Neno la Mungu ni upanga.

Neno la Mungu ni upanga.

Ni kwa namna gani Neno la Mungu ni upanga?


Biblia haisemi Neno la Mungu ni upanga tu, hapana bali inasema  ni zaidi ya upanga wowote mkali ukatao kuwili..

Waebrania 4:12 “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

13 Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.”.

Unaona? Ni zaidi ya upanga. Na kama tunavyojua upanga unaokata kuwili ni upanga ambao unatumika sana sana katika vita, yaani ukiupeleka upande wa kulia unakata na vilevile ukiurudisha upande wa kushoto bado unakata(Ufunuo 1:16, 2:12, 19:12).. Ni mfano wa msimeno unakata mbele na nyuma.

Sasa Mungu anakuambia Neno lake ni zaidi ya huo upanga. Akiwa na maana kuwa linakata pande zote, kwa wale wote watakaokwenda kinyume nalo, linakata matajiri, linakata maskini, linakata wenye vyeo linakata wasio na vyeo, linakata weupe, linakata weusi, linakata wenye dhambi vilevile linakata na waliookoka ikiwa hawatadumu katika maagizo yake.

Na kukata kwake sio butu, bali kwa ukali sana, likipita linatenganisha kabisa kabisa, yaani mfano Mungu akipitisha upanga katika taifa basi ujue taifa hilo ndio mwisho wake umefika, akipitisha upanga katika familia basi ujue ni upanga kweli kweli unaotenganisha, haijalishi  ndugu hao watakuwa wanapendana au wameshikamana kiasi gani.Soma.

Mathayo 10:34 “Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga.

35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu;

36 na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake”.

Vilevile alisema, katika wakati wa Mwisho atayaangamiza mataifa kwa Neno lake, ambao ndio huo upanga utokao katika kinywa chake..

Ufunuo 19:14 “Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.

15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.

16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA Bwana WA MABwana”.

Hivyo, Mungu anatuasa tutubu, tumgeukie yeye, ili kusudi kwamba Neno lake, liwe chakula na uzima kweli badala ya upanga, Kwasababu kwa kupitia hilo hilo Mungu alifanya mbingu na nchi, kwa kupitia hilo hilo, alituumba sisi, kwa kupitia hilo hilo alinatuponya na kutuokoa, na kutubariki. Lakini kwa kupita hilo hilo atatuhukumu kama tusipotaka kuitii injili. Na ndio anatuhimiza mpaka sasa tutubu kwa kurudi kwake kumekaribia.

Ufunuo 2.16 Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu.

Neno la Mungu ni upanga.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

USIPOLITENDEA KAZI NENO LA MUNGU.

UTASIMAMA PEKE YAKO SIKU ILE.

MAPAMBANO DHIDI YA SHETANI.

KWANINI TUNAPASWA TUJIZUIE?

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

UTAWALA WA MIAKA 1000.

ROHO ZILIZO CHINI YA MADHABAHU:

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments