Kitabu cha Matendo ya mitume hakimtaji moja kwa moja mwandishi wake, lakini tunaweza kumtambua, kutokana na utambulisho wake mwanzoni mwa waraka huo, kwamba ni LUKA. Kwasababu waraka huu aliulekeza kwa mtu mmoja aliyeitwa Theofilo, ambaye anamtaja pia alimtumia waraka wa kwanza uliozungumzia habari za Yesu tangu mwanzo hadi siku alipochukuliwa juu, na huu si mwingine zaidi ya waraka wa Luka. Soma Luka. (1:1-3)
Ndio maana inaaminika aliyeandika waraka huu ni Luka.
Matendo 1:1 Kitabu kile cha kwanza nalikiandika, Theofilo, katika habari ya mambo yote aliyoanza Yesu kufanya na kufundisha,
2 hata siku ile alipochukuliwa juu, alipokuwa amekwisha kuwaagiza kwa Roho Mtakatifu wale mitume aliowachagua;
3 wale aliowadhihirishia nafsi yake, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, ya kwamba yu hai, akiwatokea muda wa siku arobaini, na kuyanena mambo yaliyouhusu ufalme wa Mungu.
Kitabu hichi cha matendo ya mitume, kama jina lake linavyojieleza kinaeleza hasaa jinsi mitume wa Bwana walivyoanza kulitekeleza lile agizo kuu la Yesu alilowaambia wakahubiri injili kwa kila kiumbe. Tangu Yerusalemu, uyahudi, samaria na dunia nzima.
Kinatufundisha jinsi Roho Mtakatifu alivyowaongoza hadi kukamilisha jukumu hilo la injili ulimwenguni mwote kwa mafanikio makubwa.
Na mambo ambayo tunajifunza kwao ni haya:
Umoja: Hawakuwa na nia tofauti tofauti, bali moja ya Kristo, walikubali kudumu katika fundisho la mitume bila shuku yoyote. Walifanya yote kwa ushirikiano kwasababu vitu vyote waligawana kama kila mtu alivyokuwa na hitaji lake.
Matendo 4:32 Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika.
Mashauri ya pamoja: Hata mahali ambapo hakukueleweka vema, au kutokea kwa mikanganyiko waliweza kukaa katika Baraza la wazee na mitume, kutafakari kwa pamoja ndipo hekima ya Roho ikaamua yawapasayo kutenda.(Matendo 15: 1-21).Ndio maana hawakuwa na madhehebu.
Furaha ya Roho: Kanisa lilifurahia ibada, na imani ndani ya Kristo. Sio la watu ambao walisukumwa kufanya majukumu yao, bali wote waliona ni raha kumfuata Kristo kwa moyo mweupe.
Matendo 2:46 Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe
Maombi: Mara nyingi walidumu katika maombi, hekaluni, na manyumbani mwao (Watendo 1:14)
Upendo: Walipendana, Waliweza kuwa na vitu vyote shirika, hawakubaguana, wala kuwa na ubinafsi kiasi kwamba hakukuwa na yoyote aliyekuwa na mahitaji ndani ya kanisa.
Matendo 2:44 Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika, 45 wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja
Uvumilivu: Walipitia dhiki, wengine wapigwa mawe, waliburutwa, lakini hawakuitupilia mbali imani, kinyume chake ndio injili walizidi kuihubiri.
Matendo 8:1,4
1 Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume…..4 Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno.Hivyo hayo ni baadhi ya mambo ambayo na sisi tunaweza kujifunza katika kanisa la mwanzo.
Je! Umeokoka?
Kama bado unasubiri nini? Kumbuka hizi ni siku za mwisho. Tubu dhambi zao leo, mwamini Yesu, ukabatizwe akusamehe dhambi zako, Ikiwa utapenda kupata msaada huo wa kumpokea Kristo, basi fungua hapa kwa mwongozo huo >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
About the author