Yesu akalia kwa sauti kuu..
Wengi tunajiuliza ni maneno gani aliyatoa Bwana Yesu pale msalabani alipolia kwa sauti ya juu namna hiyo?
Embu tusome vifungu vyenyewe;
Marko 15:34 “Na saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? 35 Na baadhi yao waliosimama pale, walisema, Tazama, anamwita Eliya. 36 Na mmoja akaenda mbio, akajaza sifongo siki, akaitia juu ya mwanzi, akamnywesha, akisema, Acheni, na tuone kwamba Eliya anakuja kumtelemsha. 37 NAYE YESU AKATOA SAUTI KUU, AKAKATA ROHO. 38 Pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini. 39 Basi yule akida, aliyesimama hapo akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu”.
Marko 15:34 “Na saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
35 Na baadhi yao waliosimama pale, walisema, Tazama, anamwita Eliya.
36 Na mmoja akaenda mbio, akajaza sifongo siki, akaitia juu ya mwanzi, akamnywesha, akisema, Acheni, na tuone kwamba Eliya anakuja kumtelemsha.
37 NAYE YESU AKATOA SAUTI KUU, AKAKATA ROHO.
38 Pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini.
39 Basi yule akida, aliyesimama hapo akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu”.
Ili kujua ni maneno gani aliyasema, ni vizuri tukaangalia katika vitabu vingine vya injili vinasema katika wakati huo huo alipokuwa anakaribia kukata roho Tusome..
Yohana 19:28 “Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu. 29 Kulikuwako huko chombo kimejaa siki; basi wakatia sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakampelekea kinywani. 30 Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, IMEKWISHA. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake.”.
Yohana 19:28 “Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu.
29 Kulikuwako huko chombo kimejaa siki; basi wakatia sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakampelekea kinywani.
30 Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, IMEKWISHA. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake.”.
Unaona hapo mstari wa 30 unaonyesha dakika ile ya mwisho kabla ya kuikata roho yake alisema haya maneno “IMEKWISHA”..
Maneno haya hakuyasema kwa unyonge, au kwa utaratibu, au kwa sauti ya kawaida kama yale mengine..Hapana, bali alipofika hapo biblia inasema AKATOA SAUTI KUU.. IMEKWISHA.
Sauti ambayo kila mmoja aliyekuwa maeneo yale aliyasikia maneno haya..kiasi kwamba Yule akida wa askari alipoona jinsi alivyokata roho kwa Tamko zito kama lile..Akakiri kuwa Yule alikuwa kweli ni mwana wa Mungu.
Yesu akalia kwa sauti kuu,
Lakini kwanini Bwana Yesu aamue kufanya vile?,
Ilikuwa ni kutuambia mimi na wewe kuwa Ile hati ya mashitaka imekwisha. Na ndio maana saa ile ile pazia la hekalu likapasuka, na kiti cha rehema kikaonekana, ikiwa na maana kuwa tangu wakati wa Kristo kufa, rehema inapatikana bure, na kwa uwazi, sio tena nyuma ya pazia ambapo ilihitaji kuwepo na mtu wa kuwapatanisha na Mungu(Kuhani mkuu)..Lakini sasa hilo halipo tena, kwasababu hati ya mashitaka imeondolewa.
Mtu yeyote anaweza kumkaribia Mungu na kusamehewa kupitia YESU KRISTO.
Hivyo hata na wewe leo, kama ni mwenye dhambi unaweza kuupokea msamaha kutoka kwake hapo hapo ulipo. Yesu anaweza kuja ndani ya moyo wako siku hii hii ya leo, bila hata ya kuhani kuwepo karibu yako, au mchungaji, au mtu yeyote..Ni wewe tu kufungua moyo wako, na kukubali kumpokea Yesu.
Ikidhamiria kufanya hivyo alisema mwenyewe..
Yohana 6:37 “Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.”
Hivyo leo hii ukimpa maisha yako utaanza kuona badiliko la ajabu sana ndani yako. Kama upo tayari sasa kutubu dhambi zako..Basi fungua hapa kwa ajili ya sala ya toba. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Mada Nyinginezo:
Kwanini Bwana Yesu alisema pale msalabani naona kiu?
USO WAKE ULIKUWA UMEHARIBIWA SANA ZAIDI YA MTU YE YOTE.
KWANINI YESU KRISTO NI WA MUHIMU KWETU SASA?
WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.
MKUU WA UZIMA AKUWEKE HURU.
Rudi Nyumbani:
Print this post