Ni YESU au JESUS au YESHUA
Swali: Je tunapaswa kutumia jina lipi katika maombi na utumishi?..Je tutume YESU (kwa lugha ya kiswahili) au JESUS (kwa lugha ya kingereza) au YESHUA (kiyahudi)?.
Jibu: Moja ya mafundisho yaliyogeuzwa na adui ni pamoja na matumizi ya jina la YESU?.
Lipo kundi linaloamini kuwa jina la “Masihi” linapaswa litamkwe vile vile kama Malaika Gabrieli alitamka kwa Bikira Mariamu, ambalo ni “Yeshua” (ישוע) kiebrania.
Na lipo kundi linaloamini kuwa jina la Masihi linaweza kutafsiriwa katika lugha mbalimbali na kuwa na matokeo yale yale.
Na mfano wa tafsiri hizo mbalimbali ni kama “JESUS” (ambayo ni lugha ya kiingereza)…nyingine ni “YESU” (ambayo ni lugha yetu ya kiswahili).. Na katika lugha nyingine pia jina hilo linatafsirika katika namna nyingine…ambapo likisikika haliwi mbali na ile lile la asili “ Malaika Gabrieli alilomwambia Mariamu Yeshua”.
Sasa swali ni je! Ni sahihi kulitafsiri jina hilo kutoka kiebrania kwenda katika lugha nyingine ikiwemo kiswahili, kama hivi tunavyosema leo YESU?.
Jibu ni Ndio!.. Ni sahihi kabisa na matokeo ya jina hilo yanabaki kuwa yale yale Mungu aliyoyakusudia, ikiwa na maana kuwa mtu anayetaja jina la YESHUA, na yule anayetaja JESUS na yule anayetaja YESU, wote wa wapo sawa…(hakuna ambaye anakosea)…Hapo ni suala la lugha tu!
Sasa utauliza tunalithibitisha vipi hilo kibiblia?.
Tunasoma siku ile ya Pentekoste, Roho Mtakatifu alivyoshuka kwa mara ya kwanza juu ya kanisa, kilichotokea ni watu kusikika wakisema kwa lugha nyingine.
Sasa zile lugha walizokuwa wanazungumza hazikuwa za kimbinguni bali za duniani, (ambazo zinazungumza na jamii mbalimbali za watu) soma Matendo 2:7-11.
Hali kadhalika na maneno yaliyokuwa yanazungumzwa sio makelele, (yasiyo na maana) kwamba mtu akisikiliza haelewi ni kitu gani kinazungumzwa.
Bali ni maneno ya kumwadhimisha na kumtukuza Mungu, kama Roho alivyowajalia….jambo kama hilo pia lilitokea katika nyumba ya Kornelio, soma Matendo 10:46.
Kwahiyo wale waliojaliwa kuzungumza kiyunani, maana yake lugha yao yote ilibadilika na kuwa kiyunani ikiwemo na majina ya Mungu, wasingeweza kuzungumza kiyunani halafu jina “MUNGU” au “YESU” liendelee kubaki vile vile kiebrania, (maana yake vyote vilibadilika, kuanzia maneno mpaka majina).
Vile vile waliojaliwa kusema kirumi siku ile ya Pentekoste na maneno yao yote yalibadilika na kuwa kirumi, ikiwemo jina la Mungu na Yesu.
Na kama kiswahili kingekuwepo pale basi hata jina la YESU lingetajwa na Mungu pia
Hiyo ni kufunua nini?
Ni kufunua kwamba katika agano jipya Bwana Mungu anazikubali lugha zote, na katika mataifa yote jina lake litatajwa na injili itahubiriwa kila Taifa, na kila lugha na kila kabila.
Zaburi 86:9 “Mataifa yote uliowafanya watakuja; Watakusujudia Wewe, Bwana, Watalitukuza jina lako”.
Na hiyo ndio sababu pasipo hata kujua kiebrania, bado pepo wakisikia jina la YESU kwa lugha yetu hii hii ya kiswahili wanaondoka…
Vile vile wakisikia jina la YESU kwa lugha ya kiyunani wanatoka, au kwa lugha ya kingereza JESUS wanahama.
Kwahiyo suala sio tafsiri ya jina suala ni Imani katika hilo jina.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Rudi Nyumbani
Print this post