine likajidhihirisha kama HEKIMA Ambayo aliwavaa waamuzi na wafalme wa Israeli akianziwa na Sulemani na wengineo waliomfuata, ili tu kutimiza lengo la kuwaokoa na kuwatunza watu wake kupita wafalme wale Mungu aliowachagua hekima yake ikae ndani yao.
Ukisoma Mithali sura ya 8 na ya 9 utaona kabisa jinsi Sulemani anavyoilezea hekima kama kitu chenye uhai na kinazungumza, Pia soma (1Wakorintho 1:24) utaona inamtaja KRISTO kama yeye ndio hiyo Hekima ya Mungu yenyewe.
Sehemu hizo hatuna muda wa kuzielezea moja moja, Lakini nataka uone picha Fulani hapo, NENO LA MUNGU jinsi lilivyopana, Na jinsi lilivyokuwepo tangu mwanzo. Hivyo baadaye sasa wakati ulipofika, Mungu kuufunua utimilifu wote, Mungu kuweka wazi WAZO lake lote kwa mwanadamu, Mungu kuufunua uzima wote na Ukombozi wote, akaona ni vyema sasa aunde mwili maalumu, mahususi, uzaliwe na mwanamke bikira, uitwe jina la YESU (Maana yake YEHOVA-MWOKOZI) ili sasa liweze kukaa na wanadamu milele, lizungumze nao, liwajibu maswali yao, liwafundishe, walipapase, walitegemee hilo, liwaongoze katika njia ya kweli na ya haki na ya uzima hata milele. Hapo ndipo tunaona Lile Neno ndani ya mwili unaoitwa Yesu…ambaye kwa ujumla sasa ndio tunamwita BWANA YESU KRISTO HALELUYA! HALELUYA!.
Yohana 1:14 “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli”.
Ndio maana mtume Yohana alikuwa anaoujasiri kabisa kusema maneno haya…
1Yohana 1:1 “Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima;2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);”
Sasa tukirudi kwenye zile kauli za Yesu anaposema kabla Ibrahimu hajawapo mimi nipo, hapo tunaona alikuwa hauongelei ule mwili uliozaliwa na bikira, bali alikuwa anaongelea lile Neno la Mungu ndani yake. Ukilijua hilo hutasema kuwa Mungu anazo nafsi tatu. Wewe na MAWAZO yako au NIA yako hamwezi kuwa vitu viwili tofauti vinavyojitegemea, ni kitu kimoja.Lile Neno ndio Mungu mwenyewe, Yesu Kristo ni Mungu ndani ya Mwili.
Hivyo ndugu tukirudi kwenye kichwa cha Somo je! Huyu Melkizedeki ni nani?. Jibu ni kuwa Huyu Melkizedeki ni Neno la Mungu lililojidhihirisha katika mwili kutimiza kusudi fulani kabla ya wakati wake mtimilifu. Lakini baadaye ndilo liliokuja rasmi kuitwa YESU KRISTO.Hata sasa tunaposema mkaribishe YESU Kristo ndani ya maisha yako, tunamaanisha likaribishe Neno la UZIMA la Mungu ndani ya maisha yako, Kwasababu Neno hilo sasa limefunuliwa ndani ya Kristo Yesu Bwana katika utimilifu wote. Kwahiyo unavyolisikia hili Neno na kulipokea, ni sawa umempokea Yesu Kristo mwenyewe ndani ya maisha yako…
Je! Leo hii bado Upo katika dhambi?, Na hali Tumesharahisishiwa wokovu namna hii bado unauona ni mgumu kuupokea?. Watu wa Agano la Kale japo walilifahamu hili Neno la Mungu kwa sehemu tu kwa kupapasapasa lakini walitii kwa utimilifu wote wakapata wokovu sisi je! Tutapataje kupona tusipouthamini wokovu mkuu namna hii?(Waebrania 2:3). YESU KRISTO ndio wazo la Mungu, ndio NIA ya Mungu, ndio MUNGU MWENYEWE katika Mwili. Tumfuate yeye tupate kuwa salama, katika safari yetu hii fupi hapa duniani.
Ubarikiwe sana.
NEHUSHTANI (NYOKA WA SHABA).
KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIANI?
MJUE SANA YESU KRISTO.
SIRI YA MUNGU.
Shalom mtu wa Mungu, karibu tujifunze tena maneno ya Mungu.
Kama wengi wetu tunavyojua kuwa, siku ya Bwana inakuja, siku ya hukumu yake ambapo Bwana atauhukumu ulimwengu kwasababu ya ubaya wake..(Isaya 13:11 inasema hivyo)
Na katika siku ya Mwisho,wafu wote watafufuliwa na Kiti cheupe cha Hukumu kitawekwa na Yesu Kristo ataketi juu yake, na kila mtu, mmoja baada ya mwingine atasimama mbele yake atoe hesabu ya mambo yake yote aliyoyafanya tangu siku alipozaliwa mpaka siku aliyokufa, yote hayo yatamulikwa katika kioo kikubwa sana, na kuonekana mbele ya watu wote na hapo ndipo kila mtu atapasa sifa yake, au aibu yake. (1Wakorintho 4:5)
Litaonekana tendo moja baada ya lingine, liovu au la haki litaonekana pale…kama mtu alikuwa ni mwasherati yataonekana matukio yote aliyoyafanya ya uasherati, siku aliofanya, mtu aliyefanya naye, mwaka, mwezi, mpaka dakika na sekunde alizokuwa anafanya…na watu wote wataona hakutakuwa na siri, kama mtu aliyafanya tendo Fulani la haki nalo pia litaonekana mwaka, siku, mpaka sekunde ya tendo hilo. Iwe alifanya kwa siri au kwa wazi yote yatakuwa bayana.
Na ni kwanini Mungu anataka watu wote waone?..Ni kwasababu yeye ni muhukumu wa haki na hivyo asitokee mtu yeyote atakayesema Yule kaonewa au Yule kapendelewa, watu wote watashuhudia matukio ya yaliyokuwa yanaendelea miongoni mwa watu.
Yohana 5: 28 “Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. 29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, NA WALE WALIOTENDA MABAYA KWA UFUFUO WA HUKUMU”.
Yohana 5: 28 “Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.
29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, NA WALE WALIOTENDA MABAYA KWA UFUFUO WA HUKUMU”.
Na Leo kwa Neema za Bwana tutaangalia ni kwa namna gani..MATUKIO(AU MATENDO) YA WANADAMU YANAVYOREKODIWA MBINGUNI.
Unajua unapoingia Benki au kwenye duka Fulani kubwa lenye bidhaa nyingi za thamani huwa wanaweka camera Fulani zizazorekodi matukio yote yanayoendelea kule ndani (CCTV). Wakati mwingine zinawekwa sehemu za kujificha wakati mwingine sehemu za wazi kabisa…
Sasa lengo la kuweka hizi camera kwa wazi ni ili watu wote wazione wanaoingia pale na waliopo kule ndani, ili wajue kuwa mambo yao yote wanayoyafanya yanarekodiwa na hivyo iwatengenezee hofu ya kutaka kujaribu aidha kuiba au kufanya kitendo chochote cha uhalifu. Hilo ndio lengo la hizo camera (CCTV) kuweka wazi. Ni ili mtu anapoingia na kuziona zile aingiwe na hofu ya kutaka kujaribu kufanya tukio lolote ovu..
Na ndivyo hivyo hivyo katika maisha haya…Tunapoingia katika huu ulimwengu Bwana Mungu ameweka camera yake juu inayorekodi mambo yote ya wanadamu tangu tunapozaliwa mpaka tunapokufa..na lengo la kuifanya ionekane ni ili watu waionapo waogope kufanya mambo maovu hapa duniani wakijua kuwa siku moja itaweka bayana matukio yote…Na hiyo camera (au CCTV) Ni huu MWEZI TUNAOUONA! Hapa juu ya vichwa vyetu..Huu mwezi tunaouona haupo tu pale juu kutufurahisha sisi wanadamu hapana! Au kutoa tu mwanga wakati wa usiku…ile ni camera Mungu aliyoiweka ionekane wazi ili watu tuogope kuishi maisha yasiyofaa hapa duniani.. Leo nitakuhakikishia kwanini Mwezi ni Camera ya huu ulimwenguni.
Kama ni mfuatiliaji mzuri wa mambo ya Sayansi…utakuwa umekutana au umewahi kusikia kitu kinachoitwa SATELLITE ( au satelaiti). Satelaiti ni kifaa cha kisayansi kinachowekwa juu sana (Maili nyingi sana angani)…ambacho kifaa hicho kinawekwa katika mfumo wa kuizunguka dunia kama vile mwezi unavyoizunguka dunia…Na kinakuwa na kazi nyingi tofauti tofauti…Lakini kazi kubwa satelaiti inayofanya ni KUREKODI NA KUPIGA PICHA ZA MATUKIO YANAYOENDELEA DUNIANI.
Kwa kutumia satelaiti mtu anaweza kukuona mpaka hapo ulipo na shughuli unazofanya si hivyo tu Satelaiti pia inauwezo wa kupiga picha za miji, na mienendo ya watu wengi na shughuli zao…unaweza kuchunguzwa hapo ulipo pasipo wewe kujijua kwa kupitia satellite…na inamatumizi mengine mengi tu.
Sasa wanasayansi walikitengeneza hichi kifaa kwa kujifunza tabia za mwezi, wakatumia fomula ile ile ya jinsi mwezi ulivyo juu na unavyozunguka dunia, wakaitumia na wao pia kupandisha kifaa chao hicho kama MWEZI WAO juu angani. Na kwasababu hiyo MWEZI huu tunaouona sisi wakaupa tafsiri ya kisayansi kuwa NI SATELAITI YA ASILI…Kwahiyo Wanasayansi hawaujui huu mwezi kwa tafsiri nyingine zaidi ya hiyo..wenyewe wanajua kuwa Mwezi ni satelaiti ya asili(kwa kiingereza natural satellite)…na hizo wanazozitengeneza wao wanazijua kama “satelaiti za kutengenezawa (kwa kiingereza artificial satellites)”. Kafuatilie jambo hilo utalielewa zaidi.
