Swali: Katika 1Samweli 17:49, tunasoma kuwa ni Daudi ndiye aliyemwua Goliathi, lakini katika 2Samweli 21:19, tunaona biblia inamtaja mtu mwingine kabisa aliyeitwa Elhanani kuwa ndiye aliyemwua Goliathi, je kiuhalisia ni yupi aliyemwangusha Goliath kati ya hao wawili?
Jibu: Tusome,
1Samweli 11: 49 “Daudi akatia mkono wake mfukoni, akatwaa humo jiwe moja, akalitupa kwa kombeo lake, akampiga Mfilisti katika kipaji cha uso; jiwe hilo likamwingilia kipajini, akaanguka chini kifudifudi. 50 Hivyo Daudi akamshinda yule Mfilisti kwa kombeo na jiwe, akampiga Mfilisti, akamwua; walakini Daudi hakuwa na upanga mkononi mwake”
1Samweli 11: 49 “Daudi akatia mkono wake mfukoni, akatwaa humo jiwe moja, akalitupa kwa kombeo lake, akampiga Mfilisti katika kipaji cha uso; jiwe hilo likamwingilia kipajini, akaanguka chini kifudifudi.
50 Hivyo Daudi akamshinda yule Mfilisti kwa kombeo na jiwe, akampiga Mfilisti, akamwua; walakini Daudi hakuwa na upanga mkononi mwake”
Tusome tena..
2Samweli 21:19 “Kulikuwa na vita tena na Wafilisti huko Gobu; na Elhanani, mwana wa Yairi, Mbethlehemi, ALIMWUA GOLIATHI, MGITI, ambaye mti wa mkuki wake ulikuwa kama mti wa mfumaji. 20 Kulikuwa na vita tena huko Gathi; ambako kulikuwa na mtu mrefu sana, mwenye vidole sita katika kila mkono, na vidole sita katika kila mguu, jumla yake ishirini na vinne; yeye naye alizaliwa kwa Mrefai”.
2Samweli 21:19 “Kulikuwa na vita tena na Wafilisti huko Gobu; na Elhanani, mwana wa Yairi, Mbethlehemi, ALIMWUA GOLIATHI, MGITI, ambaye mti wa mkuki wake ulikuwa kama mti wa mfumaji.
20 Kulikuwa na vita tena huko Gathi; ambako kulikuwa na mtu mrefu sana, mwenye vidole sita katika kila mkono, na vidole sita katika kila mguu, jumla yake ishirini na vinne; yeye naye alizaliwa kwa Mrefai”.
Goliathi halikuwa jina la mtu mmoja maalumu, kwamba hakuna mtu mwingine kabla ya hapo, au baada ya hapo aliyeitwa kwa jina hilo, bali lilikuwa ni jina ambalo watu wengi walikuwa wanalitumia/wanaitwa, kwahiyo huyu Goliathi aliyeuawa na Daudi ni tofauti na huyu aliyeuawa na Elhanani.. Ingawa wote wana majina yanayofanana na sifa zinazofanana.. Ni kama tu Yohana Mbatizaji na Yohana Mwanafunzi wa Yesu, walivyokuwa na majina yanayofanana na utumishi unaokaribia kufanana lakini ni watu wawili tofauti.
Kwahiyo hawa ni watu wawili tofauti wenye majina yanayofanana..Ndio maana utaona hapo kwa huyu Elhanani ni vita vingine kabisa, ambavyo tayari Daudi alikuwa ameshakuwa mfalme…” 2Samweli 21:19 “Kulikuwa na vita tena na Wafilisti huko Gobu; na Elhanani, mwana wa Yairi, Mbethlehemi, ALIMWUA GOLIATHI, MGITI, ambaye mti wa mkuki wake ulikuwa kama mti wa mfumaji”.
Sasa ili kujua ni nini tunaweza kujifunza kwa huyu shujaa Elhanani aliyemwua Goliathi, pamoja na mashujaa wengine wa Daudi (idadi yao 37) ambao walioangusha majitu kama alivyofanya Daudi.. basi unaweza kufungua hapa >>>LIPO LA KUJIFUNZA KWA WALE MASHUJAA 37 WA DAUDI.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
NI MAONO YAPI HAYO UNAYOSUBIRIA?
VITA DHIDI YA MAADUI
Je! ile habari ya watu wawili wenye pepo inajichanganya?
Je! kuna sikukuu za pasaka mbili? (Hesabu 9:11)
Je mwanamke Fibi, alikuwa ni askofu wa makanisa, kama mitume?
Rudi nyumbani
Print this post