UTUKUFU WA MUNGU NI KITU GANI?

UTUKUFU WA MUNGU NI KITU GANI?

Utukufu wa Mungu ni nini?

Utukufu ni heshima fulani ya hali ya juu inayomfunika mtu au kitu. Wanadamu tuna utukufu wetu, Wanyama wanao utukufu wao kadhalika Mungu naye anao utukufu wake.

Sasa utukufu wa Mungu ni nini/ ni kitu gani?

Jibu: Utukufu wa Mungu ni UTAKATIFU! Ndio Heshima ya juu kabisa Mungu aliyo nayo..Yeye anatambulika kwa utakatifu wake, ambao ni ukamilifu, usafi na HAKI, Hilo ndilo vazi lake kuu, na kitambulisho chake na Heshima yake.

Kutoka 33:17 “Bwana akamwambia Musa, Nitafanya na neno hili ulilolinena, kwa maana umepata neema mbele zangu, nami nakujua jina lako.

18 Akasema, Nakusihi unionyeshe utukufu wako.

19 Akasema, Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza jina la Bwana mbele yako; nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu.

20 Kisha akasema, Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi.

21 Bwana akasema, Tazama, hapa pana mahali karibu nami, nawe utasimama juu ya mwamba;

22 kisha itakuwa wakati unapopita utukufu wangu, nitakutia katika ufa wa ule mwamba, na kukufunika kwa mkono wangu hata nitakapokuwa nimekwisha kupita;”

Mbele kidogo utaona Bwana anamwonesha Musa utukufu wake..

Kutoka 34:5″ Bwana akashuka ndani ya lile wingu, akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina la Bwana.

6 Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli;

7 mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne”.

Hivyo huo ndio utukufu wa Mungu, (Utakatifu na Ukamilifu), yeye ni mwenye rehema, mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu na si mwepesi wa hasira kwa ufupi ni “UTAKATIFU”..

Lakini pia pamoja na kwamba ni mwenye Huruma lakini bado pia hachukuliani na uchafu ndio maana anasema hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia..Hatamwesabia mwasherati, mzinzi, mwongo, mlevi, muuaji, msengenyaji kuwa hana hatia.

Ikimaanisha kuwa Utukufu wake alionao wa UTAKATIFU NA UKAMILIFU, Anataka na sisi tuwe nao.

Ndio maana alisema katika .

Walawi 11:45 Kwa kuwa mimi ni Bwana niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu; basi mtakuwa watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu.

Je! Utukufu wa Mungu upo juu yako nawe pia?..Kumbuka utukufu wa Mungu ni utakatifu, na biblia inasema hakuna mtu atakayemwona Mungu asipokuwa nao…(Waebrania 12:14).

Kwahiyo matendo yote yasiyotokana na utakatifu ndio yanayoondoa utukufu juu ya mtu.

Warumi 3:23 “kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu”

Na huo  Mtu huwezi kuupata ukiwa nje ya Kristo, hivyo ni lazima UOKOKE! Kwa kutubu na kumaanisha kuacha dhambi, kisha ubatizwe katika ubatizo sahihi kwa maji tele (Yohana 3:23) na kwa jina la Yesu kwaajili ya ondoleo la dhambi sawasawa na Matendo 2:38, na baada ya hapo Roho Mtakatifu ataingia ndani yako,. Ambaye ndiye utukufu wa Mungu, atakayekusaidia kuwa Mtakatifu kama vile jina lake lilivyo na kukuongoza katika kweli yote ya Biblia.

Kumbuka anasema “basi mtakuwa watakatifu kwakuwa mimi Bwana ni Mtakatifu”

Bwana akuabariki sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

DHAMBI ILIYOMKOSESHA SHETANI:

SAYUNI ni nini?

JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?

KWANINI DAUDI ALIKUWA NI MTU ALIYEUPENDEZA MOYO WA MUNGU?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
2 years ago

Be blessed with the good explanations