Sasa wao wameutafsiri mwezi kama SATELAITI YA ASILI, lakini hawajui kwanini wameutafsiri hivyo.. Lakini sisi Wakristo Bwana katupa macho ya rohoni kujua. Kama wao walitengeneza mwezi wao wa asili na kuupandisha juu sana, na kuzunguka dunia kwa lengo la kurekodi matukio yanayoendelea duniani..kadhalika na huu mwezi wa asili au satelaiti ya asili kama wanavyouita..unafanya kazi hiyo hiyo kama ya kwao…ya kurekodi matukio yote yanayoendelea duniani tena kwa ufasaha zaidi. Ingawa kwa namna ya macho ya kawaida huwezi kulihakiki hilo.
Ndugu yangu…MWEZI NI SATELAITI YETU. … TV unayoitazama matukio unayoyatazama Youtube na internet yote hayo ni kazi ya satellite, sasa hizi wakati mwingine hazina uwezo wa kuchukua kila tukio duniani vizuri…lakini hiyo satellite ya asili iliyotengenezwa na Mungu mwenyewe haina chenga hata kidogo..inarekodi kila kitu hata vile vya sirini.
Ndugu hakuna chochote unachoweza kukificha sasa, Mbingu na Nchi zinarekodi.. huu mwezi ni Jicho la Mungu ambalo kaliweka wazi ili watu wote waone, na wajue kuwa wanatazamwa juu, na waogope kufanya maasi…Waebrania 4:13 “…Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu”….Je! na wewe unaficha dhambi zako? Ni mwasherati kwa siri? Fahamu kuwa matendo yako yanarekodiwa juu, je! Ni mlawiti kwa siri? Mtazamaji wa pornography kwa siri?, ni mfanyaji masturbation kwa siri? Ni mwuaji kwa siri?, mchawi kwa siri? Mwizi kwa siri?…Tambua kwamba hakuna chochote unachoweza kukificha mbele za Mungu…
Siku ile mambo yako yote yatawekwa wazi screen itaonekana mbinguni ukiwa unafanya tukio moja baada ya lingine na utaambiwa ulitolee hesabu na utashindwa na utatupwa katika lile ziwa la Moto, huku moyoni ukijua kabisa umehukumiwa kwa haki…Mgeukie Muumba wako kabla siku za HUU MWEZI KUWA DAMU hazijafika. Kwasababu itafika siku Jua litatiwa giza na mwezi utakuwa mwekundu kama damu…kuashiria mwisho wa kumbukumbu za wanadamu…ndio maana kwenye mbingu mpya na nchi mpya hakutakuwa na MWEZI tena, kwasababu hakutakuwa na kurekodiwa tena kwa matukio ya watu kwasababu watu wote watakuwa wakamilifu.
Biblia Inasema katika Mithali 28: 13 “Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema. 14 Mwanadamu mwenye kicho yu heri sikuzote; Bali mshupavu wa moyo ataangukia madhara”.
Unaona inasema MSHUPAVU WA MOYO ATAANGUKIA MADHARA, Hayo madhara ni ZIWA LA MOTO
Ufunuo 21: 7 “Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu. 8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.
Ufunuo 21: 7 “Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.
8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.
Usizifiche dhambi zako leo kwasababu siku moja zitaanikwa mbele ya wote, Tubu leo kwa kukusudia kuziacha kuzifanya, unakusudia kuacha rushwa, ulevi, utukanaji, ulawiti, umalaya, utoaji mimba, uvaaji mbaya, anasa na mambo yote mabaya…Na Bwana atakupokea na kukupa Roho wake mtakatifu atakayekufanya usiwe na hamu ya kufanya hayo mambo tena..ili siku ile ya kutoa hesabu ya mambo yako yaonekane mambo mema tu! Huku
SWALI LA KUJIULIZA!
USILITAJE BURE JINA LA BWANA!
TULICHUNGUZE UMBO LA YESU NA MWENENDO WAKE.
NOTI YA UFALME WA MBINGUNI
Tukisoma biblia kwa utulivu tutagundua kuwa maandiko yamegawanyika katika sehemu kuu tatu, sehemu ya kwanza ni maandiko ambayo yamefunuliwa moja kwa moja kwa wakati wote, na ya pili ni maandiko ambayo yalikuwa yamefungwa lakini yakaja kufunguliwa baadaye. Na sehemu ya Tatu ni maandiko ambayo yalionekena tu kwa sehemu lakini yakaja kufungwa tena.
Ni vizuri tukalielewa hilo ili tusiichukulie biblia kirahisi rahisi tu au kama kitabu kingine chochote cha kawaida ambacho hakina habari mpya ndani yake.
Sasa Maandiko yaliyofunguliwa moja kwa moja kwa wakati wote ndio yapi?, ndio haya ambayo kwa sehemu kubwa mimi na wewe tunayafahamu, ni maandiko ambayo yapo wazi, yalinakiliwa katika vitabu mtu yeyote anaweza akasoma na kwa kupitia hayo akamwomba Mungu na Mungu akamfunulia hekima iliyopo ndani yake, kwamfano unaposema vitabu vya Torati vyote, unaposoma vitabu vya wafalme, Ayubu, Esta, Zaburi, Yeremia, Isaya, Ezekieli, unaposoma vitabu vya Injili ya Yesu Kristo na Injili ya Mitume, n.k. vyote hivyo ni vitabu vilivyofunuliwa kwetu kwa wakati wote havina masharti Fulani au makomeo au mipaka. Yaani kwa lugha rahisi ni vitabu vinavyotufaa kwa wakati wote, kufundishia, kuonya na kufariji, kujenga n.k..sawasawa wakolosai 3:16
Lakini pia kuna aina nyingine ya maandiko ambayo hayo yalikuwepo tangu zamani, yalikuwa yamefungwa mpaka ulipofika wakati Fulani wa kufunuliwa..Na mfano wa haya tunaona ni kile kitabu cha Mihuri 7 katika kitabu cha Ufunuo mlango wa 6 ambacho kilikuwa kimetiwa muhuri ndani na nje, siri zilizokuwa ndani yake, hazikuwahi kujulikana na mtu yeyote mpaka wakati wa kufunuliwa kwake ulipofika, na tunasoma ni Yesu peke yake ndiye aliyestahili kuivunja mihuri ya kile kitabu na kwa kupitia ufunuo ule mkubwa ndipo tulipofahamu sisi ni akina nani, ndipo tulipofahamu tulipotoka na tunapokwenda, ndipo tulipofahamu mwenenendo wa yule mpinga-kristo, Yule Asi, jinsi atakavyoanza mpaka atakapomaliza na mahali kiti chake cha enzi kilipo, atakapotokea na atakapoishi. Mambo hayo hayakujulikana hapo kabla..Isipokuwa kwa wakati husika..
Vile vile yapo maandiko mengine ambayo, yaliyoonekana kwa sehemu tu na baadhi ya watu lakini yalifungwa mpaka wakati husika uliowekwa Na ndio maana utasoma Danieli aliambiwa..
Danieli 12:3 “Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele. 4 Lakini wewe, Ee Danieli, YAFUNGE MANENO HAYA, UKAKITIE MUHURI KITABU, HATA WAKATI WA MWISHO; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka”.
Danieli 12:3 “Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele.
4 Lakini wewe, Ee Danieli, YAFUNGE MANENO HAYA, UKAKITIE MUHURI KITABU, HATA WAKATI WA MWISHO; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka”.
Sasa tunaona watu hawa walipotaka kuyarekodi katika biblia walikatazwa wakaambiwa wasiyaandike kwanza, kwani hayo yametengwa mahususi kwa wakati Fulani wa mwisho. Ndugu nataka nikuambie, Mungu anayo Agenda yake kama vile ibilisi alivyo na Agenda yake, Sio kila siri ya ufalme wa mbinguni imerekodiwa katika kitabu hichi cha biblia, mambo mengine Mungu karuhusu makusudi yafichwe kwasasa, ili shetani asielewe chochote Mungu alichokipanga, Embu fikiria maneno yale Bwana Yesu aliyoyasema, msitupe Lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.. Ikiwa Mungu ameruhusu sio kila jambo la ufalme wa mbinguni tutalifichua kwa kila mtu tu, kwanini na yeye asitenge fungu lake kwa ajili ya familia yake tu?.
NGURUMO SABA ZIPO MBIONI KUTOA SAUTI ZAO.
Tunaona Yohana alipokuwa Patmo, alionyeshwa maono mengi sana na Bwana Yesu Kristo, na mengi ya hayo aliambiwa ayaandike, ikiwemo ufunuo wa yale makanisa 7 na jumbe zao, ikiwemo baragumu saba, na vitasa saba, Lakini alipofika kwa Yule malaika mwenye nguvu sana aliyeshika kile kitabu kidogo, alipolia na ngurumo saba kutoa sauti zake alipotaka kuandika, alikatazwa asiandike. .Tunasoma hayo katika Ufunuo mlango wa kumi:
Ufunuo 10: 1 “Kisha nikaona malaika mwingine mwenye nguvu akishuka kutoka mbinguni, amevikwa wingu; na upinde wa mvua juu ya kichwa chake; na uso wake ulikuwa kama jua, na miguu yake kama nguzo za moto. 2 Na katika mkono wake alikuwa na kitabu kidogo kimefunguliwa. Akaweka mguu wake wa kuume juu ya bahari, nao wakushoto juu ya nchi. 3 Naye akalia kwa sauti kuu, kama simba angurumavyo. NA ALIPOLIA, ZILE NGURUMO SABA ZIKATOA SAUTI ZAO. 4 Hata ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nalikuwa tayari kuandika. Nami nalisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, YATIE MUHURI MANENO HAYO YALIYONENWA NA HIZO NGURUMO SABA, USIYAANDIKE”.
