YAKUTI NI MADINI GANI?

YAKUTI NI MADINI GANI?

Yakuti ni aina ya madini inayokaribiana kufanana sana na madini ya Rubi (yaani Marijani).

Madini ya Yakuti kwa lugha ya kiingereza ndio yanajulikana kama SAPPHIRE. Kazi yake ni kutengenezea vito bya thamani kama pete, saa za mkononi n.k, na thamani yake inakaribiana kufanana na ile ya madini ya Rubi, na yana muonekano mzuri sana.

Madini ya Yakuti yapo ya aina mbili, yapo Yakuti ya manjano na Yakuti ya Samawi (yaani blue).

Katika biblia Yakuti ya manjano imetajwa katika mistari kadhaa..

Ayubu 28:19 “Yakuti ya rangi ya manjano ya Kushi haitasawazishwa nayo, Wala haitatiwa kima kwa dhahabu safi”.

Unaweza pia kusoma juu ya Yakuti hiyo ya manjano katika Kutoka 28:17, na Ezekieli 28:13.

Kadhalika unaweza kusoma juu ya Yakuti-Samawi katika mistari ifuatayo.. Kutoka 28:18, Kutoka 39:11 na Isaya 54:11.

Hivyo Kwaufupi madini haya kwenye biblia yametumika kuwakilisha vitu visafi na vitukufu, na vyenye heshima, kwamfano utaona kile kiti cha enzi cha Mungu, Nabii Ezekieli alichooneshwa kilikuwa ni mfano wa Yakuti-Samawi.

Ezekieli 10:1 “Ndipo nikaangalia, na tazama, katika anga lililokuwa juu ya vichwa vya makerubi, kulionekana juu yao kana kwamba ni yakuti samawi, kuonekana kama mfano wa kiti cha enzi”.

Halikadhalika katika ule mji Yerusalemu mpya, utakaoshuka kutoka mbinguni, maandiko yanasema utakuwa umepambwa kwa vito vya thamani, vya mfano Yakuti.

Ufunuo 21:19 “Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi;

20 wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto”.

Kama vile tunavyoona madini ya Yakuti yalivyo mazuri, basi mbinguni kuna mazuri zaidi ya hayo tuliyoandaliwa, biblia imetaja tu Yakuti ili tuweze kuelewa na kutengeneza picha uzuri wa kule, lakini kiuhalisia vito vilivopo kule sio vya kidunia.

Mji ule Yerusalemu mpya ni mzuri sana, tujitahidi tuuingia,na tunauingia kwa kuishi maisha ya wokovu kwa uaminifu wote.

Ufunuo wa Yohana 22:14 “Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake”.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Risasi inayotajwa kwenye Ezekieli 27:12 ni ya namna gani?

NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.

KWA HIYO NDUGU, VUMILIENI, HATA KUJA KWAKE BWANA.

HEKIMA YA KIMUNGU, INAINGIAJE MIOYONI MWETU?

KWA HIYO NDUGU, VUMILIENI, HATA KUJA KWAKE BWANA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments