Neno “Mungu” linatokana na neno “Muumbaji” au “mtengenezaji”…Kwahiyo hata mtu akiumba gari yeye ni mungu wa hilo gari..
Hivyo kama gari limeumbwa na mtu, kadhalika kuna kitu kilichomuumba huyo mtu ambaye ni mungu kwa gari…na kitu hicho kilichomuumba mwanadamu ndio kinachoitwa “Mungu wa miungu”…Hakiwezi kuelezewa kwa undani kwasababu hata gari haliwezi kumwelewa mtu kazaliwa wapi, mwaka gani, na anaishije… hata lingefanyaje.
Kwahiyo huyo aliyemuumba mwanadamu ndiye anayeitwa Mungu, (zingatia ‘M’ inaanza kwa herufi kubwa na si ndogo). Huyo anakaa mahali pa kiroho mbali sana panapoitwa mbinguni. Anafanana na mwanadamu lakini si mwanadamu, anatabia kama za mwanadamu lakini si mwanadamu.
Kwasababu sisi wanadamu tunaishi kwa pumzi, kwa chakula, tunahitaji mwanga ili tuone, tunahitaji maji ili tuishi, lakini huyo Mungu yeye ana pua lakini hategemei pumzi, yeye ana macho lakini hategemei mwanga kuona, yeye anaishi lakini hategemei kula, kwasababu kila kitu kimeumbwa na yeye.
Kwahiyo hatuwezi kumwelezea Mungu kwa undani kwasababu ni kitu kilichotutengeneza sisi. Kama vile ilivyo ngumu roboti nililolitengeneza mimi kwa mfano wangu na sura yangu liwe na uwezo wa kujua asili yangu au mwanzo wangu au kunichambua kwa undani mimi ni nani? hata tu huo ufahamu haliwezi kuwa nao…Vivyo hivyo Mungu tukitafuta kumchambua tutakuwa tunapoteza muda, na ndio tutakuwa tunakwenda mbali naye na kuishia aidha kupotea au kukosa majibu kwasababu upeo wake ni wa mbali sana
Lakini pamoja na hayo hajatuumba sisi kama maroboti, sisi katuumba kama wanawe, ambao anatupenda na kutujali kwa namna isiyoelezeka. Na anataka tuishi katika haya maisha kwa kufuata sheria zake ili tupate faida na kufanikiwa, kwa kulitekeleza hilo alimtuma mwanawe wa pekee duniani ili kila amwaminiye asipotee bali apate uzima wa milele. Na huyo mwanawe ndiye Yesu Kristo tunayemfahamu…
Huyu Yesu Kristo pekee ndiye aliyekabidhiwa mamlaka yote ya mbinguni na duniani, hakuna mtu yeyote atakayeweza kumfikia Mungu Baba mbinguni pasipo kupitia kwa yeye (Yesu Kristo)
Yohana 6:44 “14.6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”
Je unataka kwenda kumwona Baba mbinguni?. Kama ndio je umemwamini mwanawe mpendwa Yesu Kristo, na kutubu dhambi zako na kuoshwa kwa damu yake? kama ndio basi unalo tumaini la kumwona Mungu siku moja lakini kama hutamwamini na kuwa mtakatifu hutamwona kamwe.
Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”;
Bwana akubariki sana.
Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
+225693036618/ +225789001312
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
YEZEBELI ALIKUWA NANI
Mbona Mungu anaruhusu watu wapate shida, ilhali ana uwezo wa kutuepusha?
JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.
Rudi Nyumbani:
Print this post