Yakobo 3:11 “Je! Chemchemi katika jicho moja hutoa maji matamu na maji machungu?”
“Jicho” linalozungumziwa hapo sio “jicho” lililo kiungo cha mwanadamu kinachotumika kutazama bali ni chemchemi ya maji.
Ukiendelea mbele kidogo mstari wa 12, Mtume Yakobo kafafanua Zaidi..
Yakobo 3:12 “Ndugu zangu, Je! Mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? Kadhalika chemchemi haiwezi kutoa maji ya chumvi na maji matamu”.
Jambo ambalo ni kweli kabisa, huwezi kukuta mto unatiririsha maji ya chumvi, na muda huo huo unatiririsha maji yasiyo na chumvi.
Kadhalika na sisi hatuwezi kuwa wema wakati ndani ni waovu..Bwana Yesu alizidi kuliweka hili wazi katika Mathayo 12:34.
Mathayo 12:34 “Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake. 35 Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya”
Mathayo 12:34 “Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.
35 Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya”
Kumbe mioyo yetu ni visima, na tena ni visima vinavyotoa Maji, na maji hayo ni aidha Matamu au Machungu.
Mtu aliyejawa na Roho Mtakatifu kisima chake kinatoa maji Matamu tena ya Uzima..
Yohana 4:14 “walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele”
Lakini kinyume chake mtu asiye na Roho Mtakatifu kisima cha moyo wake kinatoa maji machungu.
Je umemwamini Yesu na kutubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha?..Na je umebatizwa ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Mwokozi Yesu?
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
NI WAPI UTAKUTANA NA MALAIKA WA BWANA?
TAA YA MWILI NI JICHO,
Bwana alimaanisha nini kusema “kila mtu atatiwa chumvi kwa moto”
Ni kwa namna gani Kristo analitakasa kanisa kwa Maji katika Neno? (Waefeso 5:26)
Utakapoketi kwa chakula pamoja na mtawala Mwangalie sana
Rudi nyumbani
Print this post