SWALI: Kwanini katika Mwanzo 5:2 tunasoma Mungu aliwaita Adamu na Hawa jina moja la Adamu..na sio mawili tofauti.?
Mwanzo 5:2
[2]mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.
JIBU: Kumbuka siku Mungu alipowaumba wanadamu(mwanamke na mwanamume)..hàkuwaumba wote kwa pamoja..Bali alimuumba ADAMU peke yake..kisha hawa baadaye..ambaye alikuja kuumbwa kutoka katika ubavu wa Adamu.
Hivyo wakati Mungu anatoa majina kwa viumbe vyake Hawa hakuwepo..Jina hilo alikuja kupewa na Adamu mwenyewe baadaye soma..
Mwanzo 3:20
[20]Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa; kwa kuwa yeye ndiye aliye mama yao wote walio hai.
Kwahiyo kwanini Mungu aliwaita jina moja ni kwasababu alipomuona Hawa alimuona Adamu kwasababu ni zao lake..hivyo machoni pake hakuona mwanamke anastahili kuitwa kitu kingine tofauti na jina la Mume wake ..Ni sawa na wewe uone ‘sisimizi’ huwezi wala huioni sababu ya kumuita sisimizi wa kike jina tofauti na yule wa kiume..wote utawaita tu jina moja sisimizi..na ndivyo ilivyokuwa machoni pa Mungu kwa Adamu na Hawa.
Lakini Mungu alitaka kutufundisha nini kwa kuwaita vile?
Ikiwa wewe ni mwanamke fahamu kuwa ukishaolewa, Mungu hakuoni tena kama ni mtu tofauti na mumeo. Atakutambua kwa jina lake. Hivyo jifunze kumtii mumeo. Kwasababu yeye ndio kila kitu kwako kwa muda huo.
Vilevile wewe kama mume..mpende mke wako, kwasababu ule ni ubavu wako. Na ndio maana haitwi jina lingine zaidi ya hilo la kwako. Hata kama utajaribu kumuita kwa majina mengine lakini Mungu anamtambua kwa hilo jina lako. Hivyo jifunze kumpenda na kumuhudumia.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?
Je Mungu aliumba watu wengine kabla ya Adamu?
Ahera ni wapi? Kama tunavyosoma katika biblia.
Mafundisho
Rudi nyumbani
Print this post