NINI MAANA YA KUKUA KIROHO

NINI MAANA YA KUKUA KIROHO

Ni muhimu kujifunza nini maana ya kukua kiroho,Namna ya kukua kiroho, faida za kukua kiroho. Na pia ni vizuri kujifunza mbinu za kukua kiroho.

Nini maana ya kukua kiroho

Roho ni Utu wa Ndani wa Mtu ule unaozungumziwa katika kitabu cha Waefeso 3:16. Na utu huu wa ndani unakuwa si kwa kimo, bali kwa MAARIFA.

Mtu aliyemchanga kiroho anakuwa ana maarifa machache sana yamhusuyo Mungu. Haijalishi ana elimu  nyingine yoyote nyingi kiasi gani, au ana elimu ya kidunia kiasi gani. Hivyo kukua kiroho maana yake kuongezeka maarifa katika kumjua Mungu.

Namna ya kukua kiroho?

Kwanza ni muhimu kufahamu kuwa hakuna mtu yeyote duniani ambaye ameshakuwa kiroho, na kufikia kiwango ambacho ndio mwisho. Hapana kila siku tunakuwa kiroho, haijalishi tuna maarifa kiasi gani kuhusu Mungu. Bado kila siku tunamsoma yeye kwasababu yeye hamaliziki.

Hivyo njia pekee ya kukua kiroho angalau kufikia kiwango fulani ambacho kitakupa ujasiri wa kuweza kuzidhibiti hila na mbinu za yule Adui. Ni kukaa chini kujifunza Neno la Mungu. Wengi wanaikwepa njia hii na kufikiri kuwa kuna njia nyingine ya mkato ya kukua kiroho, labda ya kuombewa, au kuwekewa mikono. Hakuna njia ya mkato zaidi ya hiyo ndugu!

Mbinu ya kukua kiroho inafananishwa sana na mbinu ya kukua kimaarifa shuleni, ili mwanafunzi afaulu vizuri njia pekee ni kusoma kwa bidii na kuzingaia yale waalimu wanayomfundisha..Kadhalika na sisi wakristo njia pekee ya kukua kiroho ni KULISOMA NENO KWA BIDII. Na kufuatilia kwa makini yale yanayofundishwa na watumishi wa Mungu walio wa kweli.

Na watumishi hao ni zile karama kuu tano, Mitume, Manabii, wainjilisti, waalimu na Wachungaji. Sio Mitume na Manabii na Waalimu unaowaona leo ambao Mungu wao ni tumbo kama biblia inavyosema..Bali Waalimu na wachungaji wanaofundisha kweli yote kama ilivyoandikwa katika Biblia Takatifu. Hao ndio wa kuwafuatilia kwa makini, kama vile mwanafunzi amfuatiliavyo mwalimu darasani..

Mstari ufuatao unaelezea kwa kina dhamana watumishi wa Mungu waliyopewa katika kutuongezea maarifa ya kukua kiroho.

Waefeso 4:11 “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;

12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;

13 hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;

14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu”.

Faida za kukua kiroho

Faida za kukua kiroho tunazipata katika mstari wa 13 na wa 14 unaosema…”

13 hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;

14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu”

Lengo la kukua kiroho hata tutakapofikia cheo cha kimo cha Kristo. Ni ili  tusichukuliwe chukuliwe na kila upepo wa elimu, kwa ujanja wa watu..Kwamfano utasikia watu wanakwambia mti fulani unasababisha kifo kwa wanafamilia. Au utasikia usikae baharini saa saba mchana kuna majini. au utasikia leo kimezuka hichi kanisani watu wanalishwa majani, wengine nyoka. Wengine wataambiwa ili wafunguliwe na matatizo yao watoe pesa kiasi fulani. Ili wafanikiwe wanunue mafuta haya au yale ya upako n.k

Hayo yote ndio yanayoitwa “upepo wa elimu” ambayo huwezi kuyashinda kama ni mchanga kiroho. Hivyo unapokuwa kiroho hizi Elimu zinakuwa hazikupelekeshi..Kunakuwa hakuna elimu yoyote inayozuka inataayoweza kukuchukua kwasababu una Elimu ya kutosha kuhusu Neno la Mungu. Haleluya.

Hivyo hizo ndio mbinu za kukua kiroho. Kwanza Soma Neno kwa bidii binafsi. Pili Jifunze kutoka kwa Watumishi wa Mungu, ambapo unaweza kusikiliza mahubiri kwa njia za semina, mitandano, kwenye vitabu n.k.

Bwana akubariki.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

KIWANGO CHA TATU CHA IMANI.

JE! MUNGU NI NANI?

USIPOLITENDEA KAZI NENO LA MUNGU.

AMANI YA BWANA /AMANI YA MUNGU.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Mwl Lukumay
7 months ago

Mnafundisha vizuri Sana watumishi wa MUNGU…. MUNGU awabariki mno…..Lakini Kuna swali linanisumbua Sana Mimi…. “”Nini inawakilishwa na chura kila Mara kunitembelea kitandani mwangu mpaka kichwani usiku ??”” Naombeni msaada wapendwa !!!

Dickson magambo
Dickson magambo
2 years ago

Nahitaji kujifunza zaidi msaada wako juu ya uwepo wa mungu kwangu na kwako utanisaidio