Wakolosai 3:5 inamaana gani?

Wakolosai 3:5 inamaana gani?

SWALI: Wakolosai 3:5 inamaana gani?. Tofauti kati ya tamaa mbaya na kutamani ni ipi?


JIBU: Wakolosai 3:5 Inasema..

  “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;”

Hapo anaanza kwa kusema vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi. Ikiwa na maana kuwa kuna viungo vya duniani ambavyo kazi yake kimsingi ni kutimiza mapenzi ya duniani (ya shetani). Tofuati na vile vya ki mbinguni ambavyo vinatimiza mapenzi ya Mungu. Viungo hivi sio mikono, miguu, macho, masikio au pua hapana, bali viungo vya rohoni.

Viungo vya kimbinguni vimeelezwa kwenye mstari wa 12-17. Lakini vya duniani ndio hivi vinavyozungumziwa hapa katika mstari wa 5, ambavyo tunapaswa tuviue. Navyo ni;

1) Uasherati.

Uasherati unajumuisha kitendo chochote cha zinaa nje ya ndoa pamoja na mambo yafanywayo kinyume na asili. Ikiwemo Uzinzi, ufiraji, na ulawiti. Vitu hivi havipaswi vipewe nafasi kwa mtakatifu yoyote.

2) Uchafu

Uchafu ni kinyume na usafi. Mtu mchafu kimsingi anakuwa amebeba takataka katika mwili wake. Vivyo hivyo, mtu ambaye anaruhusu takataka za hii dunia zimtawale ni mchafu kiroho. Mfano wa takatakata hizi ni miziki ya kidunia, anasa, matusi, ulevi, kubeti, mazungumzo yasiyofaa, kutazama vitu visivyojenga mitandaoni, ushabiki n.k. Epuka kujitia unajisi na vitu vya ki-ulimwengu.

3) Tamaa mbaya.

Kuzipa tamaa za mwili nafasi ya kukutawala. Na matokeo ya tamaa hizi mbaya kukutawala ndani yako, utaishia, ni kutazama picha chafu, muda wote kuwa na mazungumzo ya kizinzi, kuchat na jinsia tofauti na wewe kusikokuwa na sababu, kuvaa mavazi ya namna hiyo au kujiwekwa kimwili uvutie uzinzi kwa mwengine. Tabia hizi ndani yako unapaswa uziue.

4) Mawazo mabaya.

Mawazo mabaya ni kinyume cha mawazo mazuri. Mtu mwenye mawazo mazuri huwaza yaliyo mazuri, ya kujenga. Lakini mwenye mawazo mabaya sikuzote ni kubomoa. Mawazo hayo ni pamoja na wivu, rushwa, uongo, wizi, uuaji, unafki, visasi,. Hivi havipaswi kuonekana ndani ya mkristo.

5) Kutamani.

Kutamani kunakozungumziwa hapa sio kule kwa tamaa za mwili, hapana, bali tamaa ya mambo ya kidunia, mfano tamaa ya kuwa na mali, tamaa ya kufanana na watu wa kidunia, wanamiziki, wanamitindo n.k., na hizo ndizo zinazompelekea mtu, kugeuza vitu hivyo kuwa kama mungu wao, kuvitafuta na kuvisumbukia sikuzote .Na ndio maana mwandishi anamalizia kwa kusema “Ndiyo ibada ya sanamu” maana yake rohoni vinaonekana ni miungu kwao. Jiepushe na kutamani.

Hivyo  tukifanikiwa kuviua viungo hivi, basi mwili hauwezi kuwa na matunda yoyote, kwasababu hakuna kiungo chake hata kimoja kina uhai. Lakini pia anasema,

Wakolosai 3:12  Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,

13  mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.

14  Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.

15  Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.

16  Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.

17  Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.

Hivyo ndivyo viungo vya kimbinguni, Tujitahidi vituvae.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

Uasherati wa Kiroho maana yake nini?

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

Nini maana ya huu mstari “sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje”

WAPENDENI ADUI ZENU, WAOMBEENI WANAOWAUDHI.

Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu?

Nini maana ya mstari huu: (Mtu ambarikiye mwenzake kwa sauti kuu asubuhi na mapema; Itahesabiwa kuwa ni laana kwake.Mithali 27:14 )?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Loanyuni Tarakwa
Loanyuni Tarakwa
1 year ago

Amen. Nikejifunza

Anonymous
Anonymous
1 year ago

Tunashukuru

Anonymous
Anonymous
1 year ago

Ubarikiwe 🙏🤝

MOSES TOM SIMIYU
MOSES TOM SIMIYU
1 year ago

Please add me to your group. I want to be blessed with you brother’s and sisters.