Nifanye nini ili niishi maisha ya ushindi siku zote?

Nifanye nini ili niishi maisha ya ushindi siku zote?

Maisha ya ushindi


Shalom,

Awali ya yote ni lazima ufahamu kuwa kupita katika majaribu, kupita katika dhiki, kupita katika mateso, haimaanishi kuwa umeshindwa, hapana hivyo vyote vinaitwa vita,..Kushindwa ni pale, vita hivyo vinapokuzidi nguvu na hatimaye kukuangusha kabisa..hapo ndio umeshindwa.

Kwasababu kama ingekuwa kila anayepitia majaribu au dhiki au shida, au bonde la mauti ni kushindwa, basi Daudi angekuwa wa kwanza, kwasababu yeye, kila kukicha alikuwa anapita katika hali ya kukimbizwa na maadui zake na hatari za kufa, mpaka wakati mwingine anakwenda kuomba msaada kutoka kwa maadui zake wengine ili tu wampe hifadhi kwa muda. Lakini katika yote alikuwa na uhakika kuwa maisha yake ni ya ushindi tu..mpaka akaandika katika Zaburi 23 “Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu…. Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji”. (Zab 23)

Na kweli kama tunavyojua mwisho wa siku aliibuka mshindi, na kuwa mfalme wa Israeli, na mpaka sasa habari zake tunazisoma,

Hata Bwana wetu Yesu,vivyo hivyo alijaribiwa kama sisi tulivyojaribiwa, hata zaidi ya sisi lakini katika majaribu yake yote, hakuwahi kushindwa na hata moja, wala hakuwahi kutenda dhambi.. Na ndio maana akatuambia..

Yohana 16:33 “Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu”.

Unaona? Na watakatifu wengine wote kwenye biblia hivyo hivyo..

Lakini siri ya ushindi wao ilikuwa ni nini?

Je ni nguvu zao? Au bidii zao? Au ni nini.. Biblia imeshatoa jibu na kusema, mtu anayeweza kuushinda ulimwengu,(kuishi maisha ya ushindi) ni mtu Yule ambaye amezaliwa na Mungu tu.

1Yohana 5:4 “Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu”.

Unaona?, Ni mtu tu aliyezaliwa na Mungu ndio anapokea uwezo huo wa kuushinda ulimwengu, si mtu mwingine yeyote, nguvu za mtu binafsi haziwezi, bidii za mtu haziwezi, fedha ya mtu haiwezi, wala kipaji cha mtu hakiwezi kuushinda ulimwengu.

Huwezi kumshinda shetani atakapokuletea majaribu kama hujazaliwa na Mungu (yaani hujazaliwa mara ya pili), haiwezekani kuushinda uzinzi, haiwezekani kuishinda dhambi ile inayokusumbua, ni ngumu kuwashinda wachawi na mapepo, vilevile ni ngumu kuishi maisha ya amani na furaha hapa duniani.

Kwasababu Mungu anakuwa hayupo upande wako kukutia nguvu..Lakini wale ambao Mungu yupo ndani yao..biblia inasema hivi.

Warumi 8:31 “Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?

32 Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?

33 Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.

34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.

35 Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga”?

Kwa mtu aliyezaliwa mara ya pili kunakuwa na nguvu Fulani ya ajabu kutoka kwa Mungu inayomlinda asitetereke pindi unapopitia majaribu mazito ulimwenguni.

Hivyo ukiwa kama hujaokoka, au ulikuwa upo nusu nusu, (yaani mguu mmoja nje,mwingine ndani) na ndio maana maisha yako yamekuwa ni ya kushindwa kudumu katika wokovu, ya kushindwa kusimama, ya kushindwa kuwa na mahusiano mazuri na Mungu. Basi leo hii fanya uamuzi thabiti wa kumpa Yesu maisha yako upya kwa kumaanisha kabisa.

1Yohana 1:9 “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote”.

Kama upo tayari kumruhusu Yesu ayaunde upya maisha yako, basi uamuzi huo ni wa busara, sana, fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba. Na pia kama unahitaji kubatizwa pia usisite kuwasiliana nasi .>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Ikiwa umefungua na kufuata hayo maelekezo hapo juu, basi mpaka hapo tayari ushindi wa kwanza umepata wa mauti..

1Wakorintho 15:55 “Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako?

Vilevile wachawi na mapepo hawatakuweza, kwa lolote..

Kuanzia huo  wakati utakapobatizwa na kuendelea utaanza kuona mabadiliko ya tofauti katika maisha yako,.Sina mengi ya kusema, wewe mwenyewe utayashuhudia.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye  namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

HIZI NI NYAKATI ZA KUJIINGIZA KWA NGUVU.

OLE WAO WANAOJITAHIDI KUMFICHA BWANA MASHAURI YAO.

DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?

KUZIMU NI WAPI

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments