Biblia inasema Bwana Yesu alifundisha kwa mifano. Naomba kuelewa hiyo mifano ni nini? Na dhumuni lake lilikuwa ni lipi?
Mifano, ni hadithi zinazoambatanishwa na habari husika, ili kueleza uhalisia zaidi wa ukweli huo.
Bwana Yesu alitumia mfumo huu, wa hadithi za kidunia ili kueleza uhalisia wa mambo ya ufalme wa mbinguni. Na takribani mafundisho yake yote yalitegemea mifano.
Mathayo 13:34 “Hayo yote Yesu aliwaambia makutano kwa mifano; wala pasipo mfano hakuwaambia neno;35 ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema, Nitafumbua kinywa changu kwa mifano, Nitayatamka yaliyositirika tangu awali”.
Mathayo 13:34 “Hayo yote Yesu aliwaambia makutano kwa mifano; wala pasipo mfano hakuwaambia neno;
35 ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema, Nitafumbua kinywa changu kwa mifano, Nitayatamka yaliyositirika tangu awali”.
Mpaka ikafikia wakati Fulani wanafunzi wake wanamuuliza kwanini unapenda kutumia mifano kufundisha watu?(Mathayo 13:10)
Kwamfano alipotaka kueleza habari ya madhara ya kutokusamehe, alitumia hadithi ya yule mtu aliyedaiwa talanta elfu kumi, ambaye alikuwa karibuni na kuuzwa kwa kukosa cha kulipa, lakini bwana wake akamuhurumia akamsemehe deni lote, lakini yeye alipokutana na mtumwa wake aliyemdai dinari 100 tu hakutaka kumsamehe, matokeo yake bwana wake aliposikia tabia yake hiyo akamkamata na kumtupa gerezani, mpaka na yeye atakapolipa yote(Mathayo 18:21-35).
Hivyo mtu unaposikia hadithi hiyo, inakupelekea kuelewa zaidi jinsi Mungu naye anavyojisikia pale tunaposhindwa kuwasamehe watu makosa yao .
Katika Biblia ni mifano zaidi ya 30 Bwana Yesu aliisema, lakini ni mingi zaidi ya hiyo aliifundisha, ambayo haijaandikwa kwenye biblia, (Yohana 21:25)
Madhumuni na mifano hiyo yalikuwa ni mawili:
Bwana Yesu alipoizungumza kwa waliokuwa na kiu ya kusikia, aliieleza kwa uwazi wote bila maficho yoyote.
Lakini alipokutana na kundi la watu ambao hawakuwa na nia ya kujifunza, watu wenye wivu, mafarisayo na waandishi ambao walimkufuru Roho Mtakatifu pamoja na maherodi, alikuwa anatumia mifano ya mafumbo, ili wasielewe chochote. Na alipokuwa peke yake alihakikisha anawafunulia mafumbo hayo wale ambao walikuwa na kiu ya kuujua ukweli.
Mathayo 13:13 “Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa.14 Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona.15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya”.
Mathayo 13:13 “Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa.
14 Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona.
15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya”.
Hivyo mfumo huu hata sasa Bwana anautumia rohoni.. ukiwa kweli na nia ya kumjua Mungu, atakufundisha sana, na kutumia hata mifano halisi ya kimaisha ili mradi tu ahakikishe unayaelewa mapenzi yake, vema na kwa ufasaha wote. Lakini ikiwa mwovu, na unajifanya unamjua Mungu, ukweli ni kwamba hutamwelewa, atakuja kwako kwa mafumbo mengi tu.. Utakuwa kila siku ni mtu wa kutomwelewa Mungu, na kumtumikia kidini tu.
Bwana Yesu atusaidie tuwe na kiu ya kweli kwake. Kwasababu hii biblia haijakusudiwa kila mtu aielewe bali wale wenye nia tu ya dhati kwa Bwana..walio maskini wa roho.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
KWA WALE WALIO NJE “YOTE” HUFANYWA KWA MIFANO
MPENDEZE MUNGU ZAIDI.
Kwa aibu yako mwenyewe, na kwa aibu ya uchi wa mama yako.
MAKABURI YAKAFUNUKA; IKAINUKA MIILI MINGI YA WATAKATIFU WALIOLALA;
Ni kwanini Yesu alisema “Na wakisikia wasikie, wasielewe Wasije wakaongoka?”
Biblia inamaana gani iliposema “Dhambi ilipozidi, Neema ilizidi kuwa nyingi Zaidi”.
KUOTA UNAPEWA PESA, KUNA MAANISHA NINI?
Rudi nyumbani
Print this post
Napenda sana mafundisho yenu , ninawafwadilia kila wakati na nimeparikiwa tena sana. Mungu awe nanyi daimaa.