SWALI: Mstari huu una maana gani? Je, ni kweli waandishi waliweza kubadilisha baadhi ya maneno ya torati, Na hivyo inaifanya biblia isiamike hadi sasa?
Yeremia 8:8 “Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya Bwana tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.
JIBU: Hii ni hoja inayotumiwa sana na wapinga-biblia, au wapinga-ukristo. Wakisimamia mstari huu, na kusema, unaona? Biblia ilichakachuliwa, zamani na waandishi wa kiyahudi kwa kuongeza baadhi ya maneno katika torati iliyoandikwa na mwenyezi Mungu,.. Kwahiyo hiyo inathibitisha kuwa biblia ni kitabu chenye kasoro..
Lakini je tukisoma vifungu hivyo, vinatuambia waliibadilisha torati?
Kabla ya kuendelea kusoma zaidi, embu tuitafakari tena hiyo kauli hapo mwishoni, anasema “kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo”. Ahaa Kumbe waandishi ndio wameifanya kuwa uongo..Lakini yenyewe kama yenyewe sio uongo.. Mfano nikikuambia, unanifanya kuwa mwongo mbele za ndugu zangu, haimaanishi kuwa mimi ni mwongo..maana yake ni kuwa, pengine ni kwasababu uliyawakilisha maneno yangu isivyopaswa, aidha kwa kuongeza chumvi au kupunguza, na kwasababu hiyo basi, mimi nikaonekana nimeongopa, lakini sivyo, mimi nilisema ukweli mwanzo, isipokuwa wewe ndio umeniwakilisha vibaya.
Ndivyo ilivyokuwa hapo, waandishi, ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kufundisha na kuwaelezea watu, walianza, kutoa tafsiri zisizo sawa za torati, na kuwafundisha watu na kuwaandikia, mfano Bwana Yesu alisema, waliipindua amri ya tano; inayosema waheshimu baba yako na mama yako, na kuwaambia watu, ikiwa kuna chochote umekiweka wakfu hupaswi kumsaidia mzazi wako, hata kama akiangamia kwa njaa ni sawa tu..Jambo ambalo Mungu hakuliagiza hata kidogo, ilikuwa ni wajibu wa kila mtu kumsaidia mzazi wake, awapo katika uhitaji (Soma Marko 7:7-13)
Umeona, sasa tukirudi kwenye ile habari ya mwanzo ili kuthibitisha hilo vizuri, ukiendelea kusoma vifungu vinavyofuata utaona Yeremia, anaeleza kwa undani jinsi kalamu za hao waandishi zilivyoweza kuipa torati tafsiri zisizo sahihi..
Yeremia 8:8 “Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya Bwana tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo. 9 Wenye hekima wametahayari, wamefadhaika na kushikwa; tazama, wamelikataa neno la Bwana, wana akili gani ndani yao? 10 Basi, kwa hiyo nitawapa watu wengine wake zao na mashamba yao nitawapa wale watakaowamiliki; MAANA KILA MMOJA WAO, TANGU ALIYE MDOGO HATA ALIYE MKUBWA, NI MTAMANIFU; TANGU NABII HATA KUHANI, KILA MMOJA HUTENDA MAMBO YA UDANGANYIFU. 11 KWA MAANA WAMEIPONYA JERAHA YA BINTI YA WATU WANGU KWA JUU-JUU TU, WAKISEMA, AMANI, AMANI, WALA HAPANA AMANI. 12 Je! Walitahayarika, walipokuwa wametenda machukizo? La! Hawakutahayarika, wala hawakuweza kuona haya usoni; basi wataanguka miongoni mwao waangukao; wakati wa kujiliwa kwao wataangushwa chini, asema Bwana..
9 Wenye hekima wametahayari, wamefadhaika na kushikwa; tazama, wamelikataa neno la Bwana, wana akili gani ndani yao?
10 Basi, kwa hiyo nitawapa watu wengine wake zao na mashamba yao nitawapa wale watakaowamiliki; MAANA KILA MMOJA WAO, TANGU ALIYE MDOGO HATA ALIYE MKUBWA, NI MTAMANIFU; TANGU NABII HATA KUHANI, KILA MMOJA HUTENDA MAMBO YA UDANGANYIFU.
11 KWA MAANA WAMEIPONYA JERAHA YA BINTI YA WATU WANGU KWA JUU-JUU TU, WAKISEMA, AMANI, AMANI, WALA HAPANA AMANI.
12 Je! Walitahayarika, walipokuwa wametenda machukizo? La! Hawakutahayarika, wala hawakuweza kuona haya usoni; basi wataanguka miongoni mwao waangukao; wakati wa kujiliwa kwao wataangushwa chini, asema Bwana..
Umeona hapo? Anasema, hao waandishi na makuhani, wanawatabiria watu amani, amani, na kuwaambia mnaishi sawasawa na torati ya Mungu inavyosema, hivyo hamwezi kupatwa na madhara, ili hali ndani yao wanatamani, ni waovu, waabudu masanamu, wanakula rushwa n.k..
Wakati torati inakataza vikali vitu hivyo, wenyewe wanawatumainisha watu, Mungu anawapenda, ndio hapo anasema, wanawaponya jeraha zao kwa juu juu tu, mwisho wa siku wanaadhibiwa, halafu wanasema Mungu ni mwongo.. Mbona anatupiga bila sababu!.
Je! Waandishi wa namna hii wapo hadi sasa?
Jambo hili lipo hadi sasa katika kanisa la Mungu, Siku hizi za mwisho makristo na manabii wengi sana wa uongo wametokea, nao wanawaponya watu wa Mungu juu juu tu, hawawaelezi ukweli, mpaka inafikia hatua Mungu anaonekana mwongo, hasikii wala hajibu.
Wanawaambia, utafanikiwa, utabarikiwa, kesho yako ni ya kung’ara kama jua, wanawaambia watoe sadaka nyingi, watumie maji ya upako, mafuta na chumvi, wakati mwingine wafunge mwaka mzima, Mungu atawabariki.. Lakini wanasahau kuwa hao watu wana mizigo ya dhambi, ndiyo inayowafanya wasijibiwe maombi yao.. Kama vile maandiko yanavyosema..
Isaya 59:1 “Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.3 Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong’ona ubaya”.
Isaya 59:1 “Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;
2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.
3 Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong’ona ubaya”.
Hivyo hao watu wanataabika, januari mpaka disemba, lakini hawaona nuru yoyote, hawaona uzima wowote, ndio kwanza hali inakuwa mbaya, mwishoni wanakataa tamaa wanasema Mungu hajibu maombi, wanawageukia waganga wa kienyeji.
Ndugu, Neno la Mungu ni kweli kabisa, akisema atakuponya, atakuponya kweli, akisema atakubariki atakubariki kweli, lakini ni sharti ujue, anataka nini kwanza kwako ili hivyo vyote vikujie.. Anachotaka ni wewe uache dhambi, uache, rushwa, uache uzinzi, uache uongo, uache vimini, uache fashion za kidunia, anasa, uache ulevi, uwe mtakatifu. Ndipo hayo yote yatakapokujia..
Epuka injili zizisogusia dhambi katika maisha yako, ziepuke kama ukoma, hizo huwa zinakuja na maneno mazuri sana ya kushawishi na kufariji, lakini hazitakusaidia chochote, Mungu ni mtakatifu, kamwe hajibu maombi ya mwenye dhambi.
Je! Umeokoka? Kweli kweli kwa kumaanisha kumfuata Kristo? Kama la! Basi huu ndio wakati wako sasa kuanza upya na Kristo. Ikiwa upo tayari kufanya hivyo, basi, waweza tupigia kwa namba uzionaza hapo chini.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
MAJIBU YA MASWALI YANAYOULIZWA NA WASIO WAKRISTO (Sehemu ya kwanza).
Je!Sisi kama wakristo Tunaruhusiwa kuchangia ujenzi wa Imani nyingine?
Yesu ni Mungu?, Na Kama ni Mungu kwanini alikufa?
Nini maana ya “Torati na manabii”?
Neno “Mashehe” tunaliona likitajwa katika biblia(Agano la kale); Hawa mashehe ni wakina nani?
Je! Karamu za ‘Idi’ ndio zipo hizo tunazozisoma katika Hosea (12:9)
KUONGOZWA SALA YA TOBA
Rudi nyumbani
Print this post
Amen! Amen! Amen!. Mungu akubariki sana mwana wingu,mtu wangu wandani ananona kwa sababu anakula chakula chaukweli kutoka kwenu,pia ningependa kujua kama kuna website ninaweza kutumia kudownload mafundisho yenu kwa audio.
Amina ashukuriwe Bwana kwa hilo…
Tuna youtube channel yetu…inaitwa wingu la mashahidi wa Kristo. Kuna baadhi ya masomo kwa njia ya video na audio..