USO WAKE ULIKUWA UMEHARIBIWA SANA ZAIDI YA MTU YE YOTE.

USO WAKE ULIKUWA UMEHARIBIWA SANA ZAIDI YA MTU YE YOTE.

Wokovu huu ambao tumeupata bure, tusidhani yule aliyetugawia hakuingia gharama yoyote kuupata,..Halikuwa ni jambo la kukaa mbinguni tu na kusema niamnini mimi mtaokoka!..Hilo lisingewezekana kamwe, ili kuunda kitu kinachoitwa “wokovu” ilimpasa afuate kanuni Fulani..ilimpasa kwanza aache enzi na mamlaka yote mbinguni, awe hana kitu, kisha ashuke hapa duniani, aishi kama mwanadamu mwingine yoyote yule aliyezaliwa na mwanamke, aumwe wakati mwingine, audhiwe, apitie umaskini, kisha na yeye pia ajaribiwe na shetani, aonekane kama atashinda au la, ..Lakini kama tunavyosoma aliyashida yote kwa muda wa miaka 33 bila kutenda dhambi yoyote licha ya kupitia vipingamizi vyote vya kibinadamu..

Lakini sio hilo tu, ilimgharimu uhai pia, ili aweze sasa kukikamilisha hicho kitu kinachoitwa WOKOVU KWA MWANADAMU.. Ndio hapo akalazimika aende msalaba akapigwe afe, damu imwagike ili kusudi kwamba mimi na wewe tupokee huo wokovu kwa gharama alizoingia..

Lakini wengi wetu tunadhani mateso aliyoyapita yalikuwa ni ya kawaida tu, biblia inatuambia Bwana aliharibiwa uso wake, na mwili wake, Zaidi ya mwanadamu mwingine aliyewahi kuishi hapa duniani..

Soma..

Isaya 52:13 “Tazama, mtumishi wangu atatenda kwa busara, atatukuzwa, na kuinuliwa juu, naye atakuwa juu sana.

14 Kama vile wengi walivyokustaajabia, (USO WAKE ULIKUWA UMEHARIBIWA SANA ZAIDI YA MTU YE YOTE, NA UMBO LAKE ZAIDI YA WANADAMU),

15 ndivyo atakavyowasitusha mataifa mengi; wafalme watamfumbia vinywa vyao; maana mambo wasiyoambiwa watayaona; na mambo wasiyoyasikia watayafahamu”.

Jaribu kuchua muda utafakari!, chukua muda utafakari hata dakika 15 au 20, fikiria huo uso uliwezekanikaje kuharibiwa Zaidi ya mtu yoyote hapa duniani, na mwili wake vivyo hivyo, ndipo utakapofahamu kuwa mapigo aliyopigwa Bwana hayakuwa ya mwanadamu wa kawaida, alikuwa kama nyama buchani, kile unachokifahamu kwenye filamu ni mfano mdogo wa jinsi Bwana alivyokuwa anaonekana, na hiyo yote ilimpasa apitie vinginevyo mimi na wewe tusingeupata wokovu..

biblia inasema..

“Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, NA KWA KUPIGWA KWAKE SISI TUMEPONA”.(Isaya 53:5)

Uso wake na mwili wake usingeharibiwa kwa mapigo mabaya kama yale ambayo mengine hata hayajaandikwa kwenye biblia, mimi na wewe leo hii tusingeufikia uponyaji wa roho zetu. Lakini jiulize wewe ndugu ambaye bado hujamwamini yeye licha ya kwamba umekusogezea wokovu huo bure mbele yako bila malipo yoyote..Jiulize, siku ya leo ukifa katika hali yako ya dhambi utawezaje kuokoka?

Kumbuka wokovu unapatikana bure, sasa bila gharama yoyote, usisubiri mpaka mlango wa neema ufungwe ndipo uje uutafute, hilo halitawezekana tena, wakati huo ukifika wewe utakuwa ni wa kusubiria tu kwenda jehanamu ya moto, lakini leo hii ukiyasalimisha Maisha yako kwake, licha tu ya kwamba unayo tiketi ya kwenda mbinguni, lakini pia ile damu yake ya thamani iliyomwagika pale msalabani wakati huo huo itaanza kukunenea mema juu ya Maisha yako angali ukiwa bado hapa duniani.

Hivyo tubu ndugu kama bado hujafanya hivyo..maadamu Bwana Yesu ni Rafiki yetu wa kweli, anayetupenda upeo.

Jina lake libarikiwe daima.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

YATAFUTE YALIYO JUU SIKU ZOTE.

Kwanini Mungu alisema hakuna mtu awazaye kuuona uso wake akaishi?

KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?

NI KITU GANI PETRO NA YOHANA WALIKIGUNDUA KABURINI?

KANUNI RAHISI YA KUFANIKIWA.

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!

NGUVU YA MSAMAHA

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Fmakungisa
Fmakungisa
4 years ago

Inbox