Waanaki ni watu gani katika biblia?

Waanaki ni watu gani katika biblia?

Waanaki ni jamii ya watu wakubwa na warefu waliotoka katika uzao wa mtu mmoja anayeitwa Anaki mtoto wa arba (Yoshua  15:13, 21:11)..Maana halisi ya jina hilo kulingana na lugha ya kuyahudi ni ‘MTU MREFU’ au ‘MWENYE SHINGO NDEFU’.

Watu hawa waliishi upande wa kusini mwa Israeli,  walikuwa ni wakubwa sana na wenye nguvu kuliko watu wengine wa kawaida walioishi ulimwenguni wakati ule.. vilevile walikuwa na nguvu kubwa za kivita, hakuna taifa lililoweza kushindana nalo.

Habari zao utazisoma sehemu nyingi sana katika biblia..lakini hivi ni baadhi ya vifungu vinavyowaelezea.

Kumbukumbu la Torati 1:28

[28]Twakwea kwenda wapi? Ndugu zetu wameiyeyusha mioyo yetu, wakituambia, Wale watu ni wengi, ni warefu kuliko sisi; miji nayo ni mikubwa, imejengewa kuta hata mbinguni; na zaidi ya hayo huko tumewaona Waanaki.

Kumbukumbu la Torati 9:1-3

[1]Sikiza, Ee Israeli; hivi leo unataka kuvuka Yordani uingie kwa kuwamiliki mataifa yaliyo makubwa, na yenye nguvu kukupita wewe, miji mikubwa iliyojengewa kuta hata mbinguni,

[2]watu wakubwa, warefu, wana wa Waanaki, uwajuao, uliokuwa ukisikia wakitajwa hivi, Ni nani awezaye kusimama mbele ya wana wa Anaki?

[3]Basi jua siku hii ya leo kuwa BWANA, Mungu wako, ndiye atanguliaye kuvuka mbele yako kama moto uteketezao; atawaangamiza, tena atawaangusha mbele yako; ndivyo utakavyowafukuza na kuwapoteza upesi, kama alivyokuambia BWANA.

Soma pia Kumbukumbu 2:11, 21, Yoshua 11:21, 22, 14:12, 15….utaona habari zao.

Sasa wayahudi kulingana na desturi zao wanaamini watu hawa chimbuko lao lilikuwa ni kutoka katika  ule uzao wa Wanefili (majitu) yaliyokuwepo kabla ya gharika kushushwa ulimwenguni (Mwanzo 6:4). Na ndio uzao ule ule uliokuja kuonekana hadi wakati wa mfalme Daudi (Yule Goliati)

Lakini kwanini Mungu aliruhusu watu hawa wawepo duniani?..kwanini asingeumba tu watu wote walingane?

Ni kuonyesha kuwa hata sasa rohoni wapo watu ambao ni majitu (wana wa anaki) karibu katika nyanja zote ya maisha..Na lengo lao ni kuweka vitisho tu na kuogopesha, lakini kama vile watu wa Mungu walivyoweza kuwashida kwa kumtegemea Bwana..vivyo hivyo na watakatifu wa sasa wanaweza kuwashinda kwa kumtegemea Bwana YESU katika mapito yao.

Unapoona mataifa makubwa yenye  nguvu kubwa yanakuja kupigana na wewe uliye taifa dogo huna haja ya kuogopa maadamu Bwana yuko pamoja na wewe.

Ikiwa watu wenye nguvu wamekuzunguka kuupinga wokovu wako..wewe kama mkristo huna haja ya kutikisika maadamu Bwana yupo upande wako.

Kumbuka alichokifanya kwa Waanaki wa Yeriko ndicho atakachokufanyia na wewe ambaye uliyemwamini Yesu Kristo. Lakini kama upo nje ya wokovu fahamu huna tumaini, twewe  utakuwa kama panzi kwa kila adui  atakayetokea mbele yako, kukupinga. Na mwisho wa siku utakuwa ni mtu wa kuchukuliwa mateka tu daima..Lakini ya nini yote hayo yakukute katika ulimwengu huu wa dhambi, ni heri ukampa Kristo maisha yako leo akuweke salama. Hizi ni siku za mwisho Yesu yupo mlangoni kurudi. Tubu dhambi zako kwa mumaanisha kuziacha umgeukie Yesu akusemehe. Kwasababu hakuna tumaini lolote nje ya Kristo.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

MUNGU HAONI SHIDA KUMUHAKIKISHIA MWOVU ULINZI.

INJILI YA MANENO LAINI ITAKUGHARIMU.

UZAO WA NYOKA.

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
fredy
fredy
1 year ago

Nashukulu mungu kwa kunipitisha kwenye hii page

apo kale inasemekana walikua watu wakubwa kama hawa wana wa Anaki ila lilipo pita ghalika inaaminika apakuachwa kiumbe isipokua tu wale walio ingia kwenye safina je
hawa akina majitu walio tokea baada ya ghalika eg: hesabu 13:31 walitokea wapi au chanzo chao nini au kipi