SWALI: Biblia inamaana gani kusema jivikeni silaha ya nia ile ile? (1Petro 4:1)
1 Petro 4:1-3
[1]Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi.
[2]Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani.
[3]Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;
JIBU: Tukiangalia undani wa hilo neno hapo anaposema silaha ya nia. Ni kutuonyesha kuwa kumbe “Nia ”, inaweza kuwa silaha.
Mara nyingi tunapofikiria silaha kibiblia mawazo yetu moja kwa moja yanakimbilia zile za Waefeso 6:10-18, silaha za haki, kama vile upanga wa Roho ambalo ni Neno la Mungu, chapeo ya wokovu, ngao ya imani, dirii ya haki n.k.
Lakini hapa tunaonyeshwa kuwa ipo pia silaha ndani ya Nia, ambayo nayo tunashauriwa tuwe nayo, kwasababu ilikuwa kwanza ndani ya Kristo.
Na silaha yenyewe ilikuwa ni kukubali kuteswa katika mwili ili kuiua dhambi.
Bwana wetu Yesu Kristo alijua dhambi ina nguvu sana pale mwili unapopewa raha zake. Hivyo aliikubali Nia ya kuteswa, ili dhambi ife.
Kumbuka sababu ya yeye kuchukiwa na watu, kuudhiwa, kuwindwa auawe, kuteswa mpaka kusulubiwa ni kwasababu alitangaza uadui na dhambi, Vinginevyo asingepitia maudhi yale katika mwili. Na tunaona mwisho wake ulikuwa ni ushindi. Kwani kwa kifo chake dhambi ilihukumiwa kabisa kabisa.
Alisema..
Yohana 7:7
[7]Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi; bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu.
Hivyo maandiko yanatuambia na sisi pia, tujivike nia ile ile ya kukubali pia mateso kwa ajili ya Kristo. Kwasababu tukifanya hivyo tunaonyesha kuwa tumeachana na dhambi(tumeihukumu dhambi).
Kwa ufupi ni kuwa ukichukia maisha ya dhambi, tafsiri yake ni kukubali dhiki katika mwili kwa ajili ya Kristo. Hivyo zipende sasa dhiki hizo kama Kristo alivyozipenda, ili dhambi isikutawale. Hiyo ni Silaha kubwa sana.
2 Timotheo 3:12
[12]Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.
kubali shida, kwasababu umeamua kuacha ile biashara haramu, furahia kutengwa na kuonekana mshamba, kwasababu umeamua kuacha mienendo ya marafiki wabaya, penda kupigwa na kufungwa kwasababu unahubiri kweli. Hiyo ndio SILAHA YA NIA. iwezayo kuishinda dhambi.
Ndio maana vifungu vinavyofuata anasema..
“Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani.
[3]Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;
Daima tujivike silaha hii, tukikumbuka kuwa vita vyetu si vikali tena kama vile alivyovipiga Kristo.
Waebrania 12:4
[4]Hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi;
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Kuhubiri injili kwa husuda na fitina ndio kupi?
NDUGU,TUOMBEENI.
DHABIHU ZA ROHO NI ZIPI? (1Petro 2:5)
KIKWAZO CHA EUODIA NA SINTIKE.
Rudi Nyumbani
About the author