Swali: Katika 1Wakorintho 7:36 Mtume Paulo anafundisha kuwa Mtu akiona hamtendei vyema mwanamwali wake basi aruhusu waoane”.. Je alikuwa ana maana gani kusema hivyo? (Au kwa ujumla mstari huo unamaanisha nini)?.
Jibu: Labda tuanze kusoma kuanzia juu kidogo mstari wa 34.
“1Wakorintho 7:34 “Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.35 Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine.36 Lakini mtu awaye yote akiona ya kuwa hamtendei mwanamwali wake vipendezavyo, na ikiwa huyo amepita uzuri wa ujana wake, na ikiwapo haja, basi, afanye apendavyo, hatendi dhambi, na awaruhusu waoane.37 Lakini yeye aliyesimama kwa uthabiti wa moyo wake, hana sharti, lakini aweza kuyatawala mapenzi yake, tena amekusudia moyoni mwake kumlinda mwanamwali wake, atatenda vema.38 Basi, hivyo na amwozaye mwanamwali wake afanya vema; na yeye asiyemwoza atazidi kufanya vema.”
“1Wakorintho 7:34 “Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.
35 Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine.
36 Lakini mtu awaye yote akiona ya kuwa hamtendei mwanamwali wake vipendezavyo, na ikiwa huyo amepita uzuri wa ujana wake, na ikiwapo haja, basi, afanye apendavyo, hatendi dhambi, na awaruhusu waoane.
37 Lakini yeye aliyesimama kwa uthabiti wa moyo wake, hana sharti, lakini aweza kuyatawala mapenzi yake, tena amekusudia moyoni mwake kumlinda mwanamwali wake, atatenda vema.
38 Basi, hivyo na amwozaye mwanamwali wake afanya vema; na yeye asiyemwoza atazidi kufanya vema.”
Hapa Paulo kwa kuongozwa na roho anatoa USHAURI WA KITUME, juu ya watu wanaotaka kuoa na wale wasiotaka kuoa, au wa wale wanaotaka kuolewa na wasiotaka kuolewa.
Ukisoma kuanza juu zaidi utaona anashauri kuwa ni “Ni heri mtu akae bila kuoa kabisa, au kutoolewa kabisa kwaajili ya Bwana, kuliko kuoa au kuolewa”.. lakini hiyo sio sharti au Amri, bali chaguzi la mtu!!. Maana yake ni kuwa Mtu atakayeoa atakuwa hafanyi dhambi, na vile vile atakayeolewa atakuwa hafanyi dhambi… Lakini mtu ambaye atakaa bila kuoa au kuolewa, huyo ana faida mara nyingi zaidi kwasababu atakuwa atajishughulisha zaidi na mambo ya Mungu pasipo kuvutwa, au kusongwa na mambo mengine ya kifamilia.
1Wakorintho 7:32 “Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe”
1Wakorintho 7:32 “Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;
33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe”
Lakini Paulo hajaishia tu kutoa ushauri kwa Watu wanaotaka kuoa au kuolewa, bali alienda mpaka kwa wazazi wenye mabinti majumbani kwao ambao ni mabikira (wanawali).
Akashauri kuwa ikiwa Mzazi, anaye binti au mabinti ambao bado hawajaolewa, Na mzazi huyo anatamani mabinti wake wamtumikie Mungu pasipo kuvutwa na mambo mengine, zaidi sana na yeye mwenyewe ana uwezo wa kuyatawala mapenzi yake (Yaani sio kigeugeu, cha kutamani kupata wajukuu au kuitwa mkwe), basi anaweza kuwadumisha wanawe (mabinti wake) katika kuishi maisha ya kutotamani kuolewa, ili wamtumikie Mungu vyema, pasipo kuvutwa na mambo mengine..kama wale mabinti wane wa Filipo waliokuwa manabii, wanatabiri..
Matendo 21:8 “Asubuhi yake tukaondoka, tukafika Kaisaria, tukaingia nyumbani mwa Filipo, mhubiri wa Injili, aliyekuwa mmoja wa wale saba, tukakaa kwake.9 Mtu huyu alikuwa na binti wanne, mabikira, waliokuwa wakitabiri”.
Matendo 21:8 “Asubuhi yake tukaondoka, tukafika Kaisaria, tukaingia nyumbani mwa Filipo, mhubiri wa Injili, aliyekuwa mmoja wa wale saba, tukakaa kwake.
9 Mtu huyu alikuwa na binti wanne, mabikira, waliokuwa wakitabiri”.
Kuwalea mabinti kwa namna hiyo kuna faida kubwa sana…kwasababu biblia inasema katika Mithali 22: 6 “Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee”. Ikiwa na maana kuwa msingi ambao mtoto wako utakaomwekea tangia akiwa mdogo huo hawezi kuuacha mpaka atakapokuwa mtu mzima. Na msingi mmojawapo ambao ni mzuri ndio huo wa Kutokuja kuolewa/kuoa, ili kusudi wamtumikie Mungu pasipo kuvutwa na mambo mengine, katika siku za mbeleni.
Sasa Paulo hajatoa amri kwamba ni lazima wazazi wote wafanye hivyo kwa mabinti zao… bali ni “Ushauri tu wa kitume anaoutoa”.. Lakini pia anaendelea kusema, ikiwa mzazi anaona kuwa binti yake (Mwanamwali wake), hamtendei jinsi ipasavyo (maana yake binti yake anatamani kuolewa na yeye mzazi ni kikwazo) basi hapaswi kuendelea kumshikilia huyo binti kwa kumzuia kuolewa, bali amruhusu aolewe, na kwa kufanya hivyo pia atakuwa hatendi dhambi..
1Wakorintho 7:36 “Lakini mtu awaye yote akiona ya kuwa hamtendei mwanamwali wake vipendezavyo, na ikiwa huyo amepita uzuri wa ujana wake, na ikiwapo haja, basi, afanye apendavyo, hatendi dhambi, na awaruhusu waoane.37 Lakini yeye aliyesimama kwa uthabiti wa moyo wake, hana sharti, lakini aweza kuyatawala mapenzi yake, tena amekusudia moyoni mwake kumlinda mwanamwali wake, atatenda vema.38 Basi, hivyo na amwozaye mwanamwali wake afanya vema; na yeye asiyemwoza atazidi kufanya vema”.
1Wakorintho 7:36 “Lakini mtu awaye yote akiona ya kuwa hamtendei mwanamwali wake vipendezavyo, na ikiwa huyo amepita uzuri wa ujana wake, na ikiwapo haja, basi, afanye apendavyo, hatendi dhambi, na awaruhusu waoane.
38 Basi, hivyo na amwozaye mwanamwali wake afanya vema; na yeye asiyemwoza atazidi kufanya vema”.
Ni nini tunajifunza?
Kama mzazi, mojawapo ya mafundisho au msingi wa kuwawekea wanao ni pamoja na huo wa kutafakari au kufikiri kutokuja kuoa au kuolewa huko mbeleni (kwaajili ya Bwana).. Kumbuka “sio kumzuia mwanao kuoa au kuolewa” la! bali kumfundisha au kumwekea msingi huo, ili atakapokuja kufikia umri wake mwenyewe aone kila sababu za yeye kuishi kama alivyo kwaajili ya Bwana na utumishi wake..
Ushauri huu unaweza kuonekana kama mpya na wa ajabu lakini ndio ushauri wa kitume. (Paulo, aliye baba yetu wa kiroho alilihakiki hilo kwa msaada wa roho) hivyo na sisi tukitaka tupate faida nyingi za kiroho basi tusikilize ushauri huo. Lakini si Lazima, wala si sharti.(hatujalazimishwa)
1Timotheo 2:7 “Nami kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mhubiri na mtume, (nasema kweli, sisemi uongo), mwalimu wa Mataifa katika imani na kweli”.
Bwana akubariki.
Ikiwa kama unapenda kujua zaidi kama ni Sharti mchungaji kuoa au kutokuoa katika utumishi wake basi unaweza kufungua hapa>> Je! Mtu ambaye hajaoa anaruhusiwa kulichunga kundi?
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
JE NI HALALI KUOA WAKE WENGI, AU KUTOA TALAKA?
Wanafunzi wa Yesu, walimaanisha nini kusema kama “Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa”?
Biblia imemaanisha nini iliposema “hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu”
Hapo ndipo, atakapompa Mungu Baba ufalme wake.
JE BIKIRA MARIAMU ALIKUFA?
Rudi nyumbani
Print this post
Naomba niwe kwa group ya what’s up