SWALI: Sheria ya uhuru ni ipi inayozungumziwa na mtume Yakobo kulingana na maandiko?
Yakobo 2:11 Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria. 12 Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru.
Neno hili pia utaliona likitajwa na mtume Yakobo katika vifungu vingine vya juu.
Yakobo 1:25 Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.
Katika biblia zipo sheria kuu mbili
Sheria ya dhambi na mauti ndio ile ya torati, ambayo kazi yake kubwa ni kufichua uovu, kushtaki makosa, lakini haimfanyi mtu kuwa huru, kwa mfano sheria inasema usizini, mtu atakataa kuzini, sio kwasababu hapendi uzinzi, lakini kwasababu sheria imesema tu hivyo, anaogopa adhabu atakapotenda hiyo dhambi atauawa.
Lakini sheria ya Roho wa uzima, ni sheria ya Mungu, isipokuwa hii mtu anavuviwa na Roho Mtakatifu, nguvu ya kuisha sawasawa na matwaka ya Mungu, bila shuruti Fulani, ni ya uhuru. Mfano labda sheria inasema usiue, mtu haui sio kwasababu sheria imesema, lakini kwasababu moyoni mwake hiyo nia, tamaa, au kiu ya kuua haipo, hivyo hata kama sheria isingesema hilo jambo lisingekubalika ndani yake, Hivyo mtu kama huyu tunasema ni huru na sheria, hayupo ki-sheria, sheria haimtawali ijapokuwa sheria yenyewe ipo.
Mtu ukishaokoka, anakutana na sheria mpya ya Mungu, ambayo hiyo ni lazima ifuatwe na ishikwe, lakini inakuwa ya uhuru, sio tena ya kifungo, kwasababu Roho Mtakatifu anamsaidia huyo mtu kuuishi..
Ndio hiyo inayoitwa sheria ya uhuru, kwenye kitabu cha Yakobo.
Maana yake ni nini? Sisi kama waamini, Mungu anatarajia tuonyeshe matunda ya Imani yetu katika upendo, huruma, na matendo mema, kwasababu tunaye Roho.
Hivyo inapotokea, hayo hayaonekani, sheria itatuwajibisha, kutuhukumu, au vinginevyo hatukipokea sheria hiyo ya uhuru.. Ni sawa, na mtu aende kuua watu ovyo bila sababu yoyote,
Mtu huyu atahukumiwa, sawa tu na yule ambaye amesukumwa na sababu fulani, labda kisasi, hasira, wivu, chuki n.k.,
Hivyo sisi waamini, tulipokuwa huru na dhambi, hatupaswi kufikiri kuwa ndio tuna uhalali wa Kutenda dhambi. Kinyume chake, tujue kuwa ipo sheria yetu ya uhuru, itakayotuhukumu, kama tu vile wale wengine walivyohukumiwa kwa sheria ya dhambi na mauti (torati).
Ndicho alichokisema mtume Yakobo..
Kwa hitimisho ni kuwa sheria ya uhuru, ni sheria tunayoitimiza kwa nguvu za Roho Mtakatifu. Ambayo hiyo pia itatuhukumu. Hivyo wewe kama mwamini, hakikisha wokovu wako unathibitika kwa kazi zake njema, chini ya upendo
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
Kama Bwana anawajua walio wake tangu asili kwanini tunahubiri injili? (Warumi 8:29)
Fahamu maana ya Warumi 7:25 je tunatumikia sheria ya dhambi?
Silaha za Nuru ni zipi? (Warumi 13:12)
Print this post
SWALI:Je? ni sahihi kwa watu wa MUNGU kutumia majina ya wanyama kuwaita wengine.mfano “We kenge njoo hapa”, kama YESU alivyo tumia mbweha katika
luka 13:32.
JIBU: Katika biblia tunaona watu wakiitwa kwa majina mbalimbali ya wanyama mfano mbwa mwitu (Mathayo 7:15), kondoo(Yohana10:27), nyoka(Mathayo 13:34). Lakini pia mbweha, Njiwa, nguruwe, Simba, mbuzi.
Sasa ni vema kufahamu makusudio ya watu/jamii kuitwa hivyo yalikuwa ni nini, hayakuwa kwa lengo la kutukana, au kukejeli, au kudharau..
Hapana Bali kwa lengo la kuonyesha tabia ya mtu, jinsi ilivyo hilo tu.
Kwamfano Yesu alipomuitwa Herode Mbweha, hakuwa na kusudi la kumtukana, au kumdharau, bali alikuwa Anaeleza tabia zake zilizo mfano wa mbweha, ambaye anatabia ya kuvizia na kurarua wanyama wadogo na kuwaua. Maana hivyo ndivyo Herode alivyokuwa, jambo lililoonekana Hata kwa baba zake Kipindi Yesu anazaliwa walimwinda ili wamuue.
Sasa Ikiwa mtu atajulikana kwa namna kama hiyo, kibiblia sio tusi.
Lakini kinyume chake watu hutumia Majina ya wanyama kuwatukana Wengine, au kuwaabisha, au kuonyesha dharau kinyume chao, chuki au hasira, hayo biblia imekataza…na ni dhambi
Kusema “wewe kenge njoo hapa”..Moja kwa moja kauli hiyo inaonyesha chanzo chake ni hasira, dharau au chuki.
Waefeso 4:29
[29]Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.
Wakolosai 3:8
[8]Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu.
Mathayo 5:22
[22]Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.
Hivyo chunga kinywa chako. Kila Neno ulisemalo pima makusudi yaliyo nyuma yake.
VILIO VINAVYOUFIKIA MOYO WANGU.
JAWA SANA MOTO ULAO
USIWAOGOPE WAZAMZUMI
SWALI: Naomba kufahamu tunaposema Bwana Yesu asifiwe tunamaanisha nini? Na ni nani anayepaswa kuisema hiyo salamu, na kwanini wengine wanasema ‘shalom’ badala yake?
JIBU
‘Bwana Yesu asifiwe’ ni kauli inayotangaza kustahili kwa Yesu sifa kwa ile kazi njema aliyoifanya Hapa duniani.
Yesu ndiye Mtu pekee ambaye alikubali kuingia gharama ya kuacha enzi na mamlaka Mbinguni, na kuja kuishi hapa duniani kwa kusudi moja tu la kutukomboa sisi,katika dhambi zetu, akateswa na kujaribiwa sana, akafa baadaye akafufuka na hata sasa yupo hai ameketi kama mpatanishi wa sisi na Mungu,..
Kiasi kwamba kwa kupitia Yeye tunapokea msamaha wa dhambi, tunaponywa magojwa, tunamseta shetani, tunabarikiwa, tunawasiliana na Mungu moja kwa moja bila vikwazo vyovyote kwa damu yake.
Mtu Kama huyu ni lazima astahili kusifiwa..ndio maana inakuwa ni salamu ya Wakati wote BWANA YESU ASIFIWE..
Kwasababu ya nuru tuliyo ipata kwa kazi yake njema ya ukombozi.
Je ni nani anayepaswa kuisema?
Hakuna mtu anayekatazwa kuisema, lakini mtu asipojua kwanini Yesu asifiwe basi anaisema kwa unafki, Na Mungu hapendi unafiki. Kwamfano mtu ambaye hajaokoka, halafu anasema Bwana Yesu asifiwe, ni sharti ajiulize asifiwe kwa lipi wakati hakuna chochote kilichofanya na yeye katika maisha yake..
Ni sawa na mtu aliyeokoka aseme shetani asifiwe.. atasifiwa kwa jambo gani hapo wakati hakuna ushirika wowote alio nao na shetani. Lakini mganga wa kienyeji Akisema hivyo hiyo ni kweli kwasababu kuna faida amezipata Kwa shetani.
Salamu hii pia, au kauli hii, ni sahihi kutumika katika matamshi ya kiibada..mfano kwenye mahubiri, mafundisho, nyimbo, maombezi N.k. kwasababu katika Maeneo haya kazi za Yesu hudhihirishwa.
Lakini shalom Ni neno la kiyahudi linalomaanisha ‘Amani’. Ni Neno ambalo mtu yeyote anaweza kulitumia awe ameokoka au hajaokoka kwasababu ni Neno la kilugha zaidi kuliko kiimani. Ni sawasawa na sisi tunavyosema, ‘habari yako’. Mtu yeyote anaweza kutumia hilo neno. Lakini Bwana Yesu asifiwe ni Neno la kiimani ambalo anayestahili kulitamka ni mtu aliyemwamini Yesu tu.
WhatsApp
Swali: Tunasoma katika Yohana 1:29 kuwa Yohana anamshuhudia Bwana YESU kuwa yeye “mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu”.. Lakini tukirudi katika Mathayo11:3 tunasoma tofauti, Yohana anawatuma wanafunzi wake wamwulize kama yeye ndiye Kristo au wamtazamie mwingine, sasa swali ni je Yohana alimtilia shaka Bwana Yesu au hakumwamini tangu mwazo?.
Jibu: Ni ngumu imani ya Yohana kutikisika kirahisi lakini hebu kwanza turejee kitabu cha Mathayo…
Mathayo 11:2 “Naye Yohana aliposikia huko gerezani matendo yake Kristo, alituma wanafunzi wake, kumwuliza, 3 Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine? 4 Yesu akajibu akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana mnayoyasikia na kuyaona; 5 vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema. 6 Naye heri awaye yote asiyechukizwa nami”.
Ni kweli Masihi ajaye alikuwa ametabiriwa kuwa atakuja na nguvu kuwaokoa Israeli na utumwa wa maadui zao, na Israeli wote walitazamia kabisa kuwa Kristo atakayekuja atawafungua na utumwa mgumu wa warumi.. lakini haikuwa hivyo kwa YESU KRISTO, kwani alianza kushughulika na dhambi za wana wa Israeli, zaidi ya Taifa.. Hiyo ikawafanya baadhi ya watu kumtilia mashaka YESU kama yeye ndiye KRISTO (Yaani Masihi).
Na bila shaka Yohana hakuwa na wasiwasi wa YESU kuwa Masihi, kwani tayari alishaonyeshwa wakati anambatiza YESU kuwa Yule atakayembatiza na ishara ya hua ikionekana juu yake basi huyo ndiye Masihi, na ni wazi kabisa Yohana alijua kuwa wakati wake aliokuwa anaishi duniani, Kristo naye alikuwa anaishi, ila hakumjua ni nani mpaka wakati wa ubatizo, Roho kama Hua aliposhuka juu ya Bwana, na mbingu kufunguka. (Mathayo 3:16-17).
Sasa kama ni hivyo ni kitu gani kilichomfanya Yohana Mbatizaji atume wanafunzi wake kwa YESU na kumwuliza swali ambalo tayari alikuwa na jibu lake?.
Jibu ni kwamba baadhi ya watu ikiwemo wanafunzi wake Yohana bado hawakuwa na uhakika wa moja kwa moja kama YESU ndiye KRISTO, kwahivyo kwa kusikia Neno linalotoka moja kwa moja kinywani mwa YESU, ingeweza kuwafanya waamini zaidi, hivyo Yohana lengo lake huu ni wanafunzi wakasikie na kujihakikishia wenyewe, kwamaana muda wake wa kuishi ulikuwa umekaribia kuisha na watakayebaki naye ni YESU. Na walipokwenda walipata majibu.
Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba Yohana hakuwa na mashaka na Bwana YESU, bali wanafunzi wake na baadhi ya watu, na hiyo ni kutokana na kwamba Bwana YESU hakuwa anajitangaza hadharani kuwa yeye ni KRISTO.
Yohana 10:24 “Basi Wayahudi walimzunguka, wakamwambia, Hata lini utatuhangaisha nafsi zetu? Kama wewe ndiwe Kristo, utuambie waziwazi”.
Soma pia Luka 22:77..
Je umempokea YESU?.. Una uhakika kwamba YESU akirudi leo utakwenda naye?.. kama bado upo nje ya Imani fahamu kuwa upo hatarini sana, hivyo mkaribie YESU leo usamehewe dhambi zako na upokee ujazo wa Roho Mtakatifu. Shalom.
Yohana aliwatiaje waasi akili za wenye haki? (Luka 1:17)
NI NINI TUNAJIFUNZA KWA YOANA NA MANAENI?
“Hakuna aniulizaye unakwenda wapi”, maana yake nini? (Yohana 16:5).
Nini maana ya “manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana” (Mathayo 11:13)
Je biblia inajichanganya kwa habari za Yohana kuwa Eliya?
Ni vema kufahamu Kanisa ni nini?
Kanisa sio jengo, au mahali, bali ni watu, walioitwa Na Mungu, waliookolewa wanakusanyika pamoja katika nia moja kumwabudu na kumtumikia yeye.
Hivyo watu hawa wanaweza kukusanyika maeneo yaliyo rasmi, lakini pia maeneo yasiyo rasmi kwa shughuli zao za kiibada..maadamu tu wamekidhi vigezo hivyo vya kiroho.
Kanisa la kwanza lilikusanyika Hekaluni (mahali rasmi kwa shughuli za kiibada tu). Lakini pia lilikusanyika majumbani…wakati mwingi pembezoni Mwa mito na kwenye madarasa..
Matendo ya Mitume 2:46
[46]Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe,
Matendo ya Mitume 5:42
[42]Na kila siku, ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema za Yesu kwamba ni Kristo.
Kama tunavyojua majumbani mahali ambapo, pana shughuli nyingi wakimaliza ibada huwenda sherehe zinafanyika hapo, au vikao vya kijamii, lakini hilo halikuwazuia kutimiza makusudi ya Mungu yaliyoyakusudia.
Hivyo yaweza kuwa ni sahihi endapo, hakuna mahali rasmi bado, ibada zinaweza kufanyika kwenye majengo ya shule, kwenye mabwalo, kwenye kumbi,.viwanjani, hata chini ya miti maadamu tu umoja huo upo na nia ni Kristo..hata hivyo yapo makanisa makubwa na yamefanikiwa lakini bado hayana maeneo yao rasmi ya kukutanikia…lakini kanisa Limesimama.
Mambo tu ya kuzingatia, ni nidhani yenu, adabu na utulivu wa mazingira ya kiroho kwa wakati huo,..ikiwa haya yapo hapo Mnapokusanyikia basi Mungu yupo nanyi..wala si dhambi.
Lakini ni busara na vema zaidi kanisa likatafuta eneo rasmi la kukusanyikia litakalokuwa ni kwa shughuli zao tu za kiibada.
Shalom.
Nini maana ya kumwabudu Mungu katika Roho na kweli?
MAISHA YA UVUGUVUGU, YANAMFANYA MUNGU AUMWE.
UNAWAZA NINI SASA, JUU YA UFALME WA MBINGUNI?
1Petro 1:12 Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.
Siku ya kujiliwa ni wakati ambao, Mungu anashuka ulimwenguni, aidha kwa kuokoa au kuhukumu.
Zote mbili ni siku za kujiliwa.
Kwa mfano kwa lengo la kuokoa. Upo wakati ambao neema ya Mungu humjia mtu, au taifa, na hivyo wakati huo mara nyingi uamsho mkubwa huwa unapita, Kwamfano, kipindi cha Kristo, kilikuwa ni kipindi maalumu cha Israeli kujiliwa lakini hawakukubali ..isipokuwa wachache..(Luka 19:41-44)
Lakini kwa lengo la hukumu ni siku ambayo kila mmoja wetu atahukumiwa kulingana na matendo yake.
Hivyo tukirudi kwenye 1 Petro 1:12, inayosema ‘Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa’.
Maana yake, matendo mema ya mwamini, hupelekea watu kuupokea wokovu na kumtukuza Mungu,siku neema yao inapowafikia, kwamfano wapo watu ambapo kwa kukuangalia, kwa kipindi kirefu, siku ya kujiliwa inapowafikia inakuwa ni rahisi kuamini na kumtukuza Mungu, kwasababu walishawahi kuona watu waliokoka walivyo na sifa zao njema, mfano upendo, amani, uadilifu..Lakini ukiwa na mwenendo mbovu, siku yao ya kujiliwa inapowafikia, wakikumbuka mwenendo mbovu waliouna kwako , ni ngumu sana kumtukuza Mungu,
Ndicho ambacho mtume Petro alikuwa anakieleza hata mbeleni kidogo, kuhusiana na Wanandoa, kwa upande wa wanawake, akasema, ikiwa mtu ana mume asiyeamini, anao uwezo wa kumvuta ndani ya Kristo kwa mwenendo wake tu.. (1Petro 3:1).
Kwa ufupi ni kuwa mwenendo wako mwema hulainisha njia ya neema ya Kristo Kutenda kazi vema juu ya mtu.
Mungu akubariki.
Biblia inamaana gani inaposema “Mungu wa neema yote” (1Petro 5:10)
Nini maana ya ombeni kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi wala siku ya sabato?.
MILANGO YA KUZIMU.
JIBU: Tukiangalia mwanzo wa mstari huo, unasema..
Mithali 11:16 Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; Na watu wakali hushika mali siku zote.
Ukitazama tafsiri nyingine maana iliyonyooka zaidi ya mstari huo, unasema “mwanamke wa adabu huheshimwa daima, lakini watu wakali hushika tu mali”.
Yaani unalinganisha, sifa njema, na vitu vingi, akilinganisha mwanamke anayewekeza maisha yake katika tabia nzuri, matokeo yake heshima itakuwa kwake ambayo itadumu daima, lakini mtu mkali anayewekeza katika kujilimbikizia mali isivyo halali, akiwakandamiza wengine, akitumia ukali, akiwanyima mshahara wengine, ni kweli na yeye atapata matokeo yake ambayo ni mali nyingi tu. Lakini hana heshima yoyote nyuma yake. Haachi kitu chenye thamani kitakachoweza kuwa faida kwa wengine, hana la kuigwa, hana la kusifiwa isipokuwa, malalamiko, uchungu na machozi kwa wengine.
Hivyo andiko hilo linalinganisha sifa njema na mali. Ni heri ujijengee sifa njema ambayo hiyo itafuatwa na vizazi hata vya mbeleni, kama vile tuwaonavyo wanawake wacha Mungu kwenye maandiko, mfano wa Ana binti Fanueli, Mariamu, Sara, watu kama akina Ayubu, Danieli, Yusufu, ambao njia zao huigwa hata sasa, kuliko kuwa kama Nabali aliyetajirika lakini mpumbavu, hana chochote cha kuigwa na watu.
Ni heri maskini ahubiriye watu, na kuwaleta kwa Kristo, wanaacha dhambi, na kupokea Roho Mtakatifu, kuliko mtu yule ambaye kutwa nzima anachowaza ni kujiwekezea nafsi yake, kuiba, na kudhulumu, kutumia ukali kupata mali mambo ambayo yataishia hapa hapa tu duniani.
Mithali 22:1 Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi; Na neema kuliko fedha na dhahabu.
Tafsiri ya Mithali 3:27 inayosema ‘Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao’
Maana ya Mithali 29:9 Mwenye hekima akijadiliana na mpumbavu; Akikasirika au akicheka, pia hapana raha.
Maana ya Mithali 26:2 Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake,
SWALI: Tumekuwa tukisikia kuwa mtu akifa, huko aendako anakutana na mateso makali ya jehanamu. Sasa napenda kufahamu je ni roho ndio itakayoteketezwa au na miili pia?
JIBU: Maandiko yanatueleza siku ya mwisho ya hukumu, wafu wote watafufuliwa. (Iwe ni wema au waovu), wote watairudia miili yao ya asili yaliyokuwa nayo duniani.
Yohana 5:28
28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu
Ufunuo 20: 12-13
12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake
Waliokufa katika Kristo (Watakatifu) watavikwa miili mipya ya utukufu, isiyoharibika (1Wakorintho 15:42-54) lakini waovu watakuwa na miili yao ya asili. Ambayo katika hiyo watahukumiwa na kutupwa katika lile ziwa la moto, lililo maalumu kwa mateso ya mtu milele.
Hivyo ni vizuri ifahamike, kuwa kitakachoteketezwa sio roho tu, bali na mwili pia, Bwana Yesu aliliweka hilo wazi katika maneno haya;
Mathayo10:28 Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.
Umeona hapo?.. Awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum. Kuonyesha kuwa mwili nao utashiriki mateso ya milele.
Tukishayajua hayo, tunapaswa tufanyaje?
Je! Umemwamini Bwana Yesu ndugu? Wokovu ni sasa, mgeukie akuponye, uwe salama, hata ukifa uwe na uhakika wa kuurithi uzima wa milele, Itakufaidia nini kuupata ulimwengu mzima, kisha upate hasara ya nafsi yako? Fanya uamuzi wa busara.
Okoka, leo uponywe. Ikiwa upo tayari kufanya hivyo, basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala ya Toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
HERI WAFU WAFAO KATIKA BWANA
MWOMBENI BWANA WA MAVUNO APELEKE WATENDA KAZI.
MAUTI NA KUZIMU ZIKAWATOA WAFU WALIOKUWAMO NDANI YAKE.
SWALI: nini maana ya Yohana 17:20
[20]Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.
Ni akina nani hao ambao wataamini Kwasababu ya Neno lao, Bwana Yesu aliotaka kuwaombea?
JIBU: Sura hiyo ya 17 ni sura iliyoelezea kwa kina dua ambayo Bwana Yesu aliifanya kwa mitume wake kwa Baba.
Ambapo aliwaombea mambo kadha wa kadha ikiwemo walindwe katika umoja wa Roho, walindwe na yule mwovu, watakaswe na ile kweli.. Lakini pia Bwana Yesu hakuishia kuwaombea wao tu, bali na wengine ambao mitume wake watawahubiria injili na kuamini baadaye. Na hao pia maombi yake yalikuwa ni yaleyale kwao.
Maana yake ni kuwa watu wote walioamini kwa injili ya mitume walishiriki dua hiyo ya Kristo, Na hao si wengine zaidi ya wale watakatifu wa kanisa la kwanza, hadi sisi tuliopo sasa, hadi na wale watakaokuja baadaye.. sisi wote ni washirika wa dua ile (Yohana 17), kwasababu tumeamini katika injili moja ya mitume..
Ndio sababu kwanini maandiko yanasema Kristo anatuombea…maana yake ni kuwa sasa anatuombea kwa yule Roho Mtakatifu auguaye ndani yetu, lakini pia analituombea alipokuwa duniani ambapo sala hiyo tunaona matokeo yake hata sasa.
Waebrania 7:25
[25]Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.
Hii ni kututhibitishia Kuwa pale tunapomwamini Kristo upo ulinzi usioelezeka unawekwa juu yetu, kiasi kwamba malango ya adui hayawezi Kushinda..kinachohitajika ni kutii tu.
Warumi 8:34
[34]Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.
Je na wewe ni mshirika wa sala hiyo ya Bwana? Kwa kumpokea Bwana Yesu? Kama ni la! Basi nafasi ni sasa mwamini Yesu upokee uzima wa milele.
Lakini pia Bwana anatufundisha namna sahihi ya kuomba..hatupaswi tu kuyaombea yale matunda tunaoyaona..bali hata na yale yatakayokuja baadaye..wale watakaokoka baadaye kwasababu ya Neno letu.
WOSIA WA BWANA YESU KWA WANAFUNZI WAKE.
MTAIFAHAMU KWELI NAYO HIYO KWELI ITAWAWEKA HURU.
“Akaiona imefagiwa na kupambwa” Maana yake nini (Luka 11:26).
Tofauti na Ibrahimu, Isaka na Yakobo ambao chimbiko lao linaonekana katika mtiririko wake tokea Adamu mpaka Nuru hadi wao wenyewe..
Ayubu yeye ni tofauti, kwani kitabu kinaanza kwa kumweleza yeye, na mahali tu alipokuwa ambapo ni Usi.
Usi ni nchi ambayo ilikuwa nje ya Israeli, maeneo ya aidha Arabia, Syria au Yordani..lakini eneo sahihi kwa uhakika halijulikani hivyo hakuwa na chimbuko lolote la kiyahudi ndani yake.
Maandiko yanamtaja tu kama “Mtu”, wala sio nabii, au kuhani bali mtu aliyekuwa mkamilifu na mwelekezo aliyemcha Mungu na kuepukana na uovu.
Ayubu 1:1
[1]Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.
kwanini Mungu aruhusu, watu kama hawa ambao hawakuwa katika mtiririko wa kifamilia waandikwe kwenye biblia na zaidi hata wawe na sehemu kubwa katika ufalme wa Mungu…
Ni kuonyesha kuwa Mungu hana upendeleo, yeyote yule amchaye yeye hukubaliwa naye..ndicho Petro alichokiona kwa Kornelio akasema..
Matendo ya Mitume 10:34-35 [34]Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo;
[35]bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye.
Mwanamke Ruthu hakuwa myahudi, lakini Bwana alimkubali.
Hata na wewe kitendo cha kutozaliwa familia ya kikristo au kichungaji haimaanishi kuwa wewe huna neema ya kumtumikia Mungu. Hapana..ukionyesha bidii ile ile wanayoonyesha wengine Mungu hukujalizilisha neema Izidiyo haijalishi ukoo wenu wote ni wa kiganga. Kila mmoja wetu ana nafasi sawa mbele za Mungu, haijalishi kama ni myahudi au mwarabu, kama ni mzungu au mwafika wote kwa Mungu wanayo neema sawa kwasababu yeye haangalii chimbuko wala sura ya mtu.
Je unamcha Mungu?