Ni dhiki ipi hiyo watu walio kwenye ndoa huipata sawasawa na 1Wakorintho 7:28?

Ni dhiki ipi hiyo watu walio kwenye ndoa huipata sawasawa na 1Wakorintho 7:28?

1Wakorintho 7:28  Lakini, kama ukioa, huna hatia; wala mwanamwali akiolewa, hana hatia; lakini watu kama hao watakuwa na dhiki katika mwili nami nataka kuwazuilia hayo.

Awali ya yote katika vifungu hivi, Mungu hashinikizi kwamba watu  wasioe au wasiolewe.  Ndoa ni jambo jema, na lina faida nyingi sana katika maisha na pia katika huduma, kwasababu humsaidia mtu akae mbali na uzinzi na tamaa mbaya, (1Wakorintho 7:2). Pia huondoa upweke (Mwanzo 2:18), wawili wawapo mwili mmoja, ni nguvu zaidi na faraja.

Lakini Mungu anatoa pia uchaguzi, kwa mtu ikiwa anao uwezo wa kujizuia yaani kutawala hisia zake (1Wakorintho 7:9), akaishi hivyo hivyo, bila shida yoyote, ni vema zaidi kihuduma. Kwasababu humfanya asisongwe na mambo mengi ya kindoa.

Kwasababu mtu aliye kwenye ndoa ni wazi kuwa upendo wake utagawanyika kwa sehemu, biblia inasema atatafuta ampendezeje mume/mke wake.

1Wakorintho 7:32  Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;

33  bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe.

Lakini pia atakutana na dhiki, zinazoambatana na ndoa. Kwamfano kutatua migogoro ya kifamilia,  malezi ya watoto, kuwagharamikia, kuwasomesha,matibabu, kuwafuatilia, kuivisha familia yako, na mambo kama hayo. Ni dhiki ambazo, zinaongezeka, na hivyo hutinga ufanisi wako kwenye utendaji kazi wa injili.  Paulo huiita “shida iliyo” sasa. Yaani Kusalitiana, upendo kupoa, kupishana,  ni vitu ambavyo mara kwa mara hujitokeza katika maisha ya ndoa.

1Wakorintho 7:26  Basi, naona hili kuwa jema, kwa ajili ya shida iliyopo, kwamba ni vema mtu akae kama alivyo.

27  Je! Umefungwa kwa mke? Usitake kufunguliwa. Umefunguliwa? Usitafute mke

Hivyo kihuduma mtu ambaye hajaoa/kuolewa, hujipunguzia dhiki, kuliko yule aliye kwenye ndoa. Hiyo haimaanishi kuwa aliye kwenye ndoa hawezi kutenda kazi vizuri, hapana kazi anaweza itenda hata zaidi ya Yule ambaye hajaoa, isipokuwa tu kwake dhiki na shida zitaongezeka.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MASWALI NA MAJIBU: YAHUSUYO NDOA

NDOA TAKATIFU NI MKE MMOJA/MUME MMOJA.

NATAKA REHEMA, WALA SI SADAKA!

Ni kweli Paulo alipuuzia maonyo aliyopewa ya kwenda Yerusalemu?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments