SWALI: Nini maana ya huu mstari?
Mithali 25:23 Upepo wa kusi huleta mvua; Vile vile asingiziaye huleta uso wa ghadhabu.
JIBU: Maandiko yanasema Upepo wa kusi huleta mvua, hapo hasemi ‘upepo’ huleta mvua hapana bali anasema ‘Upepo wa kusi’, Maana yake ni kuwa kila aina ya upepo hubeba tabia yake, kwa mfano upepo wa Kaskazi, hauleti mvua, bali unaleta joto. Vivyo hivyo na pepo nyingine zote, hubeba tabia zao.
Hii ni kufunua nini?
Na sisi wanadamu huwa tunavumisha pepo zetu..Na ndio maana utasikia Neno “UVUMI” wa jambo Fulani, na taarifa hizo husambazwa kwa maneno ya vinywa vyetu, Hivyo kila jambo unalolitoa na kulipeleka kwa mtu mwingine au kwa jamii, huo ni upepo, na ni lazima uwe makini nao sana, kwasababu mwisho wa siku ni lazima ulete faida au madhara.
Na ndio maana hapo katika sehemu ya pili ya mstari huo anasema.. “Vile vile asingiziaye huleta uso wa ghadhabu”. Kusingizia ni neno linalojumuisha usengenyaji, au mtu anayechukua taarifa siziso za kweli na kuzipeleka kwa mwingine, Watu kama hawa, mwisho wa siku watavuna ghadhabu tu, au kuchukiwa, au kusababishiwa madhara na wale waliotolewa taarifa zao. Kwasababu kila uvumi unamatokeo yake.
Lakini tukiwa watu wa kupeleka habari njema, watu wa kuhubiri habari za Kristo, Maana yake ni kuwa Upepo tunaovumisha ni wa heri sikuzote, hivyo tufahamu kuwa mwisho wake utakuwa ni mzuri, utatuletea neema badala ya ghadhabu, kupendwa badala ya kuchukiwa, kusaidiwa badala ya kufukuzwa.
Hivyo tuwe makini na taarifa, au maneno yanayotoka katika vinywa vyetu, biblia inasema..
1 Petro 2:1 Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote. 2 Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;
Epuka masengenyo, na kuwazungumzia wengine vibaya.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Kuwaogopa wanadamu huleta mtego,(Mithali 29:25)
NA UPEPO WA KUSI ULIPOANZA KUVUMA KIDOGO,
JIPE NAFASI KATI YA TAARIFA UNAYOIPOKEA NA MAAMUZI UNAYOYATOA.
Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela.
Kwanini mtu afanye miujiza na bado asiende mbinguni?
About the author