Tarshishi ni mji uliokuwepo nchi ijulikanayo kwasasa kama Lebanoni. Taifa la Lebanoni katika nyakati za kale ndio Taifa lililokuwa linaongoza kwa uzalishaji wa miti aina ya MIEREZI (Kujua Mierezi ni miti gani fungua hapa >> MIEREZI).
Mji mkuu wa Taifa la Lebanoni, ndio ulikuwa Tarshishi. Mji huu wa Tarshishi ndio uliokuwa unaongoza kwa wafanya biashara, na ndio uliokuwa kitovu cha biashara ulimwenguni. Nabii Yona alikimbilia mji huu kwasababu ulikuwa na fursa nyingi. (Kwa urefu juu ya mji wa Tarshishi na biashara zake na Taifa hilo linafunua nini kiroho, fungua hapa >>Tarshishi).
Asili ya mji wa Tarshishi ni mwana wa Yafethi aliyeitwa Yavani, ambaye huyu Yavani ndiye aliyewazaa wenyeji wa Tarshishi.
Mwanzo 10:1 “Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika. 2 Wana wa Yafethi ni Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi. 3 Na wana wa Gomeri ni Ashkenazi, na Rifathi, na Togama. 4 NA WANA WA YAVANI NI ELISHA, TARSHISHI, Kitimu, na Warodani”.
Mwanzo 10:1 “Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika.
2 Wana wa Yafethi ni Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi.
3 Na wana wa Gomeri ni Ashkenazi, na Rifathi, na Togama.
4 NA WANA WA YAVANI NI ELISHA, TARSHISHI, Kitimu, na Warodani”.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Ninawi ni nchi gani kwasasa?
Ashuru ni nchi gani kwa sasa?
MADHARA YA KUFUATA MAMBO YAKO TU!
Je Elisha alimdanganya Ben-hadadi kuwa hatakufa kwa ugonjwa wake?
BASI, IWENI NA HURUMA, KAMA BABA YENU ALIVYO NA HURUMA
Rudi nyumbani
Print this post