Isaya 43, USIOGOPE!

Isaya 43, USIOGOPE!

Isaya 43:1 “Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.

2 Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.

3 Maana mimi ni Bwana, Mungu wako; Mtakatifu wa Israeli, mwokozi wako, nimetoa Misri kuwa ukombozi wako; nimetoa Kushi na Seba kwa ajili yako.

4 Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako”.

Kuhukulu maana yake ni “kutengeneza”..Kwahiyo hapo Bwana anamwambia Yakobo aliyemtengeneza na kumuumba kwamba asiogope!. Yakobo anayezungumziwa hapo sio Yule Yakobo mwana wa Isaka…Yule alishakufa kitambo lakini Yakobo anayezungumziwa hapa ni Taifa la Israeli, Taifa zima la wana wa Israeli ndio linalojulikana kama Yakobo..Na ndilo linaambiwa lisiogope!..wapitapo katika maji mengi Mungu atakuwa pamoja nao.. na katika mito, hawatagharikishwa; na waendapo katika moto, hawatateketea; wala mwali wa moto hautawaunguza..Kwasababu alikuwa wa thamani machoni pa Bwana.

Haya ni maneno machache tu lakini ya faraja kubwa sana…Kama Mungu analikumbuka agano lake na Ibrahimu kwa watu wake Israeli..kamwe hawezi kulisahau agano la mwanawe mpendwa Yesu Kristo, ambaye alikuja kufa kwa ajili yetu sisi na kutufanya kuwa Taifa teule na Takatifu, watu wa milki yake. Agano lake hilo la ukombozi, linatufanya tuonekane wa thamani sana kuliko lile la kwanza. Na hivyo maneno hayo pia yanatuhusu sisi tuliomwamini Yesu, na wewe ambaye utamwamini leo…kwamba USIOGOPE!…Usiogope vitisho vya adui!..usiogope magonjwa!..usiogope shida na majaribu!..Bwana Mungu wako ndiye aliyekuhuluku(yaani aliyekutengeneza)…

Majaribu unayoyapitia sasa ni maji mengi…lakini amesema atakuwa pamoja na wewe!…shida unazozipitia sasa baada tu ya kusimama kiimani ni mafuriko, lakini amesema hayatakugharikisha!..misiba na mateso unayoyapitia sasa ni miali ya moto, lakini amesema haitakuunguza! Hivyo jipe moyo, simama endelea mbele..kwasababu wewe ni wa thamani machoni pake.

Na mwisho amesema “kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako”…Maana yake ni kwamba maisha yako kwake yanathamani kuliko ya watu wengine wasiomtumainia yeye na Taifa lingine lisilomcha yeye.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu ni wakina nani?

Mtu astahiliye hofu ni yupi?

MWEZI NI ISHARA GANI KWETU?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Leave a Reply