SIKUJA KULETA AMANI DUNIANI, BALI MAFARAKANO.

SIKUJA KULETA AMANI DUNIANI, BALI MAFARAKANO.

Kwanini Bwana Yesu alisema sikuja kuleta amani duniani, bali mafarakano.

Luka 12: 51 “Je! Mwadhani ya kwamba nimekuja kuleta amani duniani? Nawaambia, La, sivyo, bali mafarakano.

52 Kwa kuwa tokea sasa katika nyumba moja watakuwamo watu watano wamefarakana, watatu kwa wawili, wawili kwa watatu.

53 Watafarakana baba na mwanawe, na mwana na babaye; mama na binti yake, na binti na mamaye; mkwe mtu na mkwewe, mkwe na mkwe mtu”.

Fananisha mstari huu na..

Yohana 14:27 “ Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga”.

Swali ni Je! maneno haya ya Bwana Yesu yanajichanganya yenyewe?..Maana sehemu moja anasema sikuja kuleta amani duniani..Na sehemu nyingine anasema Amani nawaachieni.

Tukiisoma Biblia pasipo msaada wa Roho Mtakatifu hatutaambulia chochote..zaidi ya kuona Biblia ina kasoro nyingi. Lakini tukiisoma kwa Msaada wa Roho Mtakatifu tutanufaika pakubwa na kuelewa mengi.

Ni vizuri kufahamu kuwa Mtu aliye katika dhambi, akiamua kukata shauri la kumpokea Yesu moyoni mwake..Kuna mambo mawili yatatokea maishani mwake… kwanza atapata amani Fulani ya moyo isiyoelezeka…Hiyo amani inaletwa na Roho Mtakatifu mwenyewe…ataanza kuhisi kuna wepesi Fulani na tumaini la ajabu limeingia ndani yake, ambalo limemsababishia amani isiyokuwa ya kawaida…Alikuwa anahofu na huzuni anaanza kuhisi faraja, alikuwa hana tumaini lakini anaanza kuona matumaini n.k

Kupoteza amani nyingine;

Lakini pia pamoja na amani hiyo ya kiMungu kuingia ndani yake..Kuna amani nyingine mtu huyo ataipoteza…Na hiyo ni AMANI YA NJE…Ndio hapo kutokana na kuokoka kwake wale marafiki zake waliokuwa wanakwenda naye kufanya mambo mabaya wanaanza kumchukia, wengine wanaanza kukwaruzana na wazazi wao, wengine wanaanza kugombana na ndugu zao wa kike na wakiume n.k..Sasa amani hiyo ya nje ambayo Inapotea ndiyo Bwana Yesu aliyokuwa anaizungumzia katika Mstari hapo juu unaosema kwamba amekuja kuleta mafarakano.

Lakini kumbuka amani ile ya ndani ya wokovu inakuwa ipo pale pale (Hiyo haiondoki)…yaani mtu pamoja na kwamba kakorofishana na ndugu, au jamaa na marafiki kutokana na imani yake kwa Kristo, lakini bado mtu huyo huyo kila siku moyoni mwake anakuwa anapata amani na faraja na furaha isiyo na kifani kwa kumjua Yesu Kristo.

Gharama ya uanafunzi:

Tunapomfuata Kristo kumbuka siku zote, Huwezi kuepuka kupoteza amani yako ya nje na watu wanaokuzunguka…ulikuwa mshirikina sasa umeacha, washirikina wenzako wataendeleaje kukupenda?..Ulikuwa msengenyaji sasa umeacha, wasengenyaji wenzako wataachaje kukuchukia na kuanza kukusengenya wewe? Na mambo mengine yote ni hivyo.

Gharama ya kuingiza amani ndani ya moyo wako ni kuiopoteza amani ya nje.

Bwana atusaidie tusikwepe gharama hizo, na zaidi ya yote tushinde na zaidi ya kushinda katika Jina la Yesu Kristo.

Ubarikiwe.

Mada Nyinginezo:

JE! NI KWELI UMEMFUATA YESU?

TUMEPEWA, SI KUMWAMINI TU KRISTO, ILA NA KUTESWA KWA AJILI YAKE;

TUUTAZAME PIA MWISHO WA UJENZI WETU.

Biblia inamaana gani kusema;aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi?

ROHO MBAYA KUTOKA KWA BWANA.

 

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
3 years ago

Ameni amen