Bwana aliposema Maua hayasokoti alimaanisha nini? (Mathayo 6:28).

Bwana aliposema Maua hayasokoti alimaanisha nini? (Mathayo 6:28).

Jibu: Turejee…

Mathayo 6:28 “Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala HAYASOKOTI

29 nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo”

Maana ya kusokota kama inavyozungumziwa hapo ni “kitendo cha kusokota nyuzi na kuunda vazi”.

Zipo nguo/mavazi yaliyotengenezwa kwa kufuma na mengine kwa kusokota nyuzi aidha kwa mkono au mashine.

Kutoka 39:28 “na hicho kilemba cha nguo ya kitani nzuri, na zile kofia nzuri za kitani, na hizo suruali za nguo ya kitani nzuri iliyosokotwa”

Walawi 13:52 “Naye atalichoma moto vazi hilo, kwamba ni lililofumwa au kwamba ni lililosokotwa, kama ni la sufu, au la kitani, au kitu cho chote cha ngozi, ambacho kina hilo pigo ndani yake; kwa maana, ni ukoma unaokula; vazi hilo litachomwa moto”.

Soma pia Walawi 13:58..

Sasa sisi wanadamu ili tuweze kuvaa vazi zuri lililofumwa au kusokotwa ni lazima tufanye kazi za  kujiingizia kipato ili tukanunue mavazi hayo ya kusokota au sisi wenye tusokote kwa mikono yetu au mashine na kujivika…lakini kwa kawaida haiwezekani tule chakula halafu mavazi mazuri ya kusokotwa yatokee mwilini kama vile kucha inavyotokea mwilini…hilo jambo haliwezekani.

Lakini kwa upande wa MAUA ya kondeni hilo linawezekana.. yenyewe hayafanyi kazi yoyote ya kusokota lakini yanavikwa kwa rangi nzuri na za kupendeza ambazo hata Sulemani hakuwahi kuvikwa kama mojawapo ya hayo.

Kadhalika na hali yake mtu amwaminiye Bwana YESU, atakuwa hana haja ya kuhangaika sana kupata mavazi au chakula, kwasababu Bwana anajua anahitaji hayo yote.

Hata ikotokea anapitia vipindi vya kupungukiwa basi huenda ni darasa tu la muda anapitishwa lakini haitaliwa hivyo siku zote.

Mathayo 6:30 “Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?

31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?

32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.

33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa”

Kwa urefu kuhusiana na kuvikwa kwa maua ya kondeni na mfalme Sulemani fungua hapa》》》》Hii ni maana ya Mathayo 6:29 hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Kwanini pawekwe MITI pale bustanini na si kitu kingine?.

Kwanini MUNGU alimzuia Daudi asimjengee HEKALU? (1Nyakati 17:12)

Silwano  ni nani,kama tunavyomsoma kwenye biblia?(1Petro 5:12)

Mwerezi ni nini?

 UNAUELEWA, HISOPO UMEAO UKUTANI?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments