Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu ni wakina nani?

Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu ni wakina nani?

Swali linaendelea… kulingana na huu mstari   (1Wakoritho15:29) inaonekana kuwa wale wanaobatiza watu kwa ajili ya watu waliokufa zamani katika dhambi zao au kuwaombea, wapo sahihi na wanachofanya ni sawa kwasababu hata maandiko yanathibitisha hilo?.. Naomba kufahamu juu ya hilo.


 JIBU: Ili tuweze kuelewa vizuri Ni vema Tukiisoma hiyo habari tokea juu kuanzia ule mstari wa 12-14 ili tupate picha halisi kwanini alisema hivyo..Biblia inasema…

” 12 Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu?

13 Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka;

14 tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure.

15 Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.

16 Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka.

AMEN!

Mpaka hapo Tunaona Paulo alipokuwa huko Koritho alikutana na kundi la watu waliokuwa wanajiita WAAMINI na bado hawaamini kama kweli kuna kiyama ya wafu( ufufuo wa wafu),

na wakati huo huo wapo wengine waliokuwa wanashikilia imani ya kubatiza watu kwa ajili ya wafu. Mambo hayo yalikuwa yanafanywa na hawa wakoritho kama ilivyoelezewa na mwandishi mmoja wa historia aitwaye st.John Chrysostom wa karne ya nne, Achbishop;alisema …Korintho kulikuwa na utaratibu wa mtu ambaye amekufa kabla ya kuamini na hajabatizwa ili kwamba mtu huyo aweze kwenda mbinguni ni lazima mtu mwingine aliye hai ajitokeze na kubatizwa kwa niaba yake, walikuwa wanafanya kumchukua mtu mzima na kumficha chini ya kitanda cha yule marehemu, kisha kuhani anakuja na kumwongelesha yule maiti na kumuuliza kama yupo tayari kubatizwa au la na kama maiti Yule asipojibu, basi yule mtu aliyelala chini yake atamjibu kuhani kwa niaba ya yule maiti kisha atakwenda kubatizwa, na kwa kufanya hivyo atakuwa amemkomboa yule mtu aliyekufa kutoka katika adhabu ya milele.

Sasa kwanini mtume Paulo alinukuu hilo?

Ukiendelea mpaka mstari wa 29” utakutana na jambo hili..”Au je! WENYE kubatizwa kwa ajili ya wafu watafanyaje? Kama wafu hawafufuliwi kamwe, KWANINI KUBATIZWA KWA AJILI YAO? . “

Jambo hili mtume Paulo alilizungumzia kwa kutaka kuwakumbusha wale wasioamini kuwa kuna kiyama cha wafu kuwa kama hawaamini hivyo, kwanini basi wanabatiza mtu kwa ajili ya mfu?Kama wafu hawafufuliwi kamwe. maana kama hawaamini kiyama cha wafu ingewapasa wasifanye hivyo maana kwa kufanya kitendo hicho ni dhahiri kuwa wanaamini kwamba kuna maisha baada ya kufa. je! hawaoni kama wanajichanganya wao wenyewe? ..Hiyo ndiyo sababu ya mtume Paulo kuandika hivyo.

Lakini Mtume Paulo hakumaanisha kuwa yeye au wakristo wa kweli waliokuwa Korintho walikuwa wanafanya hicho kitendo cha kubatiza kwa niaba ya wafu bali ni wengine na ndio maana alitumia neno “WENYE”. wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu Ikiashiria kuwa ni kundi lingine,tofauti na watakatifu.

Na sio tu jambo hilo potofu peke yake la kubatizwa kwa ajili ya wafu lilikuwepo kwenye makanisa bali pia imani nyingine potofu kama ya kusema ” siku ya Bwana imeshakuja” N.K. zilikuwa zikihubiriwa katikati ya makanisa ya Mungu (soma 2Timotheo 2:18, 2Wathesalonike 2:2).

Leo hii imani kama hizi zimeasilishwa pia katika baadhi ya makanisa na madhehebu kama Kanisa Katoliki, likishikilia mistari hii kuthibitisha fundisho la (wakristo kwenda toharani purgatory “) ikiwa na maana kuwa mkristo aliyekufa katika dhambi na hajakamilishwa katika neema anakwenda mahali pa mateso ya muda kwa ajili ya utakaso wa dhambi zake kisha akishatakasika anaweza kwenda mbinguni, hivyo basi muda wa kuendelea kukaa katika hiyo sehemu ya mateso inaweza ikafupishwa kwa kutegemea maombi au sala za walio hai wakimwombea.

Hiyo ndio maana ya kwenda toharani, Jambo ambalo sio sahihi Biblia inasema mwanadamu ameandikiwa kufa mara moja na baada ya kufa ni hukumu (waebrania 9:27), kumuombea mtu aliyekufa, au kubatizwa kwa ajili yake ni moja ya mafundisho potofu ya kuwafanya watu waendelee kustarehe katika dhambi wakiamini kwamba hata wakifa katika dhambi watakuwa na nafasi ya pili ya kusafishwa, usidanganyike hizo ni elimu za shetani wakiyapindua maandiko kuthibitisha uongo wao, hakuna kitu kama hicho cha kwenda Toharani baada ya kufa biblia pia inasema

1 Timotheo 4:1 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, WAKISIKILIZA ROHO ZIDANGANYAZO, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;”.

Amen.

Ubarikiwe.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

KUWA MAKINI NA MITANDAO, NI SHIMO REFU.

NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?

Biblia inamaanisha nini kusema Yeye aliye na sikio, na asikie?

UFUNUO: Mlango wa 19

NILIMWONA SHETANI, AKIANGUKA KUTOKA MBINGUNI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Kaizaly mdemu
Kaizaly mdemu
1 year ago

Ibeliev our God and ilike survive

Kaizaly damasy mvango
Kaizaly damasy mvango
1 year ago

Ibeliev our God…ilike to survive Because llove God