Ufunuo 10: 1 “Kisha nikaona malaika mwingine mwenye nguvu akishuka kutoka mbinguni, amevikwa wingu; na upinde wa mvua juu ya kichwa chake; na uso wake ulikuwa kama jua, na miguu yake kama nguzo za moto.
2 Na katika mkono wake alikuwa na kitabu kidogo kimefunguliwa. Akaweka mguu wake wa kuume juu ya bahari, nao wakushoto juu ya nchi.
3 Naye akalia kwa sauti kuu, kama simba angurumavyo. NA ALIPOLIA, ZILE NGURUMO SABA ZIKATOA SAUTI ZAO.
4 Hata ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nalikuwa tayari kuandika. Nami nalisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, YATIE MUHURI MANENO HAYO YALIYONENWA NA HIZO NGURUMO SABA, USIYAANDIKE”.
Ni mambo nyeti sana na ya kutisha vile vile, kwasababu siku zote ngurumo mara nyingi kwenye biblia inaashiria hukumu ya Mungu, sasa hizi ngurumo 7 (ambazo ni Huduma 7/watu 7) zitapoanza kutoa sauti zao, kwa kupitia maubiri hayo ambayo yatasikika ulimwenguni kote, Nguvu ya Mungu itashuka kwa namna ya ajabu juu ya watu wengi wanaume kwa wanawake waliochaguliwa…. ndugu yangu, masikio ya wengi yatawasha, kwasababu mambo yatakayosikiwa yatakuwa ni mpya yatakayoambatana na hukumu na mapigo. Wanaoichezea madhabahu ya Mungu sasahivi na wakiona hakuna chochote kinachotokea siku hiyo ndio watayapojiona kuwa wao kumbe walikuwa ni takataka mbele za Mungu, watajihukumu wenyewe kabla hata ya kufika kwa Mungu, wao wenyewe watakiri kuwa hawakuwa watumishi wa Mungu kwa jinsi mambo yatakayokuwa yanasemwa na hiyo nguvu ya uamsho wa ajabu itakayokuwa inatembea katikati ya Kristo na Bibi-arusi wake duniani.
Zekaria 13:3 “Tena itakuwa ya kwamba, mtu awaye yote atakapotoa unabii, basi baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, Hutaishi; kwa maana unanena maneno ya uongo kwa jina la Bwana; na baba yake na mama yake waliomzaa watamtumbua atoapo unabii. 4 Tena itakuwa siku hiyo, ya kwamba manabii, kila mmoja wao, atayaonea haya maono yake atoapo unabii; WALA HAWATAVAA JOHO YA NYWELE ILI KUDANGANYA WATU; 5 bali atasema, MIMI SI NABII KAMWE; mimi ni mkulima wa nchi; kwa maana nalifanywa mtumwa tokea ujana wangu”.
Zekaria 13:3 “Tena itakuwa ya kwamba, mtu awaye yote atakapotoa unabii, basi baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, Hutaishi; kwa maana unanena maneno ya uongo kwa jina la Bwana; na baba yake na mama yake waliomzaa watamtumbua atoapo unabii.
4 Tena itakuwa siku hiyo, ya kwamba manabii, kila mmoja wao, atayaonea haya maono yake atoapo unabii; WALA HAWATAVAA JOHO YA NYWELE ILI KUDANGANYA WATU;
5 bali atasema, MIMI SI NABII KAMWE; mimi ni mkulima wa nchi; kwa maana nalifanywa mtumwa tokea ujana wangu”.
Huu ni unabii Zekaria aliopewa wa kipindi hicho kinachokuja, kutakuwa na utiisho mkubwa katika kanisa la Mungu ambao haujawahi kuwepo, zaidi hata ule wa Petro alipokutana na Anania na Safira, walipoanguka na kufa baada ya kumwambia uongo Roho Mtakatifu, utakuwa ni mkubwa kuliko huo.
Kutakuwa na ishara na miujiza ya ajabu ambayo haijawahi kurekodiwa katika historia yoyote ya kanisa, Mungu atafanya mambo ambayo kila jicho litashangaa, na Mungu atafanya hivyo kumpa Bibi-Arusi wake imani ya kunyakuliwa, hapo ndipo sehemu ya pili ya ule unabii wa Yoeli wa mambo yatakayotokea siku za mwisho utatimia.
Matendo 2:19 “Nami nitatoa ajabu katika mbingu juu, na ishara katika nchi chini, damu na moto, na mvuke wa moshi 20 Jua litageuka kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo kuu na iliyo dhahiri 21 Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa”.
20 Jua litageuka kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo kuu na iliyo dhahiri
21 Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa”.
Hayo yote yatatimia katika wakati huo, na hiyo itafanyika ndani ya kipindi kifupi sana, na ghafla utanyakuo utapita.
Dunia itabakia imeduwaa ikijiuliza ni nini hiki.. Na ndio maana mambo hayo yalihifadhiwa yasijulikane kwanza, na pia kumbuka kutatamkwa mambo mapya kabisa ambayo hutaweza kuyapata katika biblia, lakini hiyo haimaanishi kuwa yatapingana na Biblia hapana, bali yatakuwa mapya na sio wote watakayo yapokea isipokuwa wale wanawali werevu tu, ambao Mungu mwenyewe atawapa hekima ya kuyapokea. Huo ndio wakati Danieli aliosema Maarifa yataongeza, watu wote wa Mungu wataongezewa maarifa ya kumjua Mungu kwa kiwango cha ajabu.
Hivyo ndugu, ikiwa bado haupo ndani ya wokovu, unasubiria nini wakati huu wa neema sasa? Kumbuka Jambo hilo litakapotokea halitamuhusu kila mtu duniani bali watu ambao tayari walishaanza kutembea na Mungu tayari huko nyuma, watu waliopokea ubatizo wa Roho Mtakatifu, Watu wanaotambua majira wanayoishi, Wengine wote hawataelewa chochote wala hawatasaidiki kwasababu Yule ROHO anayewavuta watu kumwamini yeye atakuwa hayupo ndani yao.
Ukiyajua haya, ufanye uteule wako imara sasa, tubu anza kutembea na Mungu katika muda huu mfupi uliobaki, kabla ya siku za hatari hazijaanza. Kwani kwa jinsi mambo yanavyoonekana tusitazamie sana vizazi vingine mbele yetu, hichi kizazi tunachoishi mimi na wewe kinaweza kushuhudia hayo yote.
Ubarikiwe.
MIHURI SABA
HISTORIA YA WILLIAM BRANHAM
NGURUMO SABA
MIISHO YA ZAMANI.
NGUVU ZA ZAMANI ZIJAZO:
WhatsApp
Shalom, Mtu wa Mungu karibu tujifunze Neno la Mungu, Taa pekee ya kweli iongozayo miguu yetu.
Leo kwa ufupi tutajifunza ni kwanini Mwanamume hapaswi kuvaa mavazi yampasayo mwanamke, kadhalika na mwanamke hapaswi kuvaa mavazi yampasayo mwanamume.
Neno hilo linapatikana katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati 22:5 “ Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo NI MACHUKIZO KWA BWANA, MUNGU WAKO.”
Jambo la msingi na muhimu ambalo watu wengi hatulifahamu kuhusu huu mstari ni kuwa Biblia haijasema hapo, mwanamume au mwanamke asivae mavazi yaliyotengenezwa mahususi kwa jinsia nyingine hapana bali imesema “YAMPASAYO”.
Neno yampasayo ni Neno linalohusiana na maumbile, yaani mavazi yanayopatana na maumbile ya mtu husika…
Kwamfano maumbile ya mwanamume ni ya misuli, na ukomavu kidogo, na yasiyo na mvuto hivyo mavazi yake yanapaswa yawe yanaendana na jinsi mwili wake ulivyotengenezwa, kadhalika na mwanamke mwili wake ni mlaini kidogo na umbo lake ni la kipekee tofauti na mwanamume hivyo na mavazi yake yanapaswa yaendane na jinsi mwili wake ulivyotengenezwa.
Kwahiyo mwanamume umbile lake linamlazimu avae suruali, wakati mwingine na nguo ngumu hayo ndio mavazi yanayoendana na mwili wake..Na kadhalika mwanamke hana sababu ya kuvaa suruali kwasababu umbile lake sio sawa na la mwanamume..yeye nguo zake ni magauni mazuri, marefu yaliyotengenezwa kwa ustadi mbali mbali ambayo yanamsitiri na sketi zenye heshima…hayo ni mavazi yanayompasa mwanamke
Sasa kwanini ni machukizo kuvaa nguo zisizoupasa mwili wako, leo tutajua ni kwanini ni machukizo..
Machukizo maana yake, ni kitu kinachochukiza, Mfano ukifanya kitu usichokitaka au usichokipenda maana yake hicho kitu kitakuchukiza, na kama tayari kimeshakuchukiza hapo ni rahisi kuchukua uamuzi wowote aidha kukasirika au kutengana na hicho kitu. Huo ni mfano tu!…Na tabia nyingine ya kitu kinachokuchukiza ni kwamba mtu mwingine anaweza asione kama kinakuchukiza, jambo linalokuchukiza wewe kwa watu wengine linaweza kuonekana kama ni jambo la kawaida.
Na ndivyo hivyo hivyo kwa Mungu wetu tunavyoonekana, tunafanya kitu kinachomchukiza tunapovaa mavazi yasiyopasa maumbile yetu. Unaweza ukaona hakuna shida kufanya hivyo lakini ni machukizo. Ni kitu kinachomuudhi sana Mungu ndani ya moyo wake.
Unakumbuka pale Edeni, Adamu na Hawa baada ya kuasi wakashona majani wakajitengenezea mavazi ya majani?…wao waliona wamejisitiri na kupendeza lakini mbele za Mungu wote wawili walikuwa wamevaa mavazi yasiyowapasa na hivyo Mungu hakupendezwa na yale mavazi akawatengenezea mavazi mengine ya ngozi.
Kwahiyo ni machukizo makubwa sana kuvaa mavazi yasiyoupasa mwili wako, jaribu kufikiri leo labda simba wamepewa akili kama mwanadamu..halafu unakwenda porini na kukuta simba kavaa ngozi ya fisi, au unamwona simba jike kaota zile nywele za shingoni kama za simba dume, na simba dume hana zile nywele..Unaona ni kitu kisicholeta picha nzuri ni kitu cha kuchukiza.
Na ndio hivyo hivyo tunavyoonekana mbele za Mungu..
Sasa hivi utakwenda kila mahali mpaka kanisani utakuta wanawake wamevaa suruali, na ukijaribu kuuliza atakwambia hizi ni suruali za kike kwahiyo hazina shida!! Dada yangu mpendwa…shetani asikupofushe macho, hakuna suruali za kike, suruali zote ni za kiume zilitengenezwa mahususi kufuatia maumbile ya wanaume soma kutoka 28:42-43 utathibitisha hilo…sio kwasababu na wewe dada una miguu miwili iliyogawanyika kama mwanamume ndio iwe sababu ya wewe kuvaa suruali, ndugu usidanganyike…hata simba jike ana kichwa kama cha simba dume lakini yale manyoya ya kichwa yamewekwa mahususi kwa ajili ya maumbile ya kichwa cha simba dume tu!!..Kwahiyo usijaribu kulinganisha vitu bila hekima ya macho ya rohoni..Hizi ni siku za mwisho, shetani anakuja kwa ujanja mwingi sana ambao usipokuwa makini unachukuliwa nao.
Hivi unajua kuwa siku hizi kuna SIDIRIA ZA KIUME PIA??…Kama ulikuwa hulijui hilo, hebu katafute kulijua, zipo sidiria za kiume na zinauzwa bei ghali sana, nyingine mpaka kufikia sh. Laki moja za kitanzani, na nyingine zaidi ya hapo, na zipo za mitindo tofauti tofauti.. unaweza ukazi-search kwenye google utaziona, na tena zina maua maua kama zile za wanawake, na zinavalika sana na kuuzika sana duniani, na zinaheshimika…Na watu wanazivaa kama fashion, nk.
Sasa hebu nikuulize wewe mwanamke, umekwenda kanisani na kukuta mchungaji kavaa hiyo sidiria ya kike halafu anakuhubiria na anakwambia hii haina shida! Ni sidiria ya kiume haina tatizo!! Je! Utamwamini?…si utasema dunia imeisha??…Kadhalika na wewe usidanganywe na kuambia ‘‘kuna suruali za kike’’.
Kama mchungaji wako havai sidiria za kiume madhabahuni asikudanganye na wewe uvae suruali za kike kanisani au nje ya kanisa, kama yeye haweki hereni, mabangili, hapaki wanja, lipstick wala havai sketi za kiume ambazo zipo na watu wanazivaa…basi asikudanganye na wewe uning’inize mambo hayo katika mwili wako…Biblia inasema mwanamke avae mavazi ya KUIJISITIRI, na sio ya Kuficha sehemu za siri (1Timotheo 2:9)..Suruali yoyote inafunua maumbile ya mwanamke, hivyo haiwezi kumsitiri, Kwanini avae?
Weka mbali vimini, weka mbali tattoo, weka mbali hereni, mawigi, suruali.. na kila aina ya fashion za ulimwengu huu..Biblia inasema aupendaye ulimwengu hata kumpenda Mungu hakupo ndani yake…
Jehanamu ipo!! Sio hadithi za kutunga..Ni kweli ipo! Ni kitu halisi na dhahiri kabisa..Na ni maelfu ya watu shetani anaofanikiwa kuwapeleka huko.
Ni matumaini yangu kuwa Bwana atakupa macho ya kuliona hilo, ili uiepuke ghadhabu yake..
Bwana azidi kukubariki sana.
MAVAZI YA NDANI NA YA NJE.
WEWE NI HEKALU LA MUNGU.
JE! KUCHORA TATTOO NI DHAMBI?
MWANAMKE YEZEBELI
KUZIMU NI MAHALI PA NAMNA GANI, JE! HUKO WANAISHI WATU WAKIFA NA KWENDA KUPATA MATESO AU NI VINGINEVYO?
Chachu ni nini?. Chachu kwa lugha ya sasa ni HAMIRA, na kwa kawaida ukiitazama hamira unaweza ukadhani ni unga Fulani hivi, lakini kiuhalisia ule si unga bali ni mkusanyiko wa wadudu wenye uhai kwa lugha ya kitaalamu wanaitwa YEAST, hawa wanadudu ndio wanaofanya kazi ya kumengenya ule unga, na kutoa gasi maalumu ambayo ndiyo inaufanya ule unga uumuke. Kwahiyo hamira sio kama chumvi au sukari ambavyo havina uhai ndani yake, Hamira ni kitu chenye uhai kwasababu ni wadudu wale. Na ndio maana ikiwekwa mahali inaweza kubadili maumbile ya kitu na kukifanya kuwa kingine kabisa..
Kwamfano unga wa ngano ukitiwa hamira, ukila kalmati sio sawa na utakavyokula keki, na sio sawa na utakavyokula tambi au maandazi. Yote hii inafanywa na kazi moja ya Hamira (CHACHU). Kubadilisha maumbile.
Na ndio maana Bwana alitumia Neno “chachu” kuonyesha madhara yanayoweza kumtokea mtu asipojihadhari na hayo atakayoonywa.
Tukisoma.
Marko 8:15 inasema “Akawaagiza, akasema, Angalieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode”.
Mathayo 16:12 “Ndipo walipofahamu ya kuwa hakuwaambia kujilinda na chachu ya mkate, bali na mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo”.
Mahali pengine anasema:
Luka12 :1 “Wakati huo, makutano walipokutanika elfu elfu, hata wakakanyagana, alianza kuwaambia wanafunzi wake kwanza, Jilindeni na chachu ya Mafarisayo, ambayo ni UNAFIKI”.
Kwahiyo kumbe chachu anayoisemea alikuwa anamaanisha kuwa ni MAFUNDISHO YA KINAFKI. Ambayo yanaletwa na hayo makundi mawili, kundi la kwanza ni watu wa kidini na kundi la Pili ni wana SIASA.
Na leo kwa neema za Mungu tutaliangalia zaidi hili kundi la PILI. Tunajua makundi yote haya wakati wa BWANA YESU na ule wa mitume yote yalifanyika kuwa maadui wakubwa wa kazi ya Mungu, tunaona wakati tu Bwana Yesu anazaliwa Herode alitaka kumuua lakini mpango wake ukashindikana, baadaye mtoto wake akafanikiwa kumuua Yohana Mbatizaji, na ndio huyo huyo alitaka tena kuja kumuua Yesu, lakini Yesu alimwita Mbweha..halikadhalika mafarisayo na waandishi walikuwa wanamvizia siku zote za huduma yake wamwangamize mpaka baadaye mwishoni wakafanikiwa wote wawili kuungana (yaani Herode na mafarisayo) ili kumuua YESU.
Lakini heri wangekuwa wanafanya vile kwa ujinga, Lakini Bwana alikuwa anasema wanafanya kinafki, ikiwa na maana kuwa wale ambao wangepaswa wawe watenda haki na watunza sheria za Imani na za nchi wao ndio wanaokuwa wa kwanza kutokusimamia haki, kwa nje wanaonekana ni watenda haki na wanasiasa bora lakini kumbe ndani yao ni wanafki…Na kwasababu hiyo basi Yesu akawaonya wanafunzi wake wajitenge na njia zao, kwasababu kama wakiambatana nao, wao pia muda si mrefu wategeuzwa kwa unafki wao na kufanana nao, na mwisho wa siku watajikuta wanamkosea Mungu.
Jambo hilo hilo tunaonywa hata na sasa, TUJIEPUSHA NA WANASIASA, sio kwamba tusionge nao kabisa, au tusile nao au tusialikwe nao hapana…Bali tusikubali CHACHU yao iingie ndani yetu.. Kwasababu hiyo inaweza ukatubalisha maumbile yetu ya kiroho na kuwa watu tofauti kabisa, tofauti na tulivyokuwa hapo mwanzo. Na sisi tutaanza kuwa wanafki, tutaanza kufanana na wao,.na mwisho wa siku tutaangamia.
Hilo ni kosa mojawapo linalofanywa na watumishi wengi wa Mungu sasa, ikiwa Mungu amekupa ujumbe kwa mwanasiasa, basi utoe kulingana na maagizo ya ki-Mungu, na usiwe wakati wa wewe kila jambo la kisiasa upo, kampeni upo, jeshi la polisi upo, bungeni upo, ..n.k..vikao vya kisiasa mtaani kwako upo, mijadala ya kisiasa upo, Hayo ni mambo ambayo kwa nje unaweza ukaona upo sahihi lakini nyuma yake unajiangamiza mwenyewe.
Ukiwa umeamua kuwa mtumishi wa Mungu, na mtumishi wa Mungu siye anayehubiri tu madhabahuni, bali yeyote Yule anayemtumikia Mungu kwa karama aliyopewa (huyo ni mtumishi wa Mungu) weka mbali mambo ya SIASA, tuwache wao na shughuli zao na sisi tuendelee na shuhuli zetu za kutangaza habari za haki, na injili..Na ndivyo tutakavyo fanikiwa kutumika pasipo kujikwaa.
1Wakorintho 5:7 “ Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo; 8 basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli”.
1Wakorintho 5:7 “ Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;
8 basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli”.
MANA ILIYOSHUSHWA KUTOKA MBINGUNI.
NINI TOFAUTI KATI YA MYUNANI, MFARISAYO NA MSADUKAYO.
WAFAHAMU MANABII WA UONGO
TUSIFUNGWE NIRA PAMOJA NA WASIOAMINI.
Bwana wetu YESU KRISTO apewe sifa, Karibu katika mfululizo wa mwendelezo wa kitabu cha ufunuo leo tukiwa katika sura ya 22 na ya mwisho, Tusome..
Ufunuo 22
1 Kisha akanionyesha MTO WA MAJI YA UZIMA, wenye kung’aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo, 2 katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo MTI WA UZIMA, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa. 3 Wala hapatakuwa na laana yo yote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo ndani yake. Na watumwa wake watamtumikia; 4 nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao. 5 Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele. 6 Kisha akaniambia, Maneno haya ni amini na kweli. Naye Bwana, Mungu wa roho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi.
1 Kisha akanionyesha MTO WA MAJI YA UZIMA, wenye kung’aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo,
2 katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo MTI WA UZIMA, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.
3 Wala hapatakuwa na laana yo yote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo ndani yake. Na watumwa wake watamtumikia;
4 nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao.
5 Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele.
6 Kisha akaniambia, Maneno haya ni amini na kweli. Naye Bwana, Mungu wa roho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi.
Tukirejea kidogo kwenye historia ya Edeni, tunafahamu kuwa katikati ya Bustani, kulikuwa na ule mti wa uzima, na pia kulikuwa na mto kando ya mti wa uzima ambao ulikuwa unaitilia bustani yote maji, na kisha baada ya hapo uligawanyika na kuwa vichwa 4 (Mwanzo 2),ambavyo vilikwenda kuimwagilia dunia yote. Hivyo tunajua kuwa ule mti wa uzima, haukuwa mti kama mti wa matunda ya asili kama vile zabibu au peasi, la! bali ulikuwa ni mti wa rohoni, ambao matunda yake mtu akila anapata uzima wa milele, vyakula vya mwilini haviwezi kumpa mtu uzima wa milele, ukisoma kwa makini pale utaona Mungu alichepusha miti ya aina tatu: wa kwanza ulikuwa ni kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa(haya ndio matunda ya asili kama vile zabibu, embe, tufaa, n.k.)..aina ya pili ni mti wa uzima, na aina ya tatu ni mti wa ujuzi wa mema na mabaya,(Mwanzo 2:9), sasa hii miti aina 2 za mwisho ni miti ya rohoni.
Hivyo ule “mti wa uzima” ulikuwa ni NENO LA MUNGU ambao ndio baadaye ulikuja kuuvaa mwili ukaitwa YESU KRISTO, Sasa hili NENO LA MUNGU ndilo lililokuwa sheria na maagizo yote ambayo Adamu na Hawa walipewa na Mungu ili wakidumu katika hayo waishi milele. Hivyo pale Edeni Adamu na Hawa walikula matunda ya kawaida ya asili pamoja na maji ya asili kuwapa uzima miili yao, lakini pia walikula chakula cha rohoni (Matunda ya mti wa uzima), na maji ya rohoni, kuwapa uzima katika roho zao.
Lakini baada ya Adamu kuasi(kukaidi sheria ya MUNGU) tunaona njia ya mti wa uzima ilifungwa(kumbuka mti wenyewe haukuondolewa), ilipofika wakati uliokusudiwa ile njia ilifunguliwa tena, na tunajua huyu si mwingine zaidi ya BWANA wetu YESU KRISTO, Yohana 14:6″Yesu akamwambia, Mimi ndimi NJIA, na kweli, na UZIMA; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. ”
Hivyo YESU KRISTO ni NENO/maagizo yale yale ya Mungu yaliyouvaa mwili.
Yeye ndiye ule mti wa uzima, na pia ndio anayetoa yale maji ya uzima.
ukisoma Yohana 4:14″
13 Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena;
14 walakini ye yote atakayekunywa MAJI YALE nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia UZIMA WA MILELE. “
Sasa tukirudi juu, katika kitabu cha UFUNUO, tunasoma..
1 Kisha akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye kung’aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo,
Hapa tunaona mto wa maji ya uzima unaonekana ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha mwanakondoo, kumbuka kama tulivyosoma katika sura iliyopita kwamba katika ile Yerusalemu mpya(ambayo ni BIBI-ARUSI) ndipo patakapokuwa makao ya Mungu
(Ufunuo 21:3-4″Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, TAZAMA, MASKANI YA MUNGU NI PAMOJA NA WANADAMU, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. ),
hivyo kiti chake cha enzi cha Mungu kitakuwepo huko, Na MTI wa UZIMA pamoja na mto wa maji wa uzima utatokea huko.
Kwahiyo bibi-arusi wa Kristo ambaye ndo ile Yerusalemu mpya na ndio watu wale wote watakaoshinda kutoka katika nyakati mbalimbali za Kanisa, Kama Bwana Yesu alivyoahidi katika Ufunuo 2:7 “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu. ”
Hii Ikiwa na maana kuwa wale watakaoshinda tu ndio watakula mema yote na kuzishiriki baraka zote ambazo Mungu alimwahidia YESU KRISTO atakapokuja kuumiliki ulimwengu, Yaani kwa lugha rahisi hawa watu watakatifu watafanana na YESU KRISTO mwenyewe. Kwa kuwa maisha yao walipokuwa hapa duniani yalifanana sana na mwana wa Mungu, hivyo watavuna walichokipanda kwa kula matunda yake.(yaani matunda ya mti wa uzima-YESU KRISTO mwenyewe.)
Lakini pia majani yatakuwa ni ya kuwaponya mataifa, kama tunavyofahamu mti wowote wa matunda, kwa mfano mti wa mwembe, huwezi ukala majani, ukasema, huu mwembe ni mzuri pengine yanaweza kukusaidia kama dawa ukiyatwanga, au kuongeza tu virutubisho fulani mwilini, lakini anayekula EMBE ndie anayejua uzuri wa mwembe, Vivyo hivyo kwa YESU KRISTO yeye kama mti wa UZIMA matunda yake watakayoyafurahia aliyopewa na BABA yake ni BIBI-ARUSI tu, wengine wote watamfahamu YESU katika sehemu ya matawi yake, kama biblia inavyosema yatakuwa ni kwa ajili ya kuwaponya tu, waendelee kuishi milele, lakini BIBI-ARUSI atakuwa na vyote.
Kama ilivyokuwa katika bustani ya Edeni mto ulitoka katika bustani na kusambaa duniani kote, vivyo hivyo na huu mto utokao katika kiti cha Enzi cha mwanakondoo katika ile YERUSALEMU MPYA, maji yake yatasambaa ulimwenguni kote kuwanywesha mataifa, ikiwa na maana kuwa yale maji ya uzima ambayo chanzo chake ni YESU KRISTO, kwa kupitia bibi-arusi wake, yataenea duniani kote kwa kufundisha mataifa kanuni zote za Mungu na utukufu wake.
Hivyo hawa watu ambao wanaunda huu mji Yerusalemu mpya, watakuwa wametawanyika duniani kote . Unaona uzuri wa kuwa bibi-arusi wa Kristo? Kama dunia ya leo ni wasomi tu, ndio wanaotoa mwongozo wa mataifa ya dunia na kupewa kipaumbele, vivyo hivyo na kule ni BIBI-ARUSI tu, ndiye atakayetawala na KRISTO, na litakuwa ni kundi dogo, ni kwa wale watakaoshinda tu!
Tukiendelea..
Ufunuo 22:7-21 “7 Na tazama, naja upesi; heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki. 8 Nami Yohana ndimi niliyeyasikia na kuyaona mambo hayo. Na hapo nilipoyasikia na kuyaona nalianguka, ili nisujudu mbele ya miguu ya malaika yule mwenye kunionyesha hayo. 9 Naye akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako, na wa ndugu zako manabii, na wa wale wayashikao maneno ya kitabu hiki. Msujudie Mungu. 10 Akaniambia, Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia. 11 Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa. 12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. 13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. 14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.
Ufunuo 22:7-21 “7 Na tazama, naja upesi; heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki.
8 Nami Yohana ndimi niliyeyasikia na kuyaona mambo hayo. Na hapo nilipoyasikia na kuyaona nalianguka, ili nisujudu mbele ya miguu ya malaika yule mwenye kunionyesha hayo.
9 Naye akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako, na wa ndugu zako manabii, na wa wale wayashikao maneno ya kitabu hiki. Msujudie Mungu.
10 Akaniambia, Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia.
11 Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.
12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.
14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.
Ndugu hapa Bwana anatoa angalizo, Hili neno “TAZAMA NAJA UPESI” ..na thawabu yangu ipo mkononi mwangu kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo, Linaonyesha kwamba wakati umeisha, je! wewe kazi yako ni ipi?, je! umeipima thawabu yako?, je! unastahili kuitwa bibi-arusi ?, je! kazi yako inakupeleka mbinguni au kuzimu?.
maana hapa anaendelea kusema…
15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya. 16 Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi. 17 Na “ROHO na BIBI-ARUSI” wasema, NJOO! Naye asikiaye na aseme, NJOO! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.
15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.
16 Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi.
17 Na “ROHO na BIBI-ARUSI” wasema, NJOO! Naye asikiaye na aseme, NJOO! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.
Huu ni wakati wako wewe mkristo uliyevuguvugu, kimbilia kwenye chemchemi ya maji ya uzima unywe maji yaliyo hai na ufue nguo zako, ufanyike kiumbe kipya, wakati umeisha Bwana yu karibu kurudi.
Hivyo ni vyema kujua kalenda ya Mungu na ujumbe wa Mungu kwa wakati tunaoishi. Kwa kulijua hilo utaishi maisha ya uangalifu tukijua kuwa BWANA wetu yu karibu kurudi kumchukua bibi-arusi wake safi asiye na hila wala mawaa.
Bwana anaendelea kusema…
18 Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. 19 Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki. 20 Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; naja upesi. Amina; na uje, Bwana Yesu. 21 Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi nyote. Amina. Huu ni wakati wa kupiga mbio kweli kweli tuhakikishe hatukosi kuwa katika hiyo YERUSALEMU MPYA bibi-arusi wa Kristo ambayo Bwana anaendelea kuiandaa hadi sasa, na watakaokuwa huko ni kundi dogo, biblia inasema..
19 Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.
20 Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; naja upesi. Amina; na uje, Bwana Yesu.
21 Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi nyote. Amina.
Huu ni wakati wa kupiga mbio kweli kweli tuhakikishe hatukosi kuwa katika hiyo YERUSALEMU MPYA bibi-arusi wa Kristo ambayo Bwana anaendelea kuiandaa hadi sasa, na watakaokuwa huko ni kundi dogo, biblia inasema..
Waebrania Mlango 12:
1 Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu, 2 tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu. 3 Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu. “
1 Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,
2 tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.
3 Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu. “
Amen.
Maran Atha!
Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara, kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.
MWISHO WA MAELEZO JUU YA KITABU CHA UFUNUO.
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Zinazoendana..
MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA.
NINI MAANA YA USIPUNGUZE WALA USIONGEZE NENO LA MUNGU?
Rudi Nyumbani.
Bwana YESU KRISTO atukuzwe, Karibu katika mafunzo ya kitabu cha Ufunuo, leo tukiwa katika ile sura ya 21,
Tukisoma..
Mlango 21:1-8
1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. 2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. 3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. 4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. 5 Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli. 6 Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure. 7 Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu. 8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.
1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
5 Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.
6 Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure.
7 Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.
Sura hii inaelezea juu ya MBINGU MPYA NA NCHI MPYA, ikiwa na maana kuwa hapo mwanzo kulikuwa na mbingu ya zamani na nchi ya zamani, na hizi si nyingine zaidi ya hizi zilizopo sasa, kama mtume Petro alivyosema katika 2 Petro 3:5-6″…
5 Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu; 6 kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia. 7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu. 8 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja. 9 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba. 10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea. 11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, 12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? 13 Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia MBINGU MPYA NA NCHI MPYA, ambayo haki yakaa ndani yake. 14 Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake. “
5 Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu;
6 kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia.
7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.
8 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.
9 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.
10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.
11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,
12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?
13 Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia MBINGU MPYA NA NCHI MPYA, ambayo haki yakaa ndani yake.
14 Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake. “
Kwahiyo kwa maneno hayo tunaona dunia ya wakati ule wa Nuhu iliangamizwa kwa maji, vivyo hivyo na hii dunia tuliyopo sasa itaangamizwa kwa moto, kisha ndio ije mbingu mpya na nchi mpya ambaye HAKI yakaa ndani yake. Kumbuka DUNIA haitakunjwa kunjwa kama karatasi na kutupwa kuzimu kama watu wengine wanavyofikiria, hapana bali itakuwa ni dunia hii hii isipokuwa itarekebishwa na kurejeshwa katika utukufu usioneneka ambao Mungu alishaukusudia kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, Hivyo Dunia hii ndiyo makao ya mwanadamu ya milele, Mbinguni tutakaa kwa kitambo tu, kisha tutarudi kutawala na Kristo hapa duniani milele.
Mbingu mpya na nchi mpya itakuja mara baada ya ule utawala wa miaka 1000 kuisha, vilio, misiba, mauti, uchungu, biblia inasema havitakuwepo tena, kwasababu shetani atakuwa ameshatupwa katika lile ziwa la moto pamoja na waovu wote, huko ng’ambo kutakuwa na mambo mapya kabisa ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia, Vitu kama Bahari havitakuwepo tena, Mambo mazuri yasiyoneneka yatakayokuwepo huko, itapelekea hata zile taabu za kwanza zisiingie akilini. Ndugu sio sehemu ya kukosa, uchungu hautakuwa kwasababu utaangamizwa milele, uchungu utakuja pale utakapogundua unayakosa mambo matamu ya Mungu ya umilele.
Lakini tukisoma mstari wa 2, tunaona jambo jingine...” Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.”
.. Mstari huu unafunua kuwa huu mji mtakatifu si mwingine zaidi ya BIBI-ARUSI, na ndio maana ukisoma mstari wa 9-10 tunaona jambo hilo likiendelea kwa urefu,”
“9 Akaja mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na vile vitasa saba vilivyojaa yale mapigo saba ya mwisho, naye akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule BIBI-ARUSI MKE WA MWANA-KONDOO, 10 Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule MJI MTAKATIFU, YERUSALEMU, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu;”
“9 Akaja mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na vile vitasa saba vilivyojaa yale mapigo saba ya mwisho, naye akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule BIBI-ARUSI MKE WA MWANA-KONDOO,
10 Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule MJI MTAKATIFU, YERUSALEMU, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu;”
..Unaona hapo Yohana alionyeshwa bibi-arusi mke wa mwana-kondoo mfano wa MJI.
Kwahiyo hii YERUSALEMU MPYA inayozungumziwa hapo ni BIBI-ARUSI wa Kristo na sio mji tu kama mji mfano wa Ninawi au Nazareti. Pengine itakuwepo miji mikubwa na mizuri huko, lakini sio huo unaozungumziwa hapo…huo ni Bibi arusi wa Kristo.
Kumbuka mji huu Mungu amekuwa akiuundaa tangu vizazi na vizazi, na Mungu hakai katika maskani yenye muundo wa mfano wa kibinadamu, bali maskani ya Mungu ni KANISA lake TAKATIFU, kama tunavyosoma katika waefeso 2:19-22″
19 Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. 20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni JIWE KUU LA PEMBENI. 21 Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe HEKALU TAKATIFU katika Bwana. 22 Katika yeye ninyi nanyi MNAJENGWA PAMOJA KUWA MASKANI YA MUNGU KATIKA ROHO. “
19 Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu.
20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni JIWE KUU LA PEMBENI.
21 Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe HEKALU TAKATIFU katika Bwana.
22 Katika yeye ninyi nanyi MNAJENGWA PAMOJA KUWA MASKANI YA MUNGU KATIKA ROHO. “
Kwahiyo sisi kwa pamoja, (wakristo) tunajenga mwili mmoja maskani ya Mungu ambayo yeye mwenyewe anakaa ndani yake, na ndio mji ambao Ibrahimu aliuona tokea mbali akasema..Waebrania 11:8 Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako. Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. Maana alikuwa akiutazamia MJI WENYE MISINGI, AMBAO MWENYE KUUBUNI NA KUUJENGA NI MUNGU.”. Hivyo upo mji wenye misingi ambao Mungu anaundaa.
Na pia tunaona Mtume Paulo kwenye wagalatia 4, akifananisha wakristo kama watoto wa ile Yerusalemu ya mbinguni iliyofananishwa na Sara,
Wagalatia 4:25-31 25 Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto. 26 Bali YERUSALEMU WA JUU NI MWUNGWANA, naye ndiye mama yetu sisi. 27 Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo aliye na mume. 28 Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi. 29 Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo na sasa. 30 Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana. 31 Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi, BALI TU WATOTO WA HUYO ALIYE MWUNGWANA. “ .
Wagalatia 4:25-31
25 Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto.
26 Bali YERUSALEMU WA JUU NI MWUNGWANA, naye ndiye mama yetu sisi.
27 Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo aliye na mume.
28 Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi.
29 Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo na sasa.
30 Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana.
31 Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi, BALI TU WATOTO WA HUYO ALIYE MWUNGWANA. “ .
Mtume Paulo pia alionyeshwa hilo kwamba watakatifu ni watoto wa ahadi wa ule mji utokao juu(Yerusalemu mpya.)
Hivyo kwa mistari hiyo mpaka hapo tunaweza kupata picha kuwa MJI MTAKATIFU YERUSALEMU MPYA ambao Mungu alikuwa akiiunda kwa muda mrefu sio makasri ya kifahari na barabara nzuri zenye kupendeza bali hayo yote ni picha inayoelezea uzuri wa wateule wake bibi-arusi safi asiye na mawaa aliyemnunua kwa thamani ya damu yake mwenyewe.
Sasa tukiendelea na mistari inayofuata katika ile sura ya 21 tunasoma..
Mlango 21:9-14
9 Akaja mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na vile vitasa saba vilivyojaa yale mapigo saba ya mwisho, naye akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo. 10 Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu; 11 wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi, safi kama bilauri; 12 ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango kumi na miwili, na katika ile milango malaika kumi na wawili; na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila kumi na mbili za Waisraeli. 13 Upande wa mashariki milango mitatu; na upande wa kaskazini milango mitatu; na upande wa kusini milango mitatu; na upande wa magharibi milango mitatu. 14 Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi majina kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo.
9 Akaja mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na vile vitasa saba vilivyojaa yale mapigo saba ya mwisho, naye akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo.
10 Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu;
11 wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi, safi kama bilauri;
12 ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango kumi na miwili, na katika ile milango malaika kumi na wawili; na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila kumi na mbili za Waisraeli.
13 Upande wa mashariki milango mitatu; na upande wa kaskazini milango mitatu; na upande wa kusini milango mitatu; na upande wa magharibi milango mitatu.
14 Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi majina kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo.
Kama tunavyosoma hapo juu mji huu unaonekana wenye misingi 12, na wenye majina 12 ambao ni mitume 12 wa Bwana Yesu Kristo, kumbuka kama tulivyotangulia kusoma kwenye Waefeso 2:20 inasema..”Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni”. Hivyo hawa waliojengwa juu ya huu msingi wa mitume na manabii ni sisi watu wa mataifa, lakini pia kuna wayahudi ambao ni wazao wa ahadi ambao pia walikuwa wakiutazamia mji huu, vivyo hivyo nao walijengwa juu ya wale wana 12 wa Yakobo, ambao kwa ujumla wanatengeneza taifa la Israeli, Hivyo wote kwa pamoja (yaani wakristo na wayahudi ) wataunda ile YERUSALEMU MPYA ya mbinguni. Na ndio maana ule mji hapo unaonekana ukiwa na msingi 12, na milango 12 ambao ni mitume 12 na wana 12 wa Yakobo.
Tukiendelea….
MLANGO 21:15-17
15 Na yeye aliyesema nami alikuwa na mwanzi wa dhahabu, apate kuupima huo mji, na milango yake, na ukuta wake. 16 Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa. 17 Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia na arobaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, maana yake, cha malaika”.
15 Na yeye aliyesema nami alikuwa na mwanzi wa dhahabu, apate kuupima huo mji, na milango yake, na ukuta wake.
16 Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa.
17 Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia na arobaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, maana yake, cha malaika”.
Tunaona picha nyingine hapa huu mji unaonekana ukipimwa, na vipimo vyake vinaonekana kuwa ni sawasawa, havijazidiana,wala kupungukiana kuashiria kwamba uko sawa umejengwa katika utashi wa hali ya juu hivyo ni wa kudumu milele, lakini kama ungepimwa na kuonekana umepunguka, HAKIKA usingedumu milele, ungeanguka tu kama BABELI Mji ule mkuu ulivyopimwa na kuonekana umepunguka, ukaanguka. ukisoma Danieli 5:24-28″ Ndivyo Babeli ilivyoanguka kwasababu vipimo vyake vilionekana vimepunguka, lakini mji huu mtakatifu ambao Mungu ameubuni na kuujenga kwa muda mrefu VIPIMO VYAKE VIPO SAWASAWA, HALELUYA.!!!. na ndio tunafahamu kwanini biblia inasema huko hakitaingia KINYONGE.
Kwasababu mji huo(bibi-arusi) ni mkamilifu.
Tukimalizia kusoma..
MLANGO 21:18-27
18 Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya yaspi, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi. 19 Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi; 20 wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto. 21 Na ile milango kumi na miwili ni lulu kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu. 22 Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo, ndio hekalu lake. 23 Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo. 24 Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake. 25 Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku. 26 Nao wataleta utukufu na heshima ya mataifa ndani yake. 27 Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.
18 Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya yaspi, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi.
19 Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi;
20 wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto.
21 Na ile milango kumi na miwili ni lulu kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu.
22 Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo, ndio hekalu lake.
23 Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo.
24 Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake.
25 Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku.
26 Nao wataleta utukufu na heshima ya mataifa ndani yake.
27 Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.
Na kama inavyoonekana mji huo hauhitaji jua wala mwezi kuangaza, bali UTUKUFU wa Mungu huutia nuru ikiwa na maana kuwa hili kundi linalounda BIBI-ARUSI wa Kristo litapelekwa katika kiwango kingine kikubwa cha UTUKUFU, Kumbuka duniani wakati huo watakuwepo watu wengine wa kawaida, mbali na bibi-arusi, watu hawa watakuwa wametoka katika kumshinda shetani katika ule utawala wa miaka 1000, na baadhi ya waliohukumiwa katika hukumu ya kiti cheupe ambao majina yao yalionekana katika kile KITABU CHA UZIMA. kundi hili ni mbali na BIBI-ARUSI, hawa ndio watakaotawaliwa na kuleta heshima na utukufu kwa Mungu kupitia BIBI-ARUSI wake(Ambaye ndiye YERUSALEMU MPYA).
Kwahiyo bibi-arusi pekee ndiye atakayezichukua siri za Mungu na kuwafundisha mataifa pamoja na hayo utukufu wa miili yao itakuwa ni tofuauti sana na wale wengine, hawa watakuwa na uwezo na ujuzi mwingine wa kipekee kutoka kwa BWANA.
Hivyo ndugu kundi linalounda bibi-arusi wa Kristo ni dogo sana, ni wale tu wanawali werevu waliokwisha kuweka taa zao tayari pamoja na mafuta ya ziada kwenda kumlaki BWANA wao, Huu ni wakati wa kuyaangalia tena maisha yako na kujiweka sawa, Bwana yupo mlangoni kuja na mwanawali mwerevu tu, ndiye atakayemlaki BWANA, na baada ya hapo mlango utafungwa, (Mathayo 25). Biblia inasema Luka 13:23″ Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia,
24 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze. 25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako; “
24 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako; “
JE! HAPA BWANA ALIMAANISHA NI MLANGO UPI TUJITAHIDI KUUINGIA?
Jibu: ni kuingia katika milango ya MJI WA YERUSALEMU MPYA ambaye ni bibi-arusi safi. kwasababu itafika wakati nafasi ya kuwa bibi-arusi haitakuwepo tena.. Ufunuo 22:14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na KUINGIA MJINI KWA MILANGO YAKE. Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya. “
Kama tulivyosoma hapo juu biblia inatuambia:
7 Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu. Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
Hivyo maombi yangu sisi sote tufanye bidii tuwe mojawapo wa bibi-arusi wa Kristo.
AMEN!
Mungu akubariki.
Mada Zinazoendana.
MJI WENYE MISINGI.
NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.
HATARI YA KUHUBIRI INJILI TOFAUTI NA ILIYOANDIKWA KWENYE BIBLIA.
NILIMWONA SHETANI, AKIANGUKA KUTOKA MBINGUNI.
JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.
Karibu tujifunze biblia na huu ni mwendelezo wa kitabu cha Ufunuo leo tukiwa katika ule mlango wa 19,
Tunasoma..
1 Baada ya hayo nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, sauti kubwa mbinguni, ikisema, Haleluya; wokovu na utukufu na nguvu zina BWANA MUNGU wetu. 2 kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na za haki; maana AMEMHUKUMU YULE KAHABA MKUU aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake, na kuipatiliza damu ya watumwa wake mkononi mwake. 3 Wakasema mara ya pili, Haleluya. Na moshi wake hupaa juu hata milele na milele. 4 Na wale wazee ishirini na wanne, na wale wenye uhai wanne, wakasujudu na kumwabudu Mungu, aketiye katika kile kiti cha enzi, wakisema, Amina, Haleluya. 5 Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuu. “
2 kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na za haki; maana AMEMHUKUMU YULE KAHABA MKUU aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake, na kuipatiliza damu ya watumwa wake mkononi mwake.
3 Wakasema mara ya pili, Haleluya. Na moshi wake hupaa juu hata milele na milele.
4 Na wale wazee ishirini na wanne, na wale wenye uhai wanne, wakasujudu na kumwabudu Mungu, aketiye katika kile kiti cha enzi, wakisema, Amina, Haleluya.
5 Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuu. “
Katika mistari hii ya mwanzo tunaona mbingu ikishangalia kuanguka kwa yule mwanamke kahaba ambaye aliyewakosesha watu wote na kuiharibu nchi kwa uasherati wake, kama tulivyoona katika sura iliyotangulia ya 18. Na kahaba huyu si mwingine zaidi ya kanisa Katoliki
na ni kwa jinsi gani alihukumiwa? Tunasoma Mungu alitumia zile pembe 10 (Ufunuo 17:16) ambayo ni mataifa 10 yatakayounda umoja wa ulaya kwa wakati huo, ndio yatakayomkasirikia yule mwanamke kahaba na kumtekeza kabisa kwa moto,kwa maelezo marefu juu ya hukumu ya yule kahaba fautilia link hii >>> UFUNUO 18
Na ndio sababu tunaona mbingu zikishangalia, zikisema hukumu za Mungu ni za haki kwa kuwa kahaba huyu alimwaga damu za watakatifu wengi wa Mungu na ndio maana hukumu yake ikaja na moshi wake hupaa juu hata milele na milele kuashiria kuwa pigo lake haliponyeki ni la kifo cha milele wala hata kaa anyanyuke tena kuwakosesha watu wanaokaa juu ya nchi kwa uasherati wake. Mstari wa 5 unasema..
5 Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuu.
KARAMU YA HARUSI YA MWANA-KONDOO.
Tukiendelea kusoma mstari wa 6-10.
6 Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Haleluya; kwa kuwa Bwana Mungu wetu, Mwenyezi, amemiliki. 7 Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari. 8 Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu. 9 Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu. 10 Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.
6 Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Haleluya; kwa kuwa Bwana Mungu wetu, Mwenyezi, amemiliki.
7 Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.
8 Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.
9 Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.
10 Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.
Katika vipengele hivi, Arusi ya mwanakondoo inazungumziwa na mkewe amekwisha jiweka tayari, kumbuka kuna tofauti kati ya Arusi na Karamu,. Siku zote ndoa ikishafungwa (Arusi), kinachofauta ni KARAMU, Kwahiyo Karamu ni sherehe ya kuifurahia “ndoa/arusi mpya”. Vivyo hivyo na kwa YESU KRISTO kama Bwana Arusi yeye naye ana bibi-arusi wake ambaye ndio KANISA lake TAKATIFU bikira safi asiye na mawaa.
Kwahiyo katika ukristo NDOA hii inaendelea sasa hivi kufungwa duniani na hii ilishaanza tangu kipindi BWANA YESU alichopaa kwenda mbinguni mpaka leo, katika vile vipindi vyote 7 vya makanisa , na amekuwa akikusanya bibi-arusi wake kwa kila kipindi na kila nyakati na hadi sasa anaendelea kufanya hivyo,takribani miaka 2000 sasa. Na kuoana huko ni kati ya MTU na NENO LA MUNGU, na kama tunavyofahamu NENO ni YESU KRISTO MWENYEWE, hivyo wale walishikao na kuliishi NENO ndio waliooana na KRISTO
Na sio mkristo vuguvugu anayesema mimi nimeokoka halafu haliishi na halipokei NENO LA MUNGU, kwa mfano ukimwambia mtu biblia inasema hivi yeye anasema dhehebu langu halinifundishi hivyo, ukimuuliza ni kwanini ubatizo wa watoto wachanga haulingani na NENO la Mungu atakwambia dini yetu haifundishi hivyo. Mtu anajiita mkristo lakini anaupenda ulimwengu kuliko kumpenda Mungu, ukimuuliza kwanini unakunywa pombe, atasema dini inaruhusu kunywa pombe, acha kuhukumu, hapo mtu huyo anakuwa ameoana na ulimwengu badala ya Kristo (NENO), Hivyo anafanya uasherati mkuu wa kiroho.
Kwahiyo fahamu ndoa inaendelea sasa hivi katika roho, usipooana na KRISTO (NENO LA MUNGU), utaoana na shetani kwa mafundisho yake ya uongo yanayolipinga NENO LA MUNGU. Kwahiyo ni vizuri sasa hivi ukajitambua upo upande upi?.
Mtume Paulo alisema katika 2Wakorintho 11:2-4″ Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi”.
Hivyo ni jukumu kwa kila nayejiita mkristo sio tu kuwa bikira bali kuwa BIKIRA SAFI!!
Tukisoma katika mathayo 25 tunaona mfano ya wale wanawali li kumi (10), watano werevu na watano wakiwa wapumbavu. Kumbuka wote 10 walikuwa MABIKIRA wakimngoja Bwana wao, lakini kilichowatofautisha ni kwamba wale wapumbavu hawakuwa na mafuta ya ziada katika taa zao ambayo ni “ufunuo wa NENO LA MUNGU katika ROHO MTAKATIFU”,. jambo hilo tu liliwafanya wasiingie KARAMUNI japo wote walikuwa ni mabikira, kwahiyo kujiita mkristo tu haitoshi ni lazima pia uwe na ufunuo wa NENO LA MUNGU, na ndoa inafanyika hapa duniani lakini KARAMU itafanyika mbinguni pale bibi-arusi safi atakapokwenda kwenye unyakuo.
Kama tunavyosoma wale 5 werevu waliingia karamuni bali wale wapumbavu walifungiwa nje vivyo hivyo katika hichi kipindi cha mwisho kutakuwa na makundi mawili ya wakristo, werevu na wapumbavu, werevu ni wale wanaolishika na kuliishi NENO LA MUNGU bila kujali kitu kingine chochote, hao wataenda na Bwana na kuingia katika KARAMU YA MWANAKONDOO, Lakini wale wapumbavu wasiojiweka tayari, kwa kukataa uongozo wa Roho Mtakatifu katika NENO lake, hawa watatupwa giza la nje! kwenye dhiki kuu, wakati wenzao wanafurahi na Bwana katika utukufu mbinguni na kupewa thawabu zao za milele na ndio maana mstari wa 8 tunasoma bibi-arusi ” ..amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.”
Katika hii karamu kutakuwa na mambo ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia mambo ambayo Kristo kawaandalia hao wateule wake (yaani bibi-arusi wake safi), hawa watakuwa na miili ya utukufu sana na ndio baadaye watashuka na BWANA kuja kutawala ulimwengu kwa muda wa miaka 1000 wakiwa kama makuhani na wafalme wa dunia nzima, uzao mteule, watu wa milki ya Mungu, na BWANA YESU KRISTO, akiwa kama BWANA WA MABWANA, na MAFALME WA WAFALME. haleluya!!. Kosa kila kitu ndugu lakini usiikose hiyo karamu, uchungu siku hiyo hautakuwepo sana katika mateso ya dhiki kuu, hapana bali uchungu utakuja sana pale utakapogundua kuwa umekosa thawabu za milele, na usidanganyike eti huko tunapokwenda wote tutakuwa sawa tunafanana! hayo mawazo futa, kule kutakuwa na madaraja tofauti tofauti, wapo watakaokuwa wakuu sana, na wakawaida sana na ni itakuwa hivyo milele, kwanini leo hii unang’ang’ana na vitu vinavyoharibika usijiwekee hazina mbinguni?.
Mstari wa 9 unasema “.. Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.”
VITA YA HAR-MAGEDONI
11 Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. 12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe. 13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu. 14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi. 15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi. 16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA. 17 Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua; akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njoni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu; 18 mpate kula nyama ya wafalme, na nyama ya majemadari, na nyama ya watu hodari, na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana kwa watumwa, wadogo kwa wakubwa. 19 Kisha nikamwona huyo mnyama, na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, tena na majeshi yake. 20 Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti; 21 na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.
12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.
13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.
14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.
15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.
16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.
17 Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua; akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njoni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu;
18 mpate kula nyama ya wafalme, na nyama ya majemadari, na nyama ya watu hodari, na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana kwa watumwa, wadogo kwa wakubwa.
19 Kisha nikamwona huyo mnyama, na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, tena na majeshi yake.
20 Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;
21 na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.
Katika aya hizi tunaona Yohana akionyeshwa mbingu zikifunguka na kuona farasi mweupe, na yeye aliyempanda, anaitwa Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. Huyu sio mwingine zaidi ya BWANA YESU KRISTO na hapo anaonekana akiwa na vilemba vingi juu ya kichwa chake ikiashiria kuwa anamiliki juu ya wafalme wengi,
Na anaonekana pia akishuka pamoja na jeshi la mbinguni, sasa kumbuka hili jeshi sio malaika bali ni wale watakatifu (bikira safi) waliokuwa wamekwishanyakuliwa mbinguni sasa baada karamu kuisha watarudi duniani wakiwa kama MIALE ya moto kama BWANA alivyo, jambo hili tunaona Henoko miaka mingi iliyopita alionyeshwa Yuda 1:14 Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu,
15 ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake. “
Kwahiyo Bwana atakapokuja wafalme wote wa dunia watakuwa wamekusanyika tayari kupigana naye, mahali panapoitwa Harmagedoni huko Israeli (Ufunuo 16:16) pale zile pembe 10 za yule mnyama pamoja na wafalme kutoka mawio ya jua ambazo ni nchi za mashariki ya mbali kama Japan, China, Korea, Singapore n.k.
Ufunuo 16:12-16″ Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua. 13 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. 14 Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi. 15 (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.) 16 Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni. “
Ufunuo 16:12-16″ Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.
13 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo.
14 Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.
15 (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)
16 Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni. “
lakini vita hii itadumu ndani ya muda mfupi sana, kwamaana KRISTO hapigani kwa kutumia silaha za kibinadamu, bali siku zote yeye anatumia NENO, kwasababu yeye mwenyewe ni NENO, na ndio maana tukisoma hapo juu jina lake anaitwa NENO LA MUNGU, kwahiyo kwa kuzungumza tu pale megido kutakuwa ni bahari ya damu, mabilioni ya watu watakufa, na kama tunavyosoma katika mstari wa “17 Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua; akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njoni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu;
Ndege wengi wataalikwa kuja kula nyama za watu wanaojiona majemedari na wafalme wa nchi, kwahiyo unaweza ukatengeneza picha yatakuwa ni mauaji ya namna gani yeye ndiye atakayekanyaga lile shinikizo la ghadhabu ya Mungu, na ukisoma ufunuo 14:20, utaona shinikizo lile likakanyagwa nje ya mji, DAMU ikatoka katika shinikizo mpaka kwenye hatamu za farasi, kwa mwendo wa maili 200, “hii ni picha kuonyesha kwamba damu nyingi sana itamwagika kiasi cha kwamba ndege wengi wa angani watakusanyika kula nyama za mizoga ya watu.Hivyo vita hii ndio itakayohitimisha utawala mbovu wa dunia hii na kuleta utawala mpya wa BWANA YESU KRISTO duniani.
Na katika ule mstari wa mwisho tunasoma
20 “Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;
21 na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.”
Kwahiyo zile roho mbili kati ya zile tatu chafu kama vyura, zilishikwa na kutupwa katika lile ziwa la moto, kumbuka hapo anaposema mnyama na nabii wa uongo anamaanisha zile roho zilizokuwa zinawaendesha huyu mnyama na nabii wa uongo, lakini ile roho ya tatu ambayo ni roho ya shetani itafungwa kwa muda wa miaka 1000, kisha itafunguliwa tena kwa muda mfupi habari hii tutaisoma zaidi katika sura inayofuata ya 20,
Hivyo ndugu fahamu kuwa kanisa tunaloishi leo ni kanisa la mwisho la 7 linaloitwa LAODIKIA, na mjumbe wake ameshapita, muda wowote BWANA anakuja kumchukua bibi-arusi wake safi tu, aliyekwisha kujiweka tayari kwa kupokea Roho Mtakatifu na kuishi kwa NENO tu, je! umejiweka tayari kwenda naye? au utakuwa mwanamwali mpumbavu (yaani mkristo mpumbavu) vuguvugu?. Maombi yangu Bwana akufanye kuwa BIKIRA SAFI. ili sote siku ile kwa neema za BWANA TUKUTANE KATIKA ILE KARAMU YA MWANA KONDOO.
MUNGU AKUBARIKI.
Kwa mwendelezo >> UFUNUO: Mlango wa 20
KARAMU YA MWANA-KONDOO.
NDOA NA HARUSI TAKATIFU.
MAANDALIZI YA UJENZI WA HEKALU LA TATU YAPO TAYARI.
KUWA MAKINI NA MITANDAO, NI SHIMO REFU.