SWALI: Naomba kufahamu maudhui iliyo nyuma ya Luka 17:10 inayosema..
[10]Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.
JIBU: Kufahamu kwanini Yesu aliwaambia wanafunzi wake maneno hayo. Ukianzia juu utaona ni kufuatana na swali walilomuuliza kuhusiana na IMANI. Walimfuata na kumwomba awaongezee Imani.
Lakini Yesu aliwajibu na kuwaambia kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali mngeuambia mkuyu huu ng’oka ukapandwe baharini nao ungewatii.
Luka 17:6
[6]Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng’oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii.
Akimaanisha kuwa sio suala la kuongezewa Imani, ili mweze kufanya makubwa, bali kile kidogo sana kinaweza tenda yote. Na kidogo hicho mitume walikuwa nacho ndani yao, ambacho hata mimi na wewe tunacho. Isipokuwa hawakujua namna ya kukitoa.
Ndipo Yesu akaendelea kuwaambia kwa mifano sasa, ili jambo hilo litokee, kanuni yake ni kuwa wanapaswa wawe kama watumwa wasiokuwa na faida kwa Bwana wao. Sasa kwa namna gani? fuatilia mfano wenyewe…
Luka 17:7-10
[7]Lakini, ni nani kwenu mwenye mtumwa alimaye au achungaye ng’ombe, atakayemwambia mara arudipo kutoka shambani, Njoo upesi, keti, ule chakula? [8]Je! Hatamwambia, Nifanyie tayari chakula, nile; jifunge unitumikie, hata niishe kula na kunywa, ndipo nawe utakapokula na kunywa? [9]Je! Atampa asante yule mtumwa, kwa sababu ameyafanya aliyoagizwa? [10]Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.
[7]Lakini, ni nani kwenu mwenye mtumwa alimaye au achungaye ng’ombe, atakayemwambia mara arudipo kutoka shambani, Njoo upesi, keti, ule chakula?
[8]Je! Hatamwambia, Nifanyie tayari chakula, nile; jifunge unitumikie, hata niishe kula na kunywa, ndipo nawe utakapokula na kunywa?
[9]Je! Atampa asante yule mtumwa, kwa sababu ameyafanya aliyoagizwa?
Mfano huo unajieleza, zamani mtumwa aliponunuliwa hakuwa anafanya kazi kama mwajiriwa, bali kama mnyama tu mfano wa punda ambapo kazi yake ilikuwa ni moja tu kumuhudumia Bwana wake, na sio kujitafutia maisha.
Sasa hapo Yesu anatumia mfano wa huyo Bwana mwenye mtumwa wake ambaye amemweka kuwa mkulima wa shamba lake, ambaye asubuhi huondoka jioni hurudi kwa Bwana wake.
Anasema, je atakaporudi atamwambia kaa hapo upumzike? wakati mimi bado sijala? Ni wazi kuwa ataongezewa majukumu, mpaka ahakikishe Bwana wake ameshiba, hana mahitaji tena ndipo sasa na yeye apewe nafasi ya kupumzika na kula.
Hivyo Yesu alitumia mfano huo, kuwaambia wanafunzi wake, jinsi na wenyewe wanavyopaswa kuwa kwa Mungu.
“[10]Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.”
Akiwa na maana, mkihitaji hilo jambo la IMANI mjaliwe, yawapaswa muwe kama watumwa wasiokuwa na faida. Mtumikieni kwanza Bwana wenu sana, kama watu wasiotazamia malipo yoyote.
Ukihubiri sana miaka ishirini, unatanga na jua huoni faida yoyote iliyoongezeka kwenye maisha yako, huoni maendeleo yoyote. Usimuulize Bwana mbona hujanipa chochote mpaka leo. kuwa kama mtumwa asiye na faida.
Huu ndio utumishi Bwana anaoutaka kwetu, leo hii wahubiri wengi, watumishi wengi, wachungaji wengi wamepoa, wamerudi nyuma kwasababu walitazamia malipo kutoka kwa Bwana katika kwa kile walichokuwa wanakifanya, na waliopoona hawapati, kinyume chake maisha yao ndio yanakuwa magumu, wakaacha utumishi wakaenda kutafuta mambo yao.
Ndugu ni lazima tuelewe kanuni za Mungu wetu. Ikiwa unaenda kuifanya kazi ya Bwana ili ukusanye sadaka, upate unafuu kimaisha..Ni heri ukaacha ukatafute biashara nzuri uwekeze nguvu zako huko. Mungu anaweza asikupe chochote kwa miaka mingi, unataabika tu, je utaendelea kumtumikia?
tukubali kuwa watumwa wasio na faida. Akitupa sawa, asipotupa sawa. Lakini tujue kuwa sikuzote anatuwazia yaliyo mema.
Ujumbe wa Bwana hapo ni kwamba tukitaka imani itoke tuwe watumwa wa namna hii.
Shalom
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Ni kosa gani lililowafanya wana wa israeli wawe watumwa miaka 400 Misri?.
Tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu.
Nawiwa na Wayunani na wasio Wayunani.
Rudi Nyumbani
Print this post