Biblia inasema nini kuhusiana na kuvimba miguu na miguu kuuma?
Kama miguu imevimba na hujui chanzo, wala madaktari hawaoni tatizo…basi huenda ni Mungu anataka kusema na wewe jambo, ambalo ukilirekebisha basi tatizo hilo linaweza kukuisha moja kwa moja..
Hebu tusome maandiko yafuatayo katika biblia..
Nehemia 9:19 “hata hivyo wewe kwa wingi wa rehema zako hukuwaacha jangwani; NGUZO YA WINGU haikuwaondokea wakati wa mchana, ili kuwaongoza njiani; wala NGUZO YA MOTO haikuondoka wakati wa usiku, ili kuwapa mwanga na kuwaonyesha njia watakayoiendea.
20 Ukawapa na roho yako mwema ili kuwaelimisha, wala hukuwanyima mana vinywani mwao, tena ukawapa maji kwa ajili ya kiu yao.
21 Naam, muda wa miaka arobaini uliwaruzuku jangwani, wasihitaji kitu; nguo zao hazikuchakaa, wala MIGUU YAO HAIKUVIMBA”
Wana wa Israeli walipokuwa jangwani, Nguzo ya Wingu, Na nguzo ya Moto ambayo ni ufunuo wa ROHO MTAKATIFU juu yao, ambaye aliwaongoza kama ROHO MWEMA, katika njia yao..
Ikiwa na maana kuwa njia waliyokuwa wanaiendea ilikuwa ni njia sahihi waliyoongozwa na Roho wa Mungu ndio maana miguu yao HAIKUVIMBA!, lakini wangeenda njia nyingine tofauti na hiyo ya Roho Mwema, basi ni wazi kuwa miguu yao Ingevimba, hata kama wangekuwa hawatembei, wamekaa tu, bado ingevimba.
Kwahiyo na wewe kama unaona miguu yako imevimba, na hujui chanzo na wala huoni dalili ya kupona, huenda upendo wa Mungu unakukumbusha kuwa umtafute Roho Mtakatifu, kwani yeye ndiye atakayeyaongoza maisha yako ya kiroho, maumivu hayo ni ishara ya upendo wa Mungu kwako kutaka kukupa zawadi ya Roho wake Mtakatifu, akuongoze katika njia sahihi.
Sasa utampataje Roho Mtakatifu?
Utampata kwa kanuni ifuatayo..
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.
40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi”.
Tubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha, kisha tafuta ubatizo sahihi na Bwana atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu.
Maran atha.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
TATIZO LA VISIGINO KUUMA KIBIBLIA
TATIZO LA NDANI LINALOWASUMBUA VIJANA, WALIOOKOKA.
Je! Bwana Yesu alisulubiwa juu ya msalaba au juu ya mti uliokuwa wima?
Vihekalu vya fedha vya Artemi vilikuwaje? (Matendo 19:24).
About the author