Mnanaa, Bizari na Jira ni viungo gani? (Mathayo 23:23)

Mnanaa, Bizari na Jira ni viungo gani? (Mathayo 23:23)

Swali: Hivi viungo tunavyovisoma katika Mathayo 23:23, ni viungo gani na vina ujumbe gani kiroho?

Jibu: Tusome

Mathayo  23:23 “ Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za MNANAA na BIZARI na JIRA, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.

24  Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia”.

Hapa tunaona ni viungo vitatu vimetajwa ambavyo ni; Mnana, Bizari na Jira. Tutazame kiungo kimoja baada ya kingine.

1.MNANAA:

Mnanaa ni aina ya majani ambayo yanatumika kama tiba ya magonjwa ya tumbo na kinywa. Asilimia kubwa ya dawa za Meno zinazotumiwa na wengi zinatengenezwa kwa majani haya ya mnanaa, pamoja na karafuu… watu hutumia majani ya mnanaa katika kimiminika kama chai mfano wa (mchaichai unavyowekwa) na kuuchemsha pamoja na kisha kunywa.. ambapo inasaidia  kupunguza harufu ya kinywa, kuua bacteria mdomoni.

Pia Mimea ya Mnanaa ulitumika na unatumika hata sasa kusafisha tumbo, na kutibu vidonda vya tumbo, na kuondoa gesi tumboni. Zao hili ni zao kongwe ambalo lilitumika enzi na enzi, na lilikuwa ni zao la biashara, ingawa upatikanaji wake haukuwa mgumu.

2. BIZARI:

Bizari ni aina nyingine ya Mmea, ambayo majani yake yanatumika kama Kiungo cha kuongeza ladha katika chakula, na pia faida yake katika mwili ni kupunguza magonjwa ya moyo. (Tazama picha chini)

3. JIRA:

Jira ni kiungo ambacho ni maarufu zaidi kuliko viungo viwili vilivyotangulia.. Kiungo hiki ni kiungo kinachowekwa katika baadhi ya vyakula kama Wali, Mikate na Maandazi kwaajili ya kuongeza ladha na pia kupunguza kiwango cha mafuta mwilini. (Tazama picha chini).

Sasa kwanini Bwana Yesu aseme “Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za MNANAA na BIZARI na JIRA,” Ni kwasababu viungo hivi vilikuwa vinapatikana kirahisi sana na pia havikuwa vya gharama kubwa.. ni sawa tu na zao la Mchai chai, ambalo yeyote anaweza kulipanda nyumbani mwake, si kama maharage ambayo upatikanaji wake ni lazima ukayanunue tena kwa gharama kubwa.

Mazao haya katika maeneo ya Mashariki ya kati yanapatikana kirahisi sana, na hata mtu akiyalima na kuyapeleka sokoni basi faida yake si kubwa ni ndogo sana, kuliko mazao yote, kwahiyo hata zaka yake ni ndogo sana..

Sasa Mafarisayo wenyewe walikuwa wanahakikisha wanatoa ZAKA hata kwa viungo vidogo kama hivyo..hawaachi hata senti, ni waaminifu katika kulipa zaka.. Sasa ndio Bwana Yesu akawaambia, mambo hayo wanayoyafanya ni mazuri, (yaani kuzingatia kulipa zaka bila kuiba chochote, hata kama ni kidogo) lakini pia pamoja na kuwa waaminifu katika kulipa zaka, wanapaswa pia wasiyaache mambo mengine ya msingi kama Rehema, Adili na Imani.. Vinginevyo watakuwa ni wanafiki.

Kwasababu haitakuwa na maana kama Utakuwa mwaminifu katika kulipa Zaka, halafu huna Rehema, au Msamaha au Imani au Upendo.. Vyote hivyo vinapaswa viende sambamba.

Ni nini tunajifunza hapo?

Na sisi pia hatuna budi kufanya mambo yote sawasawa yaani kufanya mambo ya sheria kama Imani, Adili, Upendo, Utakatifu, uaminifu, utu wema n.k lakini pia ni lazima  KULIPA ZAKA kwa uaminifu bila kuiba chochote, Ndicho Bwana Yesu alichokuwa anakimaanisha hapo kwa Mafarisayo pamoja na sisi pia..

Swali ni Je! unalipa Zaka?..(Fahamu kuwa Zaka si agizo la agano la kale pekee bali pia ni la agano jipya, na lililoelekezwa na Bwana Yesu mwenyewe) Kama hulipi basi fahamu kuwa unaenda kinyume na hilo andiko la Mathayo 23:23, kwasababu hapo Bwana Yesu hapo kaelekeza kwamba ni lazima tulipe Zaka. Vile vile ni lazima tufanye mambo sheria kama Rehema, imani, adili na upendo.. Mambo haya yote ni lazima yaende sambamba.

Bwana Yesu akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

IPELEKE SADAKA YAKO MAHALI SAHIHI, ILI UBARIKIWE.

JE! KUNA UMUHIMU WOWOTE WA KULIPA ZAKA?

UTARATIBU WA KUTOA FUNGU LA 10 UPOJE?.

NAFASI YAKO NI IPI KATIKA MWILI WA KRISTO?

Maherodi walikuwa ni akina nani, Na kazi yao ilikuwa ni ipi?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Leticia devine
Leticia devine
1 month ago

Wow! Nimejifunza vitu ambavyo nilikuwa sifahamu hasa hio mimea japo nilikuwa naiona, ubarikiwe kwa ufafanuzi🙏