Kuota upo na mtu maarufu/kuota unaongea na mtu maarufu.

Kuota upo na mtu maarufu/kuota unaongea na mtu maarufu.

Kuota upo mtu na maarufu/kuota unaongea na mtu maarufu kuna maana gani?

Ndoto zipo katika makundi makuu matatu, zipo ndoto zinazotokana na Mungu, pia zipo ndoto zinazotokana na shetani, halikadhalika zipo ndoto zinazotokana na mtu mwenyewe.

Ili kufahamu vizuri juu ya makundi haya. Bofya hapa usome. >>> Nitajuaje kama ndoto ni ya Mungu au ya Shetani?

Wengi wetu tunakosa shabaha pale tunapotaka kila ndoto ipatiwe tayari yake ya rohoni, lakini ukweli ni kwamba si kila ndoto inayotafsiri ya maana, husususani hizo zinazotokana na sisi wenyewe.

Sasa tukirudi kwenye swali Kuota upo na mtu maarufu/kuota unaongea na mtu maarufu kuna maana gani?

Jibu ni kwamba, ndoto nyingi za namna hii zinatokana na shughuli zetu za kila siku

Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno”

Unaona Shughuli za kila siku ni Pamoja na yale mambo ambayo tunayoana mara kwa mara kila siku, au tunayasikia, kwamfano mtu kama raisi wa nchi, huyu ni mtu ambaye karibu kila siku tunamwona katika vyombo vya Habari, au tunamsikia katika radio, au tunamsoma katika magazeti, au tunamsikia akizungumziwa na watu wengine..

Ni mtu ambaye kila mmoja wetu amemkaa kichwani, kama vile tu ndugu zetu wa nyumbani. Hivyo mtu kuota raisi wa nchi, au kuota unaongea na raisi,au kuota uko na raisi si jambo la kushangaza.

Naamini ni maelfu ya watu kila siku yanamuota raisi wa nchi yao.

Na sio raisi tu, unaweza kumwota mtu mwingine yoyote maarufu, ambaye tayari anajulikana sana katika jamii, inaweza ikawa ni msanii, au mbunge, au mchungaji, au mchezaji n.k.

Hivyo ndoto ya namna hii, ikikujia usiitilie maanani sana.

Lakini ikija katika uzito wa hali ya juu, na ndoto yenyewe umeiota imeonekana kama ilikuwa ni kweli. Na ukaona kama ni bahati umekutana na mtu huyo,

Basi ujue ni Mungu anataka kukupa hisia  Fulani ya kipekee uionje pale unapokutana na mtu Fulani maarufu. Anataka uone, jinsi inavyokuwa,  ikiwa watu maarufu wa dunia hii ukikutana nao unajihisi wewe ni mtu Fulani spesheli uliyepata bahati, vipi kuhusu kukutana na yeye ambaye ni Maarufu na Mkuu kuliko watu wote na vitu vyote duniani siku ile? Utakuwa katika hali gani?

Anataka uone siku ile maelfu kwa maelfu wa watu watakapo kusanyika mbele zake , kupokea heshima zao kutoka kwake wewe utakuwa wapi?

Je! atakuita, uwe karibu naye, au atakukataa na kukufukuza?

Bwana Yesu mwenyewe alisema..

Luka 9:26  “Kwa sababu kila atakayenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wake na wa Baba na wa malaika watakatifu”.

Hivyo usimwonee haya Kristo mpe leo Maisha yako. Ili siku ile, atakapopokea heshima kutoka kwa watu wote na malaika zake, basi na wewe pia akuite.

Hiyo ndio maana ya Kuota upo na mtu maarufu/kuota unaongea na mtu maarufu.

Hivyo Kama upo tayari kumpa Yesu Maisha yako leo, utataka kuongozwa sala ya toba basi fungua hapa >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Ubarikiwe sana..

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi

Mada Nyinginezo:

KARAMU YA MWANA-KONDOO.

BASI MUNGU ALIMWADHIMISHA MNO.

MFALME ANAKUJA.

KWANINI YESU KRISTO NI WA MUHIMU KWETU SASA?

MTINI, WENYE MAJANI.

Uasherati wa Kiroho maana yake nini?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
3 years ago

Nakushauri kama hujui ndoto usiandike makala kwani unakera sana kwa tafsiri zako mbovu.