MAJESHI YA PEPO WABAYA.

MAJESHI YA PEPO WABAYA.

Shalom.

Waefeso 6:12 “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho”.

Biblia inatuambia biblia inatumia Neno “majeshi” ikimaanisha ni mengi na pia yapo makundi makundi, na inatumia pia neno “wabaya”.Ikimaanisha wanafanya kazi mbaya..

Sasa kabla ya kufahamu ni kwa namna gani yanafanya kazi, ni vizuri kwanza kujua Malaika watakatifu huwa wanafanya kazi gani kwa wanadamu. Kwasababu mapepo hapo kabla ya kuasi walikuwa ni malaika,hivyo baada ya kulaaniwa ndipo yakawa mapepo, na baadhi yao yakatupwa duniani, mengine yakapelekwa kwenye vifungo vya giza (2Petro 2:4),..Sasa haya yaliyopo duniani, hayafanyi kazi nyingine, Zaidi ya kuzitazama zile kazi za malaika watakatifu na kwenda kinyume nazo basi..

Ni mara chache sana mapepo yakitaka kumshambulia mtu, yanakwenda moja moja, huwa yanakwenda kama jeshi, yakisaidiana, kwasababu mbinu hiyo yaliwaiga malaika watakatifu..

Soma Habari za Elisha jinsi yule mtumishi wake, alivyofunguliwa macho na kuona majeshi ya malaika watakatifu yamewazunguka..

Utagundua pia na mapepo nayo yanafanya hivyo hivyo, utaona yule mtu aliyekuwa kule mlimani, uchi, Bwana alipoyaulizwa jina lao, yakasema, Legioni, maana yake tupo wengi (jeshi).

Hivyo ni vizuri kujua kazi ya malaika watakatifu duniani..Nao kazi yao kuu ni hii..KUWAHUDUMIA WATAKATIFU.

Hivyo, mapepo sikuzote ni kunyume na malaika..

Sasa kazi kuu ya malaika watakatifu duniani kama tulivyosema, si nyingine Zaidi ya KUWAHUDUMIA WATAKATIFU..Soma..

Waebrania 1:13 “ Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako?

14 Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?”

Unaweza kuona hapo malaika watakatifu hawajaagizwa kuwahudumia kila mtu tu duniani, isipokuwa wale watakatifu..kumbuka huduma, ni utumishi, malaika hawawatumikii watu waovu, bali watakatifu tu..

Sasa mapepo haya, kwasababu lengo lao sikuzote ni kwenda kinyume na malaika wa Mungu, nao pia wanafanya kazi ya kihuduma ya kuwaharibu watakatifu..na si watu wengine waovu kwasababu hao tayari walishapotea zamani..Mtu mwovu hashambuliwi na mapepo bali anatumiwa na mapepo kufanya kazi zao.

Hivyo ukiokoka leo, majeshi ya mapepo wabaya yanaanza huduma ya kutafuta njia ya kukuangusha uache wokovu. Hiyo ndiyo agenda yao ya kwanza…Hivyo ni vizuri ukajua namna ya kuyadhibiti, ili wokovu wao uwe na matunda na udumu.

Mambo ya kufanya unapooka ni lazima uwe mtu wa.

1) KUSALI: Bwana anasema..

Mathayo 2:41 “Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu”. Hakuna namna unaweza kuzidhibiti/kuyashinda hizo roho kama si mtu wa maombi…

2) KUJIEPUSHA NA UOVU: Maovu, yanauficha uso wa Mungu, Hivyo inapelekea pia na malaika wa Bwana kuondoka, matokeo yake ulinzi wa Mungu unaondoka juu yako, na mapepo yanachukua nafasi ya kukuangusha.(Isaya 59:1-2 )

3) KUJIFUNZA NENO: Neno la Mungu likikaa kwa wingi ndani yako unakuwa na maarifa ya kutosha ya kumshinda ibilisi (Wakolosai 3:16). Kumbuka Kristo alimshinda shetani kwasababu Neno la Mungu lilikuwa kwa wingi ndani yake.

4) KUFANYA USHIRIKA NA WENGINE: Kukutanika na wengine, kanisani, kwenye vikundi vya maombi, kwasababu ukiwa peke yako upo hatarini shetani kukupindua lakini mkiwa wengi, ni ngumu ibilisi kukupata..(Waebrania 10:25).

Mhubiri 4:11 “Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto?

12 Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi”.

Hayo ni mambo makuu yatakayokusaidia kujikinga na majeshi haya, na kuyakaribisha majeshi ya Malaika wa Mungu yatembee nawe.

Kumbuka shetani Pamoja na malaika zake( yaani mapepo), wanafahamu kuwa muda wao ni mchache sana. Hivyo wanaongeza bidii katika kufanya kazi ya kuwaangusha watakatifu.

Sasa endapo mtu asipojibidiisha, na kukaa kuendelea na Maisha ya kawaida ya siku zote, baada ya kuokoka , ni ngumu mtu huyo kushindana na hayo majeshi ya mapepo, Utarudi tu nyuma kama sio kuucha wokovu kabisa.

Hivyo tuongeze bidii, na kuzingatia hivyo vigezo.

Ubarikiwe.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

Shetani ni nani?

Je! Mtume Paulo alimwabudu malaika aliyetembea naye?

KIFO CHA MTAKATIFU PERPETUA NA FELISTA.

HUDUMU YA MALAIKA WATAKATIFU.

UJIO WA BWANA YESU.

RABI, UNAKAA WAPI?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Thomas
Thomas
9 months ago

Endelea kutoa maarifa juu ya mungu pia unaweza kuntmia kwnye email