Kudhili ni kufanya nini?

Kudhili ni kufanya nini?

Swali: Kudhili ni nini, au mtu aliyedhiliwa anakuwaje?

Jibu: Kudhili maana yake ni “kushusha chini” Mtu aliyeshushwa chini maana yake “kadhiliwa”.

Katika biblia, maandiko yanaonesha kuwa Mungu huwadhili watu wote wanaojikweza, na wenye kiburi..na wale wote wanaojishusha (yaani wanaojidhili) basi yeye huwakweza, kwa kuwapandisha juu!!.

Mathayo 23:11  “Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu.

12  Na ye yote atakayejikweza, atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili, atakwezwa”

Ayubu 40:11 “Mwaga mafuriko ya hasira zako, Ukamtazame kila mtu mwenye kiburi, ukamdhili”.

Zaburi 75:7 “Bali Mungu ndiye ahukumuye; Humdhili huyu na kumwinua huyu”.

Unaweza kusoma pia juu ya Neno hilo katika Zaburi 107:39, na Wafilipi 4:12.

Hivyo na sisi hatuna budi kujishusha siku zote mbele za Mungu, na mbele za watu ili Bwana atukweze.. Kwasababu Mungu hapendi watu wanaojiinua, na wenye majivuno na wanaojiona wao ni bora kuliko wengine wote.

Luka 18:9  “Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote.

10  Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru.

11  Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.

12  Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote.

13  Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.

14  Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa”

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA PILI WA YOHANA.

NI MAONO YAPI HAYO UNAYOSUBIRIA?

JE UNA MATUMAINI YA KUPATA TENA KILE ULICHOPOTEZA?

Nini maana ya kuabudu malaika? (Wakolosai 2:18)

USIWE NA HOFU, USHUKAPO CHINI.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Leave a Reply