Mshipi wa dhahabu matitini ni nini?.

Mshipi wa dhahabu matitini ni nini?.

Mshipi ni nini? na Ule mshipi wa dhahabu matitini ni nini?, na je! Yule Yohana aliyemwona ni mwanamke?, kama sio kwanini pametaja matiti?.


Jibu: Tusome,

Ufunuo 1:13 “na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa MSHIPI WA DHAHABU MATITINI”.

Tafsiri ya “Mshipi” ni mkanda. Unaweza kusoma pia Mathayo 3:4, na Matendo 21:11, na Zaburi 18:32 utaona jambo hilo hilo. Na mkanda huo unaweza kuwa umetengenezwa kwa malighafi yoyote, aidha kwa Ngozi, au kitambaa kigumu. Lakini lengo la mshipi, ni kubana sehemu ya kiuno au kifua.

Sasa Huyo Mtume Yohana aliyemwona katika maono, hakuwa mwanamke, bali alikuwa ni mwanaume, ambaye ni BWANA YESU KRISTO, Ndio maana ukiendelea mbele kidogo, utaona anajitambulisha..

Ufunuo 1:17 “Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,

18 NA ALIYE HAI; NAMI NALIKUWA NIMEKUFA, NA TAZAMA, NI HAI HATA MILELE NA MILELE. NAMI NINAZO FUNGUO ZA MAUTI, NA ZA KUZIMU”.

Na kama tunavyojua mwenye funguo za mauti na kuzimu, na aliyekuwa amekufa na sasa yu hai, si mwingine Zaidi ya Bwana Yesu Kristo. Kwahiyo huyo bila shaka yoyote alikuwa ni Mkuu wa Uzima, Yesu Kristo mwenyewe.

Lakini ni kwanini biblia iseme alikuwa amevikwa mshipi matitini na si kifuani?

Ni kuonyesha tu eneo la mwili ambalo “Mshipi huo umefungwa”.. (kwamba ni eneo la kifua, ambalo ndio eneno la matiti kwa maumbile ya wanawake), lakini sio kwamba kwa Kutaja matiti kunamaanisha kuwa ana matiti, hapana!.. biblia kumtaja Bwana Yesu kama Mwanakondoo, haimaanishi Bwana anayo maumbile kama ya kondoo, au uso wa kondoo. Ni lugha tu!, ambayo inaujumbe Fulani katika roho.

Lakini swali la msingi la kujiuliza ni kwanini asionekane kavaa tu vazi lililofika tu miguuni, lakini avae lililofungwa na mshipi?

Kama tulivyotangulia kujifunza, kuwa mshipi unafungwa aidha kiunoni au kifuani.. Bwana Yesu anaon ekana kalijifunga kifuani, Yohana Mbatizaji alijifunga kiunoni.

Mathayo 3:4 “Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na MSHIPI WA NGOZI kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu”.

Na sisi hatuna budi kujifunga mishipi, viunoni mwetu, na Mshipi huo si mwingine Zaidi ya KWELI YA NENO LA MUNGU.

Waefeso 6:13 “Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.

14 Basi simameni, HALI MMEJIFUNGA KWELI VIUNONI, na kuvaa dirii ya haki kifuani”

Tunapojivika utakatifu ambalo ndilo vazi letu refu lifikalo miguuni, (Ufunuo 19:8), na tunapojifunga KWELI YA NENO LA MUNGU KATIKA VIUNO VYA ROHO ZETU, hapo tunakuwa wakamilifu mbele za Mungu, na tunaweza kusimama, kushindana na uovu.

Je Umejifunga Neno la Mungu leo?,

Mfano wa Neno la Mungu ni hili..

1Yohana 2:15 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake”.

Na hili..

Mathayo 22:37 “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote”.

Je Wewe ni Rafiki wa dunia?, kama ndio basi Neno la Mungu hujalifunga kiunoni mwako, na hivyo upo katika hatari,  lifunge leo Neno la Uzima kiunoni mwako, ili uweze kusimama na kushinda katika siku za uovu.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

Kwanini biblia inaitaja mara kwa mara dhahabu ya Ofiri?

Fuawe ni nini? Kama tunavyosoma katika Isaya 41:7

ONDOA TAKATAKA KATIKA FEDHA, NA CHOMBO KITATOKEA KWA MTAKASAJI.

VAZI LA YESU HALIGAWANYWI.

Risasi inayotajwa kwenye Ezekieli 27:12 ni ya namna gani?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Emmanuel Kitengule
Emmanuel Kitengule
2 years ago

Amina mwalimu.