Milima ya Ararati ipo wapi kwasasa? (Mwanzo 8:4)

Milima ya Ararati ipo wapi kwasasa? (Mwanzo 8:4)

Milima ya Ararati, mahali ambapo Safina ya Nuhu ilitua, ipo wapi kwasasa?

JIbu: Tusome,

Mwanzo 8:4 “Mwezi wa saba, siku ya kumi na saba ya mwezi, safina ikatua juu ya MILIMA YA ARARATI.”.

Milima ya Ararati, ipo katika Nchi ya UTURUKI ya sasa, (Mashariki mwa Uturuki).Tazama picha juu.. Milima hiyo mpaka leo ipo, na watu wanaitembelea.

Eneo la Mashariki ya nchi ya Uturuki, zamani lilikuwa linajulikana kama Ararati.  Utaona kwenye biblia limetajwa mara kadhaa…

2Wafalme 19:37 “Ikawa, alipokuwa akiabudu nyumbani mwa Nisroki, mungu wake, Adrameleki na Shareza wakampiga kwa upanga; wakaikimbilia NCHI YA ARARATI. Na Esar-hadoni mwanawe akatawala mahali pake.”

Pia katika Kitabu cha Isaya na Yeremia, Ufalme wa Ararati umetajwa.

Isaya 37:38 “Ikawa alipokuwa akiabudu katika nyumba ya Nisroki, mungu wake, Adrameleki na Shareza, wanawe, wakampiga kwa upanga; wakakimbilia NCHI YA ARARATI; naye Esar-hadoni, mwanawe, akamiliki badala yake”.

Na

Yeremia 51:27 “Itwekeni bendera katika nchi, pigeni tarumbeta kati ya mataifa, yawekeni mataifa tayari juu yake; ziiteni juu yake FALME ZA ARARATI, na Mini, na Ashkenazi; agizeni jemadari juu yake; wapandisheni farasi, kama tunutu”.

Lakini swali ni je!.. Kuna kitu chochote cha kiungu katika hiyo milima sasa? Kiasi kwamba tukienda kutembea katika milima hiyo, tutaongeza chochote cha kiungu ndani yetu?

Jibu ni la!.

Milima hiyo haina chochote cha kiungu leo, kiasi kwamba labda tukienda kule kuna chochote tutafaidika nacho.

Lakini pako mahali ambapo tukienda leo basi tutamwona Mungu..na mahali penyewe Bwana Yesu alipataja katika mistari ifuatayo..

Yohana 4:20 “BABA ZETU WALIABUDU KATIKA MLIMA HUU, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia.

21 Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu.

22 Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.

23 LAKINI SAA INAKUJA, NAYO SASA IPO, AMBAYO WAABUDUO HALISI WATAMWABUDU BABA KATIKA ROHO NA KWELI. KWA MAANA BABA AWATAFUTA WATU KAMA HAO WAMWABUDU

24 MUNGU NI ROHO, NAO WAMWABUDUO YEYE IMEWAPASA KUMWABUDU KATIKA ROHO NA KWELI”.

Umeona?

Ni lazima tumwabudu baba katika ROHO NA KWELI, na maana ya kumwabudu Bwana katika roho na kweli, sasa nini maana ya kumwabudu Baba katika roho na  kweli? Fungua hapa >>Nini maana ya kumwabudu Mungu katika Roho na kweli?

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

JIHADHARI NA ROHO ZIDANGANYAZO.

Mlima Gerizimu na Ebali ni ipi, na umuhimu wao rohoni ni upi?

Mwandamo wa mwezi/Mwezi mpya Ni nini kibiblia?

Kisiwa cha Patmo kipo nchi gani?.

Je! kuna sikukuu za pasaka mbili? (Hesabu 9:11)

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments