Kuzimu kuna nini?
Kuzimu sio mahali pa kupatamani hata kidogo, wala sio mahali ambapo utatamani hata adui yako aingie..
Na ndio maana Bwana Yesu alisema maneno haya..
Marko 9:43 “Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanum, kwenye moto usiozimika; 44 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.] 45 Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum; [ 46 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.] 47 Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum; 48 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki”.
Marko 9:43 “Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanum, kwenye moto usiozimika;
44 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.]
45 Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum;
[ 46 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.]
47 Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum;
48 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki”.
Unaona, akiwa na maana kuwa kama itabidi kiungo chako kimoja tu cha thamani, kiondoke ni heri ukafanya hivyo kuliko uende kuishia huko milele.
Ikiwa unataka kujua kwa Urefu Jehanum ni nini? Unataka kujua hao funza wanamaanisha nini?, kuzimu kuna nini ,fungua hapa usome Habari yao.. >>>> Jehanamu ni nini?
Haya Maisha tuliyopewa ni ya kitambo kifupi sana, tunapaswa tujitathimini tukifa leo tutakwenda wapi ikiwa tupo nje ya Kristo? Biblia inatuambia Kuzimu haishibi watu, wala uharibifu hauna kifuniko, ikiwa na maana kuwa kila dakika, kila sekunde watu wanashuka huko wengi sana..
Lakini kwanini hayo yote yatukute angali bado tunao muda wa kutubu? Tutubu dhambi zetu, na kuyasalimisha Maisha yetu kwake, tuseme ulimwengu sasa basi, leo hii tunamgeukia Kristo.
Hivyo Ikiwa wewe ni mmojawapo ambaye unasema leo nipo tayari kumpa Yesu Maisha yangu, basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana.
Basi, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE. ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE. AMEN.
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.
ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.
AMEN.
Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuwa na uhalali kwa kuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako.
Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwabudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.
Hongera kwa kuokoka.
Pia nakualika kutembelea tovuti hii mara kwa mara, yapo mafundisho mengi zaidi ya 1000, na maswali mengi sana yaliyojibiwa ya kwenye biblia..
Au kama utakuwa unapenda utumiwe kwa njia ya whatsapp basi utatumia ujumbe katika namba hii +255789001312 .. Bwana akubariki sana.
Mada Nyinginezo:
MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
CHUKIZO LA UHARIBIFU
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
UTAWALA WA MIAKA 1000.
HAPO NDIPO WATU WALIPOANZA KULIITIA JINA LA BWANA.
Rudi Nyumbani
Print this post