Kwanini Raheli aliiba miungu ya Baba yake, (Labani) Mwanzo 31:19.

Kwanini Raheli aliiba miungu ya Baba yake, (Labani) Mwanzo 31:19.

Ni kwanini Raheli afanye vile, ilihali Mungu alikataza ibada za sanamu?.


Jibu: Tusome,

Mwanzo 31:18 “Akachukua wanyama wake wote, na mali yake yote aliyokuwa ameyapata, na wanyama aliowapata katika Padan-aramu, ili afike kwa Isaka babaye katika nchi ya Kanaani.

19 Basi Labani alikuwa amekwenda kuwakata manyoya kondoo zake, na Raheli akaviiba vinyago vya babaye”.

Lengo la Raheli kuiba vinyago vya baba yake si kwasababu alikuwa anataka kwenda kuviabudu (yaani kuvifanya miungu yake) kama baba yake alivyofanya..

Hapana bali lengo la kufanya vile ni ili akaviharibu. Kwasababu hivyo ndio vimekuwa chanzo cha matatizo yote, (Kati ya Labani na Yakobo).

Ikumbukwe kuwa Raheli ndiye aliyekuwa mke wa ahadi wa Yakobo, na mara ya kwanza kabisa aliahidiwa kumchukua kutoka kwa Baba yake Labani, baada ya kutumika kwa miaka 7, lakini tunaona baada ya miaka hiyo ya utumishi kuisha…Yakobo hakupewa Raheli badala yake aliozwa Lea dada yake.

Mwanzo 29:25 “Ikawa, kulipokuwa asubuhi, kumbe! Ni Lea. Akamwambia Labani, Nini hii uliyonitenda?

26 Sikukutumikia kwa Raheli? Mbona umenidanganya? Labani akasema, Havitendeki hivi kwetu, kumtoa mdogo kabla ya mkubwa”

Ukiendelea kusoma mbeleni utazidi kuona visa Labani alivyokuwa anamfanyia Yakobo, mpaka Labani kufikia hatua ya kutaka kumfilisi Yakobo mali zake.

Mwanzo 31:36-42
36 Yakobo akakasirika, akagombana na Labani. Yakobo akajibu, akamwambia Labani, N’nini hatia yangu? Nayo ni nini dhambi yangu, hata ukanifuatia namna hii?

37 Umepapasa-papasa vyombo vyangu vyote; ni kitu gani ulichokiona cha nyumbani mwako? Kiweke hapa mbele ya ndugu zangu, na ndugu zako, wakaamue kati yetu.

38 Miaka hii ishirini nimekaa kwako; kondoo zako wala mbuzi zako wake hawakuharibu mimba wala waume katika wanyama wako sikuwala.

39 Kilichoraruliwa na hayawani sikukuletea, mimi mwenyewe nimetwaa hasara yake, wewe umekidai katika mkono wangu, ikiwa kilichukuliwa mchana, au ikiwa kilichukuliwa usiku.

40 Hii ilikuwa hali yangu; mchana jua likanipata, na baridi usiku, usingizi ukanitoka machoni mwangu.

41 Miaka hii ishirini nimekaa nyumbani mwako; nilikutumikia miaka kumi na minne kwa binti zako wawili, na miaka sita kwa wanyama wako, nawe umebadili mshahara wangu mara kumi.

42 Kama Mungu wa baba yangu, Mungu wa Ibrahimu na Hofu ya Isaka, hangalikuwa pamoja nami, hakika sasa ungalinifukuza mikono mitupu. Mateso yangu na kazi za mikono yangu Mungu ameziona, akakukemea usiku huu”.

Sasa kwa mambo kama hayo na mengine mengi ni wazi kuwa Raheli aliamini miungu ya baba yake ndio chanzo cha matatizo yote (Au ndiyo inayompelekesha yeye kuwa hivyo alivyo, au kutoa maamuzi anatoyatoa, ya kusumbua Yakobo).

Hivyo siku anaondoka yeye na Yakobo, Raheli aliiba ili kwamba baba yake asiitumie hiyo ikamwaribu akili na kusababisha madhara zaidi kwa Yakobo na kwake yeye Raheli. Hivyo ikawa msaada kwa Labani baba yake na Yakobo.

Hiyo ndio sababu (Ni ili amponye baba yake)..Endapobaba yake angeendelea navyo mbali na kumharibu akili, vingemsababishia kuadhibiwa na Mungu.
Kwasababu wote wanaoabudu miungu, hawafiki mbali.

Hivyo Raheli aliiba ili akaiharibu.
Ndio maana hata baada ya kuiiba alienda kuikalia (Mwanzo 31:34-35). Sasa kwa mtu mwenye lengo la kwenda kuiabudu asingeikalia, hakuna mtu anayeweza kukalia mungu wake..(hata wote wanaoabudu sanamu, huwa wanaziheshimu hizo sanamu zao)..hawawezi kuzikalia kwa lengo lolote lile.

Na baada ya hapo hatuoni, Labani akimfuatilia wala kumsumbua tena Yakobo.
Ikifundisha kuwa kuna mazingira tutawaokoa watu kwa kuwanyakua kutoka kwenye hatari..kama Raheli alivyofanya kwa Baba yake.

Yuda 1:2 “na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili”.

Maran atha

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

MTI UANGUKAPO, PAPO HAPO UTALALA.

Nifanye nini ili niishi maisha ya ushindi siku zote?

MKUU WA UZIMA AKUWEKE HURU.

HAKUNA MTU ANIONDOLEAYE, BALI MIMI NAUTOA MWENYEWE

 

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments