Fahamu jinsi ya kusoma biblia.
Awali ya yote ninakupongeza kwa nia yako kutamani kujua jinsi ya kusoma biblia. Hapo mwanzoni kabla sijamjua vizuri Mungu, kati ya vitabu ambavyo nilikuwa ninaona ni vigumu kuvielewa, basi kimojawapo kilikuwa ni BIBLIA.
Lakini siku, na miaka ilivyozidi kwenda niligundua kuwa sio, nataka nikuambie hakuna kitabu kilicho kirahisi kama Biblia. Kwanini ninakuambia hivyo?.. Kwasababu ni kitabu kinachoweza kusomwa na watu wa makundi yote. Mzee anaweza kukisoma, kijana anaweza kukisoma, asiye na elimu anaweza kukisoma mwenye PH.D anaweza kukisoma..Na wote wakafaidika na kilichoandikwa mule. Vilevile hakina ngazi yoyote ya awali kukipitia ndio uelewe kama vilivyo vitabu vingine. Leo hii ukihitaji kusoma kitabu cha Fizikia, itakugharimu kwanza upitie elimu za chini uwe na msingi, vinginevyo hutaweza kukielewa..Lakini biblia haina misingi hiyo.
Tena na cha kushangaza Zaidi ni kwamba, biblia imetoa nafasi ya kueleweka na watu wasio na elimu kuliko wenye hekima na ujuzi..(Luka 10:21)
Jinsi ya kusoma biblia.
Mambo ya kuzingatia kabla hujaanza kusoma biblia.
Hivyo ukizingatia hizo hatua, utakuwa umeshajua jinsi ya kusoma biblia. Pia kumbuka, kwenye suala la kitabu kipi uanzane nacho, au kipi usianzane nacho, hilo halina umuhimu sana, unaweza kuanza na kitabu chochote kile na huko huko Roho Mtakatifu mwenyewe atakufunulia mambo ya ajabu, Na kukufikisha pale anapotaka ufike kwa siku hiyo, kwasababu hiyo ndio kazi yake aliikusudia juu yetu.
Yohana 16:13 “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake”.
Jinsi ya kusoma biblia.
Pia Kujifunza biblia ni Pamoja na kusikiliza na mafundisho mengine ya Neno la Mungu yanayohubiriwa.. Yale yanakuwa kama TUTION kwako. Hivyo hapa pia yapo mafundisho mengi ya kukusaidia kuielewa biblia, kwenye website hii yapo mafundisho Zaidi ya 1000 ya mada mbalimbali, na Maswali na Majibu mengi sana, ambayo ukiyasoma naamini utapiga hatua kubwa sana katika kuielewa biblia..Hivyo kama upo tayari bofya hapa uende moja kwa moja katika orodha hiyo….>> MAFUNDISHO
Bwana akubariki sana.
Jinsi ya kusoma biblia.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au tutumie ujumbe kwa namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Mihimili mikuu (4) ya mkristo katika safari yake ya wokovu.
USIPOLITENDEA KAZI NENO LA MUNGU.
JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOWAFUNULIA WATU MAANDIKO.
TABIA YA KIPEKEE USIYOIJUA KUHUSU NENO LA MUNGU.
NENO LA MUNGU NI DAWA ILIYO TOFAUTI NA DAWA NYINGINE.
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
KABLA YA MAANGAMIZI, KRISTO HUWA ANAONYESHA KWANZA NJIA YA KUTOROKEA.
About the author