KILA MMOJA WENU AJUE KUUWEZA MWILI WAKE.

KILA MMOJA WENU AJUE KUUWEZA MWILI WAKE.

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze maandiko…Si vibaya tukajikumbusha yale ambayo tumeshawahi kujifunza mahali tofauti tofauti…

biblia inasema katika..

1Wathesalonke 4:4 “kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima

5 si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu”.

Biblia imetufundisha kujizuia, maana yake ni yale ambayo unaweza kuyafanya, unajinyima kuyafanya…Kadhalika imetufundisha pia kuiweza miili yetu…Kuiweza miili yetu hakuna tofauti sana na kujizuia…Kuuweza ni hali ya wewe kuuendesha mwili na si mwili kukuendesha wewe.

Na moja ya vitu vinavyowaendesha watu wasiomjua Mungu ni tamaa ya uasherati..ndio inayozungumziwa hapo katika mstari wa 5.

Na hiyo ili iondoke ni lazima kujifunza kuulazimisha mwili kukutii wewe, na huko kwanza kunakuja kwa kumkaribisha Yesu katika maisha, na baada ya hapo kumpokea Roho Mtakatifu ambaye atakusaidia kukupa nguvu za kuweza kuutiiisha mwili wako…sio kwamba Roho Mtakatifu atakuzuia usitende dhambi hapana!..Yeye atakupa uwezo wa wewe kuishinda dhambi inayofanya kazi katika viungo vyako (yaani mwili wako)

Yakobo 4:1 “Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?”

Na baada ya kumwamini na kumpokea Yesu, hatua inayofuata ni kujitenga mbali na vichocheo vyote vya tamaa….shetani anatamani utubu tu lakini usiache ile dhambi….anataka utubie uzinzi/ uasherati lakini hataki ufanye uamuzi wa kuacha kutazama picha chafu za ngono, anataka utubie anasa na matusi lakini hataki uache kuisikiliza ile miziki ya kidunia ambayo hiyo ndio kichocheo cha kwanza cha mambo hayo..n.k

Vitu vyote vinavyokusababishia kulipuka tamaa unajiweka mbali navyo…kama ni vipindi kwenye tv na movie, unajitenga navyo, kama ni aina Fulani ya marafiki, ni hivyo ivyo kama ni magroup Fulani kwenye mitandao, unayaacha…Ni wewe kufanya uamuzi kwanza..kwa kufanya hivyo utafanikiwa kuuweza mwili wako..

Hivyo tunaonywa tujifunze kuiweza miili hii…Inawezekana kabisa kuishinda na ni rahisi sana, ndio maana biblia imesema tujifunze kuiweza! ingekuwa haiwezekani kabisa kuiweza, basi Mungu si dhalimu asingetupa jukumu zito kiasi hicho.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Je! Ni kweli ubatizo wa maji hatuuhitaji tena?

JE! PAKA KULIA USIKU NI ISHARA YA UCHAWI?

BIBLIA INATUASA TUFANYE NINI KATIKA ZAMA HIZI ZA UOVU?

KUTAHIRIWA KIBIBLIA

USIFE NA DHAMBI ZAKO!

JE BIKIRA MARIAMU ALIKUFA?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments