Mahusiano ya uchumba, ni tofuati na mahusiano ya kimapenzi. Yapo mahusiano ya uchumba ambayo mtu anakuwa nayo kwa mtu aliyemchumbia, hilo halina tatizo maadamu halihusanishwi na vitendo vyovyote vya zinaa. Watu hao wawili wanaweza wakakutana wakala pamoja, wakazungumza pamoja, wakafurahi pamoja, wakatembeleana nyumbani kwao, wakaweka mpingano pamoja..lakini si kulala, pamoja, au kukaribiana kimapenzi au kuonyesha dalili zozote za kukaribiana kihisia, ..
Lakini wapo watu wanaosema, huyu tayari kashakuwa mke wangu, hivyo hakuna shida, sasa nikifanya naye tendo la ndoa si tayari kashakuwa wangu nitamuoa tu?..
Lakini kabla hujafikiria kuwaza hivyo, embu jaribu kuwaza kwanza ni kwa nini lile tendo linaitwa Tendo la Ndoa?..Ulishawahi kujiuliza hivyo?.Linaitwa hivyo kwasababu ni tendo linalofanywa na wanandoa tu peke yao..Nje ya hapo haijalishi unampenda sana huyo mwenzako au unamalengo naye makubwa kiasi gani au kwamba atakuja kuwa mke wako baadaye au mume wako, haijalishi huo tayari ni uasherati..Na waasherati wote Mungu atawahukumu.
Kama ingekuwa ni rahisi hivyo tu, hata mtu anayekutana na kahaba barabarani na kwenda kufanya naye uasherati basi na yeye angejitetea na kusema siku moja nitakuja kumuoa wacha nifanye nae kwanza..Unaona? Hilo jambo halimfanyi yeye kutokuwa muasherati…Tendo la ndoa linalofanywa kwa watu ambao sio wanandoa ni dhambi.
Waebrania 13.:4 Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.
Hivyo ikiwa wewe umempenda binti, na umeshamchumbia, ili ndoa yako ikubaliwe na Mungu..Subiri mpaka wakati Mungu atakapokuunganisha naye rasmi mbele ya Kanisa la Kristo. Na ni kwanini iwe ni katika kanisa la Kristo na si penginepo. Ni kwasababu Mungu unayetaka awaunganishe ndipo alipo. Wapo wengine wanafungishwa ndoa za kimila, au za kiserikali n.k…Unaweza kuziita ni ndoa lakini hizo zote Sio ndoa za kikristo..Ambazo zinaweza kupokea Baraka za Kristo mwenyewe.
Kwasababu kabla ndoa haijaitwa ndoa ni lazima kuwe na makubaliano na mapatano na maagano fulani, sasa kama ukifungishwa nje ya Kristo, hapo ndipo utakutana na nyingine zinaruhusu kuolewa au kuoa mke zaidi ya mmoja, nyingine zinaruhusu kuachana wakati wowote mnapochokana, nyingine ni lazima mtambike, n.k. mambo ambayo yanakinzana kabisa na mpango wa Kristo.
Hivyo ndugu/Dada,..Ndoa yako ikipitia hatua sahihi Kristo anazozihitaji. Basi ujue zipo Baraka tele za kindoa ambazo Mungu ataziachilia kwako na kwa uzao wako baadaye ikiwemo ndoa yenu kupokea ulinzi wa kiMungu tangu huo wakati. Lakini ukiwa na haraka na kuvuruga mipango, na kukimbilia kufanya jambo ambalo wakati wake haujafika, ujue kwa hakika kabisa Mungu hayupo na wewe, na hata ndoa yako hataibarikiwa…Na jaribu kuangalia utaona wengi wa wanaofanya hivyo, mwisho wa siku hawaoani, au wanazaa, na baadaye wanaachana, na watoto wanabakia kuwa na mazazi mmoja,.Hiyo yote ni matokeo ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi nje ya ndoa.
Hivyo ikiwa leo hii upo katika mahusiano ya kimapenzi(ngono) na mwenza wako, mpaka mmeshafikia hatua ya kuzaa, acha mara moja, mkatubu dhambi zenu wote wawili, kwa kumaanisha kabisa kisha muanze utaratibu wa kwenda kufungishwa ndoa yetu kanisani..Na hapo ndipo Bwana atakapowatazama na kuwaangazia rehema zake…Lakini vinginevyo ukiendelea kufanya hivyo ujue kuwa wewe ni mwasherati mbele za Mungu.
1Wakorintho 6:9 “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,
10 wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi”.
Fanya hivyo Na Bwana atakubariki.
Mada Nyinginezo:
Nini Tofauti kati ya uzinzi na uasherati ?
MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI.HATA UASHERATI NAO
NJIA SAHIHI YA KUMPATA MWENZA WA MAISHA KIBIBLIA.
CHAPA YA MNYAMA
JINSI SODOMA NA GOMORA ILIVYOKUWA INAVUTIA SANA..
JINSI NEEMA YA MUNGU ILIVYOKUWA KUBWA KWA MKE WA LUTU.
CHUKIZO LA UHARIBIFU
About the author