Kwa namna gani mauti hufanya kazi ndani yetu na uzima kwa wengine? (2Wakorintho 4:12).

Kwa namna gani mauti hufanya kazi ndani yetu na uzima kwa wengine? (2Wakorintho 4:12).

Tusome,

2 Wakorintho 4:12 “Basi hapo mauti hufanya kazi ndani yetu, bali uzima ndani yenu”.

Ili tuelewe vizuri, tuchukue mfano wa kondoo anayepelekwa machinjoni, yeye ndani yake ipo MAUTI kwasababu dakika chache mbele anaenda kufa, lakini sisi kwetu ni UZIMA kwasababu, anageuka kuwa chakula kinachotupa uzima wa miili yetu.

Hivyo ni sawa na kusema, mauti inafanya kazi ndani ya huyo kondoo na Uzima ndani yetu sisi tunaomla.

Kadhalika maandiko yanawafananisha watumishi wa Mungu kama Kondoo, na wa kwanza kabisa kufananishwa na kondoo ni mkuu wa Uzima Yesu Kristo.

Isaya 53:7 “Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake”.

Huyo ni Bwana Yesu ambaye kwa kupitia mateso ya Mauti aliyoyapitia pale Kalvari, sisi tumepata uzima, pasipo yeye kuchubuliwa sisi tusingepata wokovu, pasipo yeye kuudhiwa sisi tusingepata ukombozi n.k

Isaya 53:5 “Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona”.

Hivyo sisi wakristo tunapopitia mateso wakati wa kuipeleka injili, ili watu wengine waokoke, hapo Mauti inafanya kazi ndani yetu lakini UZIMA ndani ya wale tunaowahubiria. Sisi tunataabika ili wao waupokee wokovu, sisi tunatukanwa ili neno la UZIMA liwafikie wengine.

Warumi 8:36 “Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa”.

Hivyo kwa hitimisho ni kwamba hatuna budi sisi wote tuliookoka kujitoa na kukubali dhiki, uzia, shida na hata kukubali kuutoa uhai ili wengine wapate uzima wa milele kama tulivyoupata sisi.

Jambo hilo lina baraka kubwa sana.

1 Yohana 3:16 “Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu”.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Noeli ni nini, na je! Neno hili linapatikana katika biblia?

DHAMBI YA MAUTI

Je ushabiki wa mpira ni dhambi?

Noeli ni nini, na je! Neno hili linapatikana katika biblia?

SISI NI WINDO BORA SANA, LA DHAMBI.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments