MUNGU ALIVICHAGUA VITU AMBAVYO HAVIKO.

MUNGU ALIVICHAGUA VITU AMBAVYO HAVIKO.

Nakusalimu katika jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo, ukuu na uweza vina yeye milele na milele. Amina.

Mtume Paulo aliandika, ANGALIENI MWITO WENU, Akiwa na maana, kwamba tunapaswa tuwe na ufahamu tosha juu ya wito wa Mungu katika Maisha yetu jinsi unavyokuja. Tofauti na tunavyodhani kuwa Mungu akikuuita, ni mpaka uwe shupavu au hodari Fulani. Mpaka uwe na miguu miwili, mpaka uwe na digrii Fulani ya dini, mpaka uwe na kipato Fulani au familia nzuri, mpaka uwe na kipaji Fulani cha kitofauti, Hapana..

Bali yeye huwa anakwenda kinyume chake..Tunalithibitisha hilo katika vifungu hivi;

1Wakorintho 1:26 “Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa;

27 bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;

28 tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, VITU AMBAVYO HAVIKO, ili avibatilishe vile vilivyoko;

29 mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu”.

Bwana anasema, anavichagua vitu ambavyo haviko, akiwa na maana sio kwamba haviko kabisa ulimwenguni, hapana, bali uwepo wake, ni kama tu vile haviko. Kwamfano nikija na kukutajia nchi kama “Marekani” au “Ufaransa” ni wazi kuwa ulishawahi kuzisikia mahali Fulani nchi hizi, kwasababu kila siku zinatajwa aidha katika vyombo vya Habari au midomoni mwa watu, Lakini nikikutajia nchi kama “Tuvalu” au “Kiribati” pengine leo ndio inaweza ikawa mara yako ya kwanza kuzisikia hizi nchi, Ni kama vile hazipo duniani sio ndio!. Lakini ni nchi ambazo zipo, na zinamfumo huru unaojiendesha kama tu vile nchi yako.

Vivyo hivyo, wito wa Mungu, unachagua, watu ambao “hawapo” yaani wasiojulikana, wasiosikika hata katika masikio ya watu, waliosahaulika zamani, kama vile Daudi, alivyoitwa hao akiwa huko maporini, ndio jicho la Mungu linawatazama sana, ili awatumie.

Pengine umekata tamaa, au unajidharau, au unajiona wewe si kitu, huna elimu yoyote, huna uzuri, huna ujuzi, upo upo tu, huna marafiki wengi, huwezi kujichanganya sana, pengine ni mlemavu, au ni mzito wa kutenda,.

Nataka nikuambie, wito wa Mungu upo karibu sana na wewe kuliko unavyodhani, kuliko kwa watu wenye nguvu, ikiwa tu, utakubali kujisogeza karibu na yeye. Wengi wa Mitume wa Kristo walikuwa hawana elimu yoyote biblia inasema hivyo katika ( Matendo 4:13), walikuwa ni wavuvi tu, lakini walipoitwa na Mungu, walitii na kumfuata kwa ukamilifu wote, bila kuwa na mawazo mawili mawili. Na ndio hao Mungu aliwatumia kwa viwango vya juu mpaka, tunawaita mababa wa Imani.

Na sisi pia, tusione madhaifu yetu, au unyonge wetu, kama ndio sababu ya kutomtumikia Mungu, kinyume chake, ndio tumtafute kwa bidii kwasababu katika hali hizo wito wake ndio mkubwa kushinda pale tunapokuwa na nguvu.

Udhaifu wowote, tuunaona ndani yetu, ndio uweza wa Mungu unapotimilikia hapo.

2Wakorintho 12:9 “Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.

10 Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu”.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Amri zilizo ndogo alizozizungumzia Yesu ni zipi?

Chuo cha vita vya Bwana ni kipi?(Hesabu 21:14)

JE WEWE NI LAZARO YUPI, WA KWANZA AU WA PILI?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments