RAFIKI MWEMA.

RAFIKI MWEMA.

Rafiki mwema ni nani?


Uzuri ni kwamba kila mmoja wetu alishawahi kuwa na rafiki au marafiki katika maisha yake.. Kama ulishawahi kuwa na marafiki wengi utagundua kuwa wengine walikuwa marafiki zako kwasababu mliendana tu tabia hivyo tu,, na  wengine walikuwa marafiki kutokana na maslahi Fulani au mazingira Fulani au fursa Fulani, labda shuleni,  au kwenye biashara au kazini, au katika mambo ya kiimani n.k…

Kati ya hao wapo ambao ni wa kudumu yaani mnaweza kupotezana hata kwa muda mrefu lakini urafiki wenu ukadumu palepale, au mazingira Fulani yakatokea aidha ya kutofautiana kipato lakini bado urafiki wenu ukaendelea kudumu,  na wapo ambao ni wa muda tu, kukitokea kutengana kidogo, au mazingira Fulani kubadilika basi urafiki huo unakufa hapo hapo..

Lakini kwa vyovyote vile katika makundi yote hayo swali ni je utawezaje kumtambua rafiki mwema?

Jibu ni rahisi rafiki mwema, ni Yule ambaye atauweza kuutoa uhai wake ili wewe upone. Kwamfano, rafiki  yako asikie wewe umelazwa figo zako zote mbili zimekufa upo hoi kitandani mahuti huti, ili uishi ni lazima figo zote mbili zipatikane kutoka kwa watu wengine ili upachikwe wewe uendelee kuishi, Halafu wakati huo huo anatokea rafiki yako, ambaye hana hata undugu na wewe, mlikutana tu mkaendana tabia, mkashirikiana pamoja..

Na sasa anakuambia rafiki yangu, mimi leo hii nimeamua kuzitoa figo zangu zote mbili, ili wewe upone, Unaweza ukajiuliza huyu mtu anawaza nini? Akitoa figo zake sisi yeye atakufa, na itakuwa hasara tu ile ile..Ukizingatia yeye bado anayo malengo yake mengi ya maisha, mimi ninafaida gani kwake? Pengine unamkatalia Lakini yeye bado anakusisitiza kuwa anakwenda kutoa figo zake zote mbili afe ili wewe upone.. Na kweli anakwenda kufanya hivyo. Anatolewa unapewa wewe na yeye muda huo huo anakufa.. Je! Mtu kama huyo si zaidi ya rafiki mwema kwako?

Ukweli ni kwamba Katika ulimwengu mzima hakuna mtu anayeweza kufanya hivyo..

Lakini habari njema ni kwamba yupo ambaye aliweza kufanya hivyo kwa ajili yangu na wewe ili tupone..Na mtu huyo si mwingine zaidi ya YESU, alisema mwenye hivi…

Yohana 15:13 “Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.

14 Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo”.

Upendo huu ni zaidi ya upendo wa ndugu, Ndugu yako hawezi kuifikia hatua hii, ya kufa ili wewe uokoke, lakini Kristo alikufa ili mimi na wewe tupate uzima wa milele..

Na ndio maana maandiko yanasema..

Mithali 18: 24 Ajifanyiaye rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe; Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.

Sasa huyu rafiki aambatanaye kuliko ndugu, ndio YESU KRISTO mwenyewe..

Hivyo ukimkaribisha huyu maishani mwako, ni uhakika kuwa utakuwa salama, na hutakuwa na wasiwasi kwamba utapotea tena baada ya hapo, kwasababu yeye tayari alishalipa gharama za upotevu wako kabla hata hujazaliwa. Kwahiyo kama ukimfanya leo kuwa rafiki yako, basi atakuwa rafiki yako kweli kweli, na mema yote utayaona..

Lakini ule mtari wa 14 anasema..

“Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo.”

Unaona?  Ili na wewe Yesu awe rafiki yako ni sharti utii anayokuamuru.. Kama ulikuwa ni mwenye dhambi unatubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, kisha unakwenda kubatizwa katika maji mengi kama alivyotupa  maagizo katika Mathayo 28:19, Na baada ya hapo atakutia muhuri kwa Roho wake Mtakatifu atayemwachilia ndani yako wakati huo huo. Na hapo ndipo utakuwa na uhakika kuwa sasa umeshafanyika kuwa rafiki yake.

Ikiwa upo tayari kufanya hivyo..

Basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU  MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.

Ubarikiwe sana.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

WAKAKAA KWAKE SIKU ILE. NAYO ILIKUWA YAPATA SAA KUMI.

YESU MPONYAJI.

Maana ya ‘Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake’

KILA MMOJA WENU AJUE KUUWEZA MWILI WAKE.

HAPO NDIPO WATU WALIPOANZA KULIITIA JINA LA BWANA.

HATA NA BARNABA PIA AKACHUKULIWA NA UNAFIKI WAO!!

